Wednesday, July 20, 2011

WIKI YA MALIASILI KATIKA KUADHIMISHA MIAKA 50

Ukuzaji utalii wa ndani ulenge kutoa elimu ngazi ya Mitaa.

Na Humphrey Shao

IKIWA wizara ya maliasili ipo katika wiki ya kuadhimisha wiki ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika kwa kufanya maonyesho Viwanja vya Mnazimmoja Dar es salaam lakini bado hali ni tete katika kuhamasisha utalii wandani.

Nathubutu kusema hivi kuwa wizara hii imeshindwa kuwa na mipango mathubuti ambayo ingewezesha kusaidia kuhamasisha utalii wa ndani kwa kupitia serikali za mitaa.

Ninasema hivi kwa makusudi kuwa ni lazima wizara hii itambue kuwa serikali za mitaa ndio inayo miliki watu kuanzia ngazi ya chini na ndio inayo wafikia watu kwa urahisi kuliko chombo chochote hivyo kinastaili kipewe nafasi katika kufanikisha malengo la utalii.

Ukiangalia hivi sasa mbinu zinazo tumika kuamasisha utalii wa ndani ni zile zinafanyika kwa wageni katika nchi zilizo endelea wakati aziendani na mfumo wetu wa nchi hii.

Katika taifa letu wenye viti wa mitaa wameshindwa kutumiwa ipasavyo kufikisha ujumbe kwa watu ingali wao wanamadaraka makubwa na nguvu katika jamii inayo tuzunguka.

Sisiti kusema mbinu zinazo tumika katika kuahamasisha utalii wa ndani ni za kisiasa zaidi na kulipana posho kuliko jambo lenyewe na uzito wake.

kwani ukisoma idadi ya nambari ya watalii wa ndani wengi wao ni wale wanafunzi wa shule ya msingi na wachache sekondari ambao wamekuwa wakiburutwa na walimu wao awaelewi chochote na mapato yao ayawezi kutufikisha popote katika taifa hili ambalo linaitaji kutegemea utalii kama sehemu ya uchumi wake.

Hivyo basi endapo tutatumia serikali za mitaa kuhamasisha utalii wa ndani tutaweza kuwafikia wananchi wengi kwa urahi mijini na vijijini hali itakayo saidia kuongeza pato la nchi amabalo limekuwa liki lalamikiwa kushuka kila siku.

Ukizunguka hapa nchini sehemu kubwa ya utalii ipo katika mitaa amabyo inaishi watu lakini watu wa eno hilo awaelewi umuhimu wa sehemu hizo na faida zake katika urithi wa taifa .

kwa mfano mwanafunzi anaweza kumaliza miaka mitatu katika chuo cha usimamizi wa fedha(IFM) bila kuingia makumbusho ya Taifa jinsi gani inavyoo onyesha wizara hiyo kushindwa hata kuwaunganisha wanafuzni wa elimu ya juu kuhusiana na utalii wa ndani.

Hii inadhiirisha uzemebe uliopo kwa watendaji ambao wanapanga mipango yakutoa elimu juu ya utalii wa ndani kwa kuiga mipango ya nchi zilizo endelea.

Ukijaribu kutembelea Maeneo ya Mtae Wilaya ya Lushoto kuna utalii mkubwa unafanyika katika magofu yaliyoachwa na wajerumani lakini wakazi wa eneo hilo awatambui nini kinaendelea katika eneo la na kufurahia wakiona wazungu wakipita barabarani.

Hii inatishia hatari ya kizazi kinacho zaliwa kuafanya uharibifu maeneo hayo kwa kutofahamu umuhimu wake na thamani yake katika historia ya nchi hii kutokana na wizara kushindwa kujipanga kutoa eleimu ya kutosha.

Kufanya maonyesho mijini na aitoshi kusema kuwa mtafanikiwa katika utalii wa ndani bali nguvu ya ziada inahitajika kwa kushirikiana na viongozi wa mitaa kama ilivyo kwa sekta zingine.

Mfano mdogo ni tume ya uchaguzi ambayo wakati wa uchaguzi ukasimu madaraka kwa viongozi hao wa mtaa hali inayoonyesha kupata mafanikio makubwa katika swala hilo ambalo ingekuwa gumu kwa wao kupeleka watumishi kila mtaa.

Hapa pia ikumbukwe ni vema kuzingatia kuwa watu bado awaelewi umuhimu wa utalii kutokana na hali ngumu ya maisha na kutoa mabiwa faida za utalii katika kujikwa mua hali hiyo ngumu.

Endapo watu watapata nafasi na fursa kupitia viongozi wao wa mitaa na kuelezwa umuhimu wa utalii kasi ya watalii wa ndani itakuwa kwa kasi kubwa sana.

Swala hili linajidhiirisha katika maonyesho ya kimataifa ya kibiashara ya Sabasaba mabapo watu wengi uwa na kiu ya kufahamu aina za wanyama na kuwatazama kama kitu kigeni ndani ya nchi yao .

Lakini hiyo ni kwa wanyama vipi kuhusu utalii ambao auhamishiki kama Olduvai Gorge watu wataelewa nini kuhusu hilo hivyo ni wakatai muafaka wizara kubadilisha mfumo wa utalii wa ndani.

Kama hilo nalo gumu hata hili la kutumia sinema na video kila mtaa kama ilivyokuwa tukionyeshwa sinema za yesu katika viwanja vya wazi hapo zamani? nadahani hii ndio njia pekee ambayo inatakiwa kuafuatwa na badala ya blaa bla za ofisini na miradi ambayo inashindwa kufikia malengo.

Waziri wangu maige lazima uwe macho na watendaji wako sio kila dokezo linafaa katika kufanikisha utalii wa ndani madokezo mengine ni ya kisanii na yanataka kufuja fedha za serikali.

Hivyo basi ni lazima kutumia jicho la tatu katika mpango huu ambao utaongeza pato la taifa letu na kuachana na tabia ya kuomba omba fedha kutoka kwa waisani.

mwishoooooooo

No comments:

Post a Comment