Sunday, October 30, 2011

MIYEYUSHO AMCHAKAZA MATUMLA KWA POINT

 


 Bingwa Mpya wa UBO katika uzito wa Bantum,Francis Miyeyusho akifurahia ubingwa wake huo wakati akivishwa mkanda wake na Mlezi wa Mchezo wa Ngumi hapa nchini,Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Afande Suleiman Kova huku Diwani wa Kinondoni,Mh. Abbas Tarimba akiangalia.Francis Miyeyusho kanyakuwa ubingwa huo baada ya kumchakaza vibaya Bingwa wa Zamani UBO,Mbwana Matumla katika mchezo uliomalizika usiku huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee hall.
 Bondia Francis Miyeyusho ampatia konde kali sana mpinzani wake,Mbwana Matumla wakati wa mchezo wao uliomalizika usiku huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee hall.Francis Miyeyusho kanyakua ubingwa katika mchezo huo kwa kushinda Mbwana Matumla kwa point.