Na Humphrey Shao
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es salaam imeahirisha kesi ya ugawaji wa viwanja katika eneo la kinyerezi iliyofunguliwa na wananchi dhidi ya Manispaa ya Ilala hadi Julai 11 mwaka huu.
Ilidaiwa na karani wake Bw. Obed Abdalla kuwa kesi hiyo iliahirishwa jana mahakamni hapo kutokana na jaji anayesikiliza kesi hiyo Agostine Shangwa kupata udhuru.
Kesi hiyo ilifikishwa mahakani hapo June 28 na wananchi wa eneo la kinyerezi wakidai manispaa ya Ilala kuendesha mradi wa kuuza viwanja vyao kinyume na taratibu.
Wananchi hao wanawakilishwa na wakili wa kujitegemea Bw. Mathias Kisegu.
Katika uamuzi wa awali baada ya kusikiliza malalamiko hayo jaji Agustino Shangwa aliagiza manispaa hiyo kusitisha ugawaji wa viwanja hivyo hadi pande zote mbili zitakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
Katika utetezi wa awali Mwenyekiti wa Kamati ya wananchi wa kinyereziDkt Silas Kishaluli alieleza mahakama hiyo kuwa walifikia hatua ya kufungua kesi baada ya mazungumzo na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bw. Gabraeli Fuime kupata muafaka juu ya hilo kushindikana.
Alisema hali hiyo ndiyo iliyowasukuma kufungua kesi ili mahakama itoe tafsiri sahihi ya kisheria kuhusu hatua zinazokusudiwa kuchukuliwa na Manispaa hiyo bila kuzingatia maslahi yao.
Manispaa ya Ilala ilitangaza kupima viwanja katika eneo la kinyerezi kama sehemu ya utekelezaji mradi wa viwanja 20000 vilivyo tangazwa na serikali kwa lengo la kupunguza uhaba wa viwanja vya makazi katika jiji la Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment