Thursday, July 28, 2011

. Genevieve apaa tena

MWIGIZAJI nyota wa filamu nchini Nigeria  Genevieve Nnaji hivi
karibuni ameteuliwa kuwa Mwanamke anavaa vizuri zaidi ‘Most Elegant
Woman’ baada ya kuwashinda wanawake nyota 30 waliopigiwa kura na
Jarida la mitindo la Encomium Magazine.



Akizungumzia siri ya mafanikio yake hayo, galacha huyo wa filamu
alisema kwamba hata yeye hajui hasa lakini pengine filamu anazoigiza
kwa umakini ndizo zilizompa nafasi hiyo kwani katika filamu hizo
amekuwa akijitahidi za sana kujikita katika mitindo ya uvaaji.

“ Unapokuwa msanii utambue kuwa ni kioo cha jamii, hivyoo unapaswa
kufanya mambo ukijua nyuma yako kuna kundi kubwa linalokutazama,
kukuiga na kujifunza kutioka kwako, kwangu mimi uanamitindo umekuwa
damuni tangu nikiwa mdogo kwa hiyo huwa ninajitahidi kuvaa vizuri
katika filamu zangu,” alisema.

Galacha huyo ambaye  hupendelea kula wali, na kutumia manukato ya Coco
Chanel, alisema kitu anachopenda katika uanamitindo ni ‘ handbag ‘.

Alipoulizwa kuhusu tuzo hiyo ya ‘Most Elegant Woman’ alisema
anajisikia vizuri na kwamba imemchukua muda mrefu kwake kushinda tuzo
kama hiyo. Pia alizungumzia maisha yake ya ndoa na kuweka wazi kwamba
ataolewa atakapopata mwaanamume  anayefaa lakini haina maana kwamba
anatafuta mwanamume.


2. Stella Damasus, Mofe Duncan wavuma tena

WASANII waliovuma katika ‘kashfa’ ya mapenzi Dj Mofe Duncan na Stella
Damasus ambaye ni mwiogizaji wa Nollywood wameibuka  na kuacha maswali
kwa mashabiki hasa wanaopenda kufuatilia mambo ya watu.

Stella Damasus na Mofe Duncan, walijikuta wakianikwa kwenye vyombo vya
habarii kuhusu uhusian wao wa mapenzi baada ya kubambwa wakiwa katika
mazingira ya kutatanisha walikuwa wakisherehekea harusi na mshikaji
wao Dakore-Olumide mwezi januari.

Vyombo vya habari viliandika mara kwa mara kuhusu uhusiano wao wa
mapenzi  ambapo hata hivyo kwa nyakato tofauti, wawili hao walikana na
kusema kwamba uhusiano wao ni wa kibiashara za si zaidi ya hapo na ni
tofauti na watu wanavyowazungumzia.

Hata hivyo Mofe ambaye ni Dj waa Radio  5ive28 Entertainment  pamoja
na Stella wameibuka ten pamoja safari hii wakiwa wameigiza pamoja
katika filamu inayoongozwa na Kampuni ya  SDA Production,  na wote
wanafanya programu itakayorushwa kwenye televisheni muda sio mrefu.


3.Omotola bado aandamwa


MWIGIZAJI galacha wa kike Nigeria Omotola Jalade bado anaandwamwa na
shutuma za kuvaa nusu uchi pamoja na kuwakilisha Afrika kati tuzo za
heshima za filamu duniani zinazojulikana kama Grammy Awards.

Hata hivyo kuna mgawanyiko wa mashabiki na wananchi wengine
wakijiuliza kama kweli msanii huyo anastahili kupewa lawama hizo hata
baada ya kuiletea sifa nchini yake Nigeria na Afrika nzima heshima
kubwa ya kukanyaga zulia jekundu.

“Mimi sidhani kama anastahili lawama zote hizo, inatupasa kuangalia
ushiriki wake katika tuzo hizoo ambao ndio kitu kikubwa zaidi, Tuzo za
Grammy ni kubwa na zenye hadhi, lakini pia hata mavazi aliyovaa yapo
katika mitindo si kwamba alivaa uchi, alisema mmoja wa mashabikki.

"Kama lilikuwa ni suala la kumwekea mikono mwanamume si jambo la
ajabu, na wla haimaanishi kwamba ni mpenzi wake,” alisema shabiki
mwingine.

Omolata alifanikiwa kukanya Zulia Jekundu  ‘Grammy Award 2011 Red
Carpet’ jambo ambalo limepokewa kwa hisia kwa wadau wote wa filamu
nchini humo lakini pia kuiletea heshima kubwa nchi yake.

Galacha huyo aliongozana na meneja wake katika kampuni anayofanyia
kazi ya Bishop Entertainment and Bungalo/Universal Records na ameeleza
kuwa hiyo imempa changamoto kubwa ya kufanya vizuri zaidi katika
tasnia ya uigizaji nchini humo na kimataifa.



1.
Elton John kumsaka baba wa mwanaye

LONDON, Uingereza

MWIMBAJI Elton John amesema yupo mbioni kumsaka mwanamume ambaye ni baba wa kibiolojia wa mtoto wake wa kiume.

Elton mwimbaji wa kibao cha 'Rocket Man' na mumewe David Furnish wamekuwa wazazi wa mtoto mwenye umri wa miezi minne Zachary Jackson kupitia kwa mama wa kuajiliwa (Surrogate mother) siku ya Christmas Day na kwa mara ya kwanza walisisitiza wasingependa kufahamu nani miongoni mwao ni baba wa ukweli.

Ingawa mwanamuziki huyo (64) sasa ameamua kupitia vipimo vya DNA kama Zachary hahitaji kufahamu nani ni damu ya karibu kwa sababu za kitaalamu.

Elton aliliambia gazeti la Daily Mirror: "Zac atatakiwa kufahamika kwa jitihada kubwa za kutafuta vipimo kama hivi. kama atakuwa ni wa David nitafurahi sana. Lakini kwangu sitajali na kinyume chake."

Lakini pia alithibitisha kuwa amemtumia zawadi familia ya mwanamke asiyejulikana aliyesimamia malezi ya mtoto wake.

Mapema baada ya Zachary kuzaliwa, rafiki wa David alisema wachuma hao hawakuwa na sababu ya kumsaka baba wa kibaolojia wa mtoto huyo ambaye angekuwa na kuwafahamu wazazi wake aliofanana naye.


                             
2
Cheryl Cole kuwa jaji shindano la X Factor

LONDON, Uingereza

MWANAMUZIKI Cheryl Cole amethibitishwa kuwa jaji katika shindano maarufu la muziki nchini Marekani la 'The X Factor'.

Simon Cowell amemthibitisha mwimbaji huyo wa kibao cha 'Promise This' kuwa ataungana naye kusimamia shindano hilo pamoja na jaji wa zamani wa shindano la 'American Idol' Paula Abdul katika mpango huo.

Simon alisema: "Pamoja na Cheryl, niliposikia ningekutana naye faragha mara moja na kumpa kazi katika 'The X Factor'. Niliona yeye ni makini, mbunifu na anafahamu anachokizungumza."

"Unaweza kukutana na mtu maalumu mara moja katika maisha, Cheryl ni mtu maalumu, ana uwezo mkubwa katika mawasiliano, ni jaji mwenye uwezo na anajipenda.Nadhani atafanya kitu kizuri Amerika."

"Nilimwonesha tepu yenye mwongozo ambao ungerekodiwa kuhusu Cheryl Uingereza kwa Darnell alisema , 'Ningependa kumsiki pia katika shindano la 'American Idol'.' Kiukweli wana mapenzi makubwa naye."

Dernell (51) alisisitiza mrembo huyo mwenye miaka 27 kuanza kutumiwa katika televisheni kama jaji mapema bila kujali uwepo wa Jennifer Lopez, Cee Lo Green na Mariah Carey ambao wanaaminika kutajwa kuwemo katika mpango huo.




1.
Elton John kumsaka baba wa mwanaye

LONDON, Uingereza

MWIMBAJI Elton John amesema yupo mbioni kumsaka mwanamume ambaye ni baba wa kibiolojia wa mtoto wake wa kiume.

Elton mwimbaji wa kibao cha 'Rocket Man' na mumewe David Furnish wamekuwa wazazi wa mtoto mwenye umri wa miezi minne Zachary Jackson kupitia kwa mama wa kuajiliwa (Surrogate mother) siku ya Christmas Day na kwa mara ya kwanza walisisitiza wasingependa kufahamu nani miongoni mwao ni baba wa ukweli.

