Saturday, January 25, 2014

MCEZAJI BORA WA TENISI ALIYENIVUTIA KATIKA MASHINDANOYA WATOTO


Dk. Ali Shein kumnadi mgombea Kiembesamaki

Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki-Januari 26.
Dk. Ali Mohamed Shein, atakuwa mgeni rasmi na kumandi Mahomoud Thabit Kombo


Dk. Ali Shein kumnadi mgombea Kiembesamaki
Na Andrew Chale, Zanzibar
MAKAMO Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi,  Dk. Ali Mohammed Shein  kesho Januari 26, anatrajiwa kumnadi mgombea wa Uwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki, Mahmoud Thabit Kombo, katika uchaguzi mdogo unaoendelea kwenye jimbo hilo.
Katika tarifa yake, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema kuwa, Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,  Dk Shein atakuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo wa nne wa hadhara kwenye kampeni hizo zinazoendelea.
Na kuongeza kuwa, Dk. Shein atawahutubia wananchi sambamba na kumnadi, Mgombea huyo wa nafasi ya uwakilishi, Mahmoud Thabit Kombo, anayewania nafasi hiyo kwenye jimbo hilo la Kiembesamaki.
Vuai aliwataka wananchi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi ilikusikiliza sera na ilani za chama hicho katika utekelezaji wake iliwakichague chama cha Mapinduzi kwa misingi imara ya kuwaletea maendeleo.
Aidha, kwa upande wake,  Mahmoud Thabit Kombo aliwaomba wananchi wa jimbo hilo, kumpigia kura hiyo Februari mbili, ili akawawakilishe kwenye Baraza la Wawakilishi.
“Nawaomba Wanakiembesamaki, kutumia fursa ya kipekee ya kunichagua ilikuweza kuwawakilisha kwenye BAraza, hakika  chama chetu ni sikivu na daima kipo na wananchi katika kuwatetea na kuwaletea maendeleo” alisema, Mahmoud.
Kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Kiembesamaki, zilianza Januari 21, ambapo zinatarajia kumalizika Februari Mosi, mwaka huu huku wananchi wakitarajia kupiga kura ya chaguzi huo, Februari mbili.
Mwisho



YANGA YAISULUBU ASHANTI BAO 2-1







Thursday, January 23, 2014

EU YAPIGA JEKI WATOTO TANZANIA

 EU1: Mkuu wa Ushirikiano kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya Tanzania Eric Beaume (kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano ya Mradi wa Kupambana na Ukatili kwa Watoto  na Mwakilishi wa UNICEF hapa nchini Jama Gulaid, kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Plan International Tanzania Jorgen Haldorsen, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid na Mkurugenzi Mkazi wa Save the Children International Tanzania Steve Thome wakishuhudia makabidhiano ya hati hiyo jana jijini Dar es Salaam
U4: Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Seif Rashid (aliyeko mstari wa mbele katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa Mradi wa kutokomeza Ukatili kwa Watoto mara baada ya kutia saini msaada kutoka Umoja wa nchi za Ulaya jana jijini Dar es Salaam.

MKUTANO MKUU WA NGUMI ZA KULIPWA

MKUTANO   MKUU  WA  NGUMI   ZA  KULIPWA

Siku ya terehe 1 ya mwezi wa pili katika ukumbi wa vijana hall kinondoni KUANZIA SAA TATU NA NUSU ,kutakuwepo na mkutano mkubwa wa wanamasumbwi wote ulioitishwa na orgnaizesheni ya ngumiza kulipwa Tanzania (TPBO) kwa lengo la kuwakutanisha mapromota wote,mabondia na makocha  wa ngumi wote kwa lengo la kujadili ngumi za kulipwa zinapoelekewa,kujuana na kuelimishana sheria za ngumi za kulipwa  zinavyotumika kinyume na sasa ,sheria nyingi zinafungiwa macho na kutumia uzoefu zaidi kuendesha mgumi nchini.  Mkutano huo ulioitishwa na Rais wa TPBO bw  Yasin Abdallah akishirikiana  na Ibrahim kamwe na Mapromota wa ngumi chini ya ufadhili wa kitwe Traders unatarajiwa  kuwa mkutano wa kwanza  kuwakutanisha mapromota wote pamoja na  mabondia wa ngumi  za kulipwa wa hapa nchini ili kuboresha ngumi na kuhamasisha wadhamini na makampuni wajitokeze kuudhamini mchezo huo ,ambao ndio mchezo unaoliletea mataji na  sifa Tanzania katika medani za kimataifa lakini hauna udhamini  wowote ,mpaka sasa ni mchezo  ambao unaojiendesha wenyewe kwa nguvu za  wadau wachache wachovu  na mabondia wenyewe ambao uwezo wao ni mdogo sana kukikidhi matakwa kamili ya mchezo wenyewekam ilivyo kwa wenzetu,ni mchezo  ambao una huduma nyingi zinazohitaji nguvu ya wadhamini ili  uendelee kuboreka zaidi.
Akizungumza na vyombo vya habari katibu wa ngumi za kulipwa nchini bw Ibrahim kamwe , amesema imewaalika viongozi wa baraza la michezo (BMT), na viongozi wengine wote wa ngumi za kulipwa watakuwepo kama vile Emmanuel mlundwa,names kavishe,  makaranga,Onesmo ngowi,kinyogoli,  matumla, Zuwena kibena(mama zugo) na viongozi wadau wa karibu na ngumi wamealikwa kuhudhulia mkutano huo ambao utafanyika Siku ya terehe moja ya mwezi wa pili katika ukumbi wa vijana hall kinondoni. hivyo kamwe alimaliza kwa kuwaomba kila anaejijua kuwa yeye ni bondia wa ngumi za kulipwa na promota wangumi  ahudhurie bila kukosa mkutano huu muhimu sana kwa wamasumbwi ya nchi  yetu.

mapambano ya ngumi mbagal azak hem


Bondia Abuu Abas kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Abdul Zugo wakati wa uhamasishaji wa tuzo za PSPF Boxing Award zilizofanyika katika viwanja vya Zakhem Mbagala Dar es salaam tuzo hizo zinafika tamati january 25 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Zugo alishinda kwa K,o ya raundi ya pili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Wednesday, January 22, 2014

ASUTWA USIKU KUCHWA KWA KUMNYANYASA MDOGO WAKE WA MIAKA SABA

 MDADA ANAYEDAIWA KUMTESA MDOGO WAKE NDO HUYO
 WATU WAKIWA WAMEJAZANA NJE YA NYUMBA ALIYOPANGA


 MJUMBE AKITAKA AMTOE NDANI
 MTO AKIWA AMESHIKWA NA WAKAZI WA ENEO HILO KEKO