DADA wa gwiji wa muziki ya miondo ya zouk nchini ambaye ni mkurugezni wa bendi ya B -Band Banana Zoro 'Maunda Zoro' amewataka wasanii wachanga kuhakikisha wanaweka mazoea ya kujifunza muziki wa kisasa ambao ni wa live Band badala ya kubweteka na wa studioni tu.
Akizungumza na Maisha Mwanamuziki huyo amesema wasanii wachanga wanatakiwa kujifunza aina ya muziki wa kutumia vyombo badala ya ule waliokuwa wamezoea ambao ni wa kurekodi studioni.
"Siwakatazi kurekodi studioni ila ni vema pia kujifunza kuimba kwa mtindo huu wa kisasa ambao ni wakuimba kwa Band kwakuwa unawakuza na kuwafanya kufahamika zaidi "alisema Maunda.
Hata hivyo amewasifu wasanii wanaotokea'cakatika jumba la kukuza vipaji vya muziki nchini maarufu kama 'THT kutokana na ubora wa kazi zao wanazifanayanya.
Aidha kwa upande mwingine amevitaka vyomba vya habari ambavyo vinachochea kupungua kwa maadli ya jamii kuachana na tabdia hizo na badala yake wapiganie mambo yatakayo saidia maendeleo.
mwisho.
No comments:
Post a Comment