Ingawa mwanamuziki huyo (64) sasa ameamua kupitia vipimo vya DNA kama Zachary hahitaji kufahamu nani ni damu ya karibu kwa sababu za kitaalamu.

Elton aliliambia gazeti la Daily Mirror: "Zac atatakiwa kufahamika kwa jitihada kubwa za kutafuta vipimo kama hivi. kama atakuwa ni wa David nitafurahi sana. Lakini kwangu sitajali na kinyume chake."

Lakini pia alithibitisha kuwa amemtumia zawadi familia ya mwanamke asiyejulikana aliyesimamia malezi ya mtoto wake.

Mapema baada ya Zachary kuzaliwa, rafiki wa David alisema wachuma hao hawakuwa na sababu ya kumsaka baba wa kibaolojia wa mtoto huyo ambaye angekuwa na kuwafahamu wazazi wake aliofanana naye.


                             
2
Cheryl Cole kuwa jaji shindano la X Factor

LONDON, Uingereza

MWANAMUZIKI Cheryl Cole amethibitishwa kuwa jaji katika shindano maarufu la muziki nchini Marekani la 'The X Factor'.

Simon Cowell amemthibitisha mwimbaji huyo wa kibao cha 'Promise This' kuwa ataungana naye kusimamia shindano hilo pamoja na jaji wa zamani wa shindano la 'American Idol' Paula Abdul katika mpango huo.

Simon alisema: "Pamoja na Cheryl, niliposikia ningekutana naye faragha mara moja na kumpa kazi katika 'The X Factor'. Niliona yeye ni makini, mbunifu na anafahamu anachokizungumza."

"Unaweza kukutana na mtu maalumu mara moja katika maisha, Cheryl ni mtu maalumu, ana uwezo mkubwa katika mawasiliano, ni jaji mwenye uwezo na anajipenda.Nadhani atafanya kitu kizuri Amerika."

"Nilimwonesha tepu yenye mwongozo ambao ungerekodiwa kuhusu Cheryl Uingereza kwa Darnell alisema , 'Ningependa kumsiki pia katika shindano la 'American Idol'.' Kiukweli wana mapenzi makubwa naye."

Dernell (51) alisisitiza mrembo huyo mwenye miaka 27 kuanza kutumiwa katika televisheni kama jaji mapema bila kujali uwepo wa Jennifer Lopez, Cee Lo Green na Mariah Carey ambao wanaaminika kutajwa kuwemo katika mpango huo.


                      
3
Binti wa Smith amfurahisha Rais Obama

NEWYORK, Marekani

RAIS  Barack Obama amempigia kinanda mwimbaji chipukizi wa Pop nchini humo Willow Smith ambaye alig'ara vilivyo katika onesho maalumu lililofanyika Ikulu ya White House.


Willom mwenye umri wa miaka (10) alifanya onesho hilo katika Ikulu ya White House katika sikukuu ya Pasaka ambako mwimbaji huyo wa 'Whip My Hair' ameripotiwa kumfurahisha vilivyo binti wa Obama, Sasha.



Willow aliimba kibao chake kipya cha 'Rockstar' na kingine cha  '21st Century Girl' na mwengine uliomg'arisha uitwao 'Whip My Hair'.


Mwimbaji huyo pia alimwimbia Obama kibao cha 'Only Girl (In the World)', ulioimbwa na wanamuziki Rihanna na Lady Gaga 'Just Dance'.


Mtoto wa Obama mwenye umri wa miaka 9 alionekana mwenye zaidi ya furaha pale wazazi wake walipomsomea Willow kitabu cha Chicka Chicka Boom Boom katika tukio hilo lililoanza saa moja asubuhi kwa siku nzima.


Mama wa Willow Jada Pinkett Smith na mke wa Obama, Michelle Obama kwa pamoja walifurahia kwa kugonganisha glasi mbele ya umati mkubwa wa watu kabla ya kumaliza sherehe kwa kula keki maalumu iliyotengenezwa mfano wa yai.


                            
4
Russell Brand kuwalea wanaye Uingereza


NEW YORK, Marekani

MWIGIZAJI Russell Brand amesema hataki watoto wake walelewe kimaadili ya bara la Amerika.

Russel raia wa Uingereza kwa sasa anaishi katika Jiji la Los Angeles pamoja na mke wake nyota wa pop Katy Perry na kuyafurahia maisha lakini anataka kuwalea watoto wake katika maadili ya nchi alikotokea.

