Sunday, July 3, 2011

Makala ya mama mipango

Mariamu Ismail"Mama Mipango" Mshairi mwenye kiu ya kupandisha chati ngoma za asili.

Na Humphrey Shao.

Hivi karibuni kulikuwa na Tamasha la mwezi la jukwaa la sanaa ambalo lilifanyika katika ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa(BASATA) na kushirikisha wasanii wa kada mbalimbali ndipo nilipopata nafasi ya kuzungumza na msanii huyu mkongwe anaye fahamika kwa jina la Mama mipango.

Mama mipango anaanza kunieleza hasa nini maana ya ngoma na kusema kuwa Ngoma ni lea ya utaratibu uliowekwa na watumiaji wenyewe .

Ngoma ni uchezaji wa wa viungo vya mwili kwa mnyambuliko na utaratibu maalum kufatia mapigo ya ngoma yenyewe ala kulingana na kabila husika na desturi zake.

Anaeleza kuwa hapo zamani mababu zetu walitumia ngoma kama chombo cha mawasiliano kwa makabila mengine walitumia kwenye sherehe mbalimbali kama chombo kikuu cha kutoa burudani.

Anasema kuwa ngoma zilitumika kwenye jando na unyago hata baada ya kazi kama chombo cha kutolea mafunzo ,maonyo au kuasa jamii ijikosoe kwa njia ya nyimbo zinazo tungwa na waimbaji maharufu .

Anaeleza kuwa nyimbo za ngoma zilitumika kama ishara ya jambo fulani hali iliyopelekea kufikisha taharifa katika vijiji vingi sana hii ni kwa sababau ngoma inasikika sana.

Hivyo basi viongozi wanapaswa kutumia ngoma kama chombo mawasiliano na kutoa ujumbe kwa jamii kwa kuanza kutumia zilizopo nchini na wasanii wa ngoma za asili kama chombo muhimu cha kuwaleta wananchi pamoja.

"Kwa hivyo basi ni tofauti sana kati ya ngoma na sanaa nyingine duniani ngoma inamvuto wa pekee kwa ni chombo ambacho kinachoweza kutumika kutambulisha utaifa wa mtu fulani"anaeleza Mama Mipango.

Hivyo ni muhimu serikali ikatenga fungu kwa ajili ya kuenzi sanaa ya ngoma hapa nchini hili kujenga sura ya utaifa kwa kurthisha kizazi chetu ngoma za asili.

Anaeleza kuwa Sanaa ya ngoma inarithiwa na sanaa hii ni raisi kurithi kuliko sanaa yoyote ile hapa duniani Tanzania ilitumia ngoma katika kudai uhuru na kuwfariji mashujaa mabalimbali walipotoka vitani hivyo basi ni vema utaratibu huu wa kutumia ngoma ukaendelezwa kwa kupitia wasanii wetu wa ngoma za asili.

Ni vema serikali ikavuta kumbukumbu hapo awali kupita radio ya taifa TBC watu waliweza kuwasilisha ngoma za asili kama sehemu ya burudani kwa watanzania na umma mkubwa ukaburudika na kuelimika na ngoma kupita TBC enzi za mzee moris watu walipigiwa ngoma kujua kua kunajambo linataraji kusemwa.

"Ngoma za asili zimetoa mchango mkubwa katika taifa hili ngoma imechochea kudumisha amani Tanzania bara na visiwani zimefanikiwa kuleta maendeleo makubwa sana hapa nchini na kujenga dhana nzima ya uzalendo "Anaeleza Mama Mipango.

Hivyo basi ni vema ngoma zikaanza kutumika katika kampeni ya kilimo kwanza kama sehemu ya kuleta maendeleo hapa nchini ikiwa na lengo la kuongeza tija na hamasa katika kampeni hii ya kilimo katika sehemu husika kutumia ngoma za asili katika makabila yetu.

Ngoma za asili za makabila miamoja na ishirini zimechezwa hapa nchini hivyo basi kama zitatumika kama zilivyotumika hapa nchini wasanii na vijana wetu wataweza kujiajiri kwa kutumia ngoma za asili.

Anaeleza kuwa kuna ngoma za ndani ambazo zilitumika kwa ajili ya kuwafunda Vijana hili waelewe maadili mema hivyo basi ni vema wataalamu wa ngoma hizi wakapatiwa eleimu ya kisasa zaidi hili waweze kutoa na elimu ya maisha kulingana na hali halisi ya kisasa.

Anaeleza kuwa ngoma hizi ni darasa tosha ambalo linaweza kutumika kuikwamua jamii yetu katika majanga mabalimbali hili kuokoa uchumi wa taifa hili.

Ngoma za unyago zinataumika kukataza mabaya yote na matendo machafu na mambo mengine ambayo hayakubaliki hivyo basi ngoma hizi zikitumika vizuri itasidia hata kupunguza migomo ya wanafunzi katika shule zetu.

Anaeleza kuwa ngoma za asili zinanafasi kubwa kurekebisha mambo maovu ambayo ni kero katika jamii inayotuzunguka.

Mwisho ninapenda kuwaasa wasanii wenzangu ili tufanye kazi zetu ipasavyo ni lazima tujitambue ni nani katika jamii inayotuzunguka hivyo ni vema tuanze kutoa elimu ya ngoma za asili na tusiwe tegemezi.

mwishoooooooo

No comments:

Post a Comment