Alipoulizwa kama angerudia na kuishi kwa Uingereza alisema: "Kwa siri nataka kufanya jambo hili.Nina wasi wasi kuwasiki watoto wangu wakinijibu wakizungumza kimaadili ya Amerika."

Hata hivyo nyota huto amesema anahitaji kufanya kazi kwa bidii ili kuuza mawazo yake katika Jiji la  California ambako Katy ana soko kubwa.

Aliliambia jarida la Seven: "Nina uhakika naweza kumfanya auze nakala ndogo tukiwa Uingereza. Watu wanataka kuwa juu siku zote, si ndio?.," alihoji Russell.

Russell na Katy walifunga pingu za maisha Oktoba mwakajana baada ya miaka mingio ya uchumba wao kupita lakini nyota huyo amesema ataendelea kumfanyia mambo asiyoyatarajia mkewe hata kama ataonyesha kubadilika ingawa akili yake ni kuona uhusiano wa uhakika



5
'Wasanii jifunzeni Kiingereza'
Na Shaban Mbegu

BAADA ya kushiriki katika filamu ya 'Devils Kingdom' msanii kutoka nchini Nigeria, Ramsey Noah amewataka wasanii nchini kuhakikisha wanajifunza na kujua kuzungumza lugha ya kiingereza kwa ufasaha.

Akizungumza na Maisha jijini Dar es Salaam Noah alisema  wasanii nchini wawezekufikia katika hadhi ya kimataifa ni lazima wajifunze lugha hiyo ambayo ndio inatumika kwa asilimia kubwa katika utengenezaji wa filamu.

Alisema katika medani hiyo ya filamu kila kitu huwa kinaelekezwa na kuzungumzwa kwa lugha hiyo,na ndio inayotambulika kimataifa zaidi.

"Japokuwa kila nchi ni lazima inakuwa na lugha yake, lakini kama msanii una malengo ya kuwa wa kimataifa ni lazima ujue kuzungumza na kuandika kiingereza kwa ufasaha kwa kuwa ndio lugha inayotumika zaidi katika filamu duniani", alisema.

Akizungumzia filamu hiyo alisema pamoja na kukumbana na changamoto ya kutofautiana lugha na washiriki wenzake, ametumia usanii wake kuhakikisha anatimiza wajibu wake kama mhusika mkuu katika filamu hiyo inayohusu mambo ya kishirikina.

Mbali na wasanii hao, ndani ya filamu hiyo pia kutakuwa na wasanii wengine akiwemo Patchou Mwamba, Kajala Masanja, Kimlola Kimlola, Stanley Msungu, Bakari Makuka na wengine



6
Sabrina kuja na 'Justis'
Na Laurent Samatta

NYOTA wa filamu nchini Sabrina Omari Kameya 'Salome', amesema anatarajia kutoa kazi yake mpya inayoitwa  'Justis', filamu ambayo itakuwa ya maajabu ya kila aina lakini haina mazingira ya uchawi.

Akizungumza na Maisha hivi karibuni nyota huyo alisema filamu haina mapenzi lakini kikubwa kinachoelezewa humo ni hukumu ambayo itakuwa inatolewa na muhusika mkuu ambaye atakuwa anauwezo wa kujibadilisha jinsia.


Alisema yeye ni mwanamke lakini atakuwa anacheza kama mwanaume wakati mwingine atabadilika na kuwa babu au bibi, kutokana na hukumu itakayokuwa inatolewa kwa watu waovu.

'Watanzania wamezoea kila msanii anataka na filamu ya mapenzi lakini kwa upande wangu nataka kuleta changamoto na ndiyo maana kazi hiyo itakuwa na maajabu lakini siyo ya kutisha au uchawi," alisema.



7
Songombingo kutoka June
Na Andrew Ignas.

KUNDI la muziki wa dansi la Talent Bendi imetarajia kuingia kambini Mei 24 mwaka huu kwa ajili ya kurekodi Video yao ya 'SONGO MBINGO'ambayo inatarjia kutoka mwanzoni mwa mwezi June mwaka huu.

Akizungumza na Maisha hivi karibuni Mkurugenzi wa bendi hiyo Husein Jumbe alisema kuwa kundi lake litaingia kambini  Mei maeneo ya Mbagala ili kukamilisha kurekodi Video yao hiyo.

"Lengo letu kwa sasa ni kuhakikisha tunamalizia kurekodi video zetu zote zilizobakia katika albamu hii ya Subiri Kidogo na tunatarajia kuingia kambini ili kutoa video ya 'SONGO MBINGO'"alisema Jumbe.


Alisema kuwa pia baada ya kukamilisha kurekodi video zao ambazo zitakuwa zimebakia katika albamu yao wataanza kuandaa nyimbo mpya ya albamu ya pili katika kundi la Talent bendi.


Hata hivyo Msanii huyo amewataka wasanii wachanga ambao wapo mitaani lakini wenye vipaji vya muziki kujiunga na bendi yake ambayo imeundwa na vipaji vingi vya wasanii wachanga.

8
Kshabab kuja na 'Karazinga'

Na Agnes Mwaijega

MSANII chipukizi wa kizazi kipya nchini aliyetamba na kibao cha komando ,Adam Kigoda 'Kshabab' amesema anatarajia kutoa single mpya pamoja na video yake mwezi huu.


Akizungumza na Maisha alisema wapenzi wa muziki wategemee kuona mabadiliko makubwa katika kazi hiyo aliyoirekodi.


Alisema 'single' hiyo iitwayo 'Karazinga' iko katika mtindo wa zouk,rumba na kiarabu na itamfanya atambulike zaidi kuliko ile ya awali.

"'Single' niliyoirekodi mara ya kwanza haikunitambulisha,nina imani kuwa hii  ya sasa itanitangaza kwa sababu nimeifanya kwa umakini mkubwa," alisema

Alisema amepata prodyuza mpya ambaye pia ni meneja wake anayesimamia kazi zake kwa umakini mkubwa.


9
PASHA kuja na warembo
Na Andrew Ignas.

MWANAMUZIKI wa muziki wa kizazi kipya nchini ambaye alitamba na kibao cha Hidaya Hija Mtepa'PASHA'ameanza maandalizi ya video ya nyimbo yake ya Warembo ambayo inatarajia kutoka mwezi Mei mwaka huu.

Akizungumza na maisha jana muimbaji huyo alisema kuwa kwa sasa yupo mbioni kurekodi video yake mpya ambayo inafanya kupitia Visual Lab.


"Nimeshaanza maandalizi ya Video yangu ya Nyimbo ya Warembo ambayo itakuwepo katika Albamu ya Hidaya ambayo natarajia kuitambulisha hivi karibuni"alisema Pasha..


Alisema kuwa katika albamu yake hiyo ya Hidaya itakuwa na nyimbo 10 na tayari mpka sasa amesharekodi nyimbo chache ambazo ni Hidaya,Warembo,na nyinginnezo.


Hata hivyo muimbaji huyo amewahasa wanamuziki ambao wanatabia za kuiba myimbo au mashairi ya wasanii chipukizi.

10

Daimond mbioni kuachia albamu ya pili

Na Laurent Samatta

MUIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul 'Daimond', baada ya albamu yake ya kwanza kufanya vizuri hivi sasa yupo katika maandalizi ya kutoa albamu ya pili ambayo bado hajaipa jina.

Akizungumza na Maisha jijini Dar es Salaam, nyota huyo wa kibao cha 'Mbagala' alisema albamu hiyo inatarajia kuwa na nyimbo nane ambazo ni Moyo wangu, Mboni zangu, Chanda chema, Lala salama na nyingine.

Alisema albamu hiyo anaamini itafanya vizuri lakini kikubwa alichokipaga kabla hajatuoa albamu hiyo anataka kufanya ziara mikoa yote ya Tanaznia Bara na nje ya nchi kwa lengo ya kuitagaza kupitia buradani atakazokuwa anazitoa ili iweze kuuza vizuri.

"Albamu bado sijaipa jina kwa sababu kila wimbo nilionao ni mzuri hivyo naamini baada ya maandalizi yote kukamilika nitaweza kujua ni upi uweze kubeba albamu yangu," alisema.

Alisema hata hivyo katika suala la kukuza muziki hapa nchini kwa upande mwingine wananchi wanachangia kushusha thamani ya msanii husika kwa sababu hawana tabia ya kununua kanda halisi badala yake wananunua iliyotolewa kopi kitu ambacho hakieleti maandeleo.

No comments:

Post a Comment