Monday, December 16, 2013

.YANGA IMETIMIA


Mchezaji mpya wa Yanga Hassan Dilunga Kushoto akijaribu kuchukua mpira wa kutoka kwa kiungo wa Timu hiyo Athuman Iddi(Chuji) Wakati wa mazoezi ya timu hiyo, wachezaji hao ambao wamejiunga na kikosi hich jana mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya Chalenji. Picha na Humphrey Shao.




Na Humphrey Shao, Dar es Salaam

KOCHA wa klabu ya Yanga Ernie Brandts amesema ameridhishwa na kiwango kilichionyeshwa na mchezaji wa timu hiyo wakati wa mazoezi na kumtaja ni mmoja kati ya wachezaji wenye uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza.
Brandts alisema hayo alipiokuwa akizungumza na Rai mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu hiyo katika viwanja vya bora kijitonyama.

“Kila mchezaji ananafasi ya kucheza kikosi cha kwanza lakini Yule anayeonyesha uwezo na juhudi mara zote ndio ushikilia hiyo namba, hivyo kwa dilunga kwake ni mwanzo mzuri kama nilivyomuaona tangu awali naamini ataleta mabadiliko makubwa” alisema Brandts.

Alisema kuwa kwa sasa timu yake iko vizuri na inajiandaa na mchezo wake wa kirafiki dhidi ya timu ya Simba unaotambulika kw ajina la nani mtani jembe.

Aliongeza kuwa kwa sasa ni mapema sana kuzungumzia mchezo huo kwani nasubiri wachezaji wangu wote watimie ndio nitakuw ana kauli kwa ajili ya mchezo huo.
Mwisho

Na Humphrey Shao, Dar es Salaam
Beki wa kulia wa klabu ya Yanga Rajabu Zahir ameumia goti la kushoto wakati akiwa mazoezini na timu hiyo nakupelekea kutolewa nje.
Kwa mujibu wa taharifa ya daktari wa timu hiyo Nassoro Matyuza alisema kuwa maumivu hayo sio makubwa sana hivyo anahitaji mapumziko ya siku moja kwa ajili ya kujiweka sawa.

“Maimivu yake sio makubwa hivyo nawatoa hofu wapenzi wa yanga kuwa muda mfupi tu atakuw afiti hivyo tgemeeni kumona katika michezo inayokuja “ alisema matuzya .

Mbali na huyo wachezaji wengine ambao walikaa nje kwa ajili ya mejeruhi ni Salum Telela na Nadir Haroub ‘Canavaro’ ambao wao walikuwa nje ya uwanja.

Wachezaji Kelvin Yondani,Emmanuel Okwi pamoja na Amisi Kiiza ambao bado awajaripoti kikosini mpaka sasa.




Mshambuliaji wa klabu ya Yanga Said Bahanuzi akimpa mwili kiungo wa timu hiyo Haruna Niyonzima wakati wa Mazoezi ya timu hiyo katika viwanja vya bora kijitonyama. Picha Na Humphrey Shao.

Saturday, December 14, 2013

Thursday, November 14, 2013

Mlinzi wa kagame mbaroni



Mlinzi wa kagame mbaroni

ALIYEKUWA mlinzi mkuu (bodyguard) wa Raisi wa Rwanda, Paul Kagame, Luteni Joel Mutabazi, ametekwa na kikosi cha jeshi la Uganda na kukabidhiwa kwa Serikali ya Rwanda.

Taarifa za Kiitelejensia zinasema kuwa Luteni Mutabazi ambaye alikuwa akiishi nchini Uganda kwa hati maalumu ya ukimbizi ya Umoja wa Mataifa baada ya kutoroka nchini Rwanda pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya nchi hiyo, Faustin Kayumba Nyamwasa.

Luteni Mutabazi alitorokea nchini Uganda Oktoba 2011, baada ya kutoroka jela yenye ulinzi mkali ya kijeshi ya Kami nje ya Mji wa Kigali akishutumiwa akihusishwa na kutoroka kwa mkuu huyo wa majeshi na kukimbilia Afrika Kusini. Alikuwa mlinzi mkuu wa Rais Kagame mpaka mwaka 2010 alipotoroka na kukimbilia Uganda.
Mlinzi huyo pia anashutumiwa na Serikali ya Rwanda kwa kutoa siri kwa Kikosi Maalumu cha Umoja wa Mataifa chini ya Majeshi ya Umoja ya Kulinda Amani Kongo, (MONUSCO) na kuwezesha kuchakazwa na kushindwa kwa kikosi cha M23.

Tayari Serikali ya Uganda imemsimamisha kazi Mkuu wa Intelejensia katika jeshi la Polisi, Joel Aguma, ambaye alihusika ka kumteka na kumkabidhi Luteni Mutabazi kwa Serikali ya Rwanda kwa kutii amri ya Rwanda kwa kukubali hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa mlinzi huyo.

Tayari Serikali ya Rwanda imekiri kumkamata Luteni Mutabazi na kuzuiliwa katika jela maalumu ya kijeshi ya nchi hiyo mjini Kigali.

Msemaji wa Polisi wa Rwanda, Damas Gatare amesema kuwa huu ni mpango endelevu wa Rwanda na Uganda wa kukabiliana na maasi na majasusi kutoka sehemu mbali mbali duniani na kuwa sheria itachukua mkondo wake.

Serikali ya Rwanda imesema kuwa Luteni Mutabazi atashitakiwa kwa kosa la ujasusi na uhaini na kuwa hakuna mtu yoyote nchini humo ambaye atafanikiwa kutoroka mkono wa sheria na kuwa itaendelea kuwasaka na kuwarejesha nchini wahalifu wote kutoka nchin hiyo.

Mkuu wa Polisi wa Uganda aliyesimamishwa kazi na ambaye amehusika katika utekaji na kumrudisha Rwanda, Luteni Mutabazi alirudi Uganda Oktoba mwaka huu, baada ya kuhudhuria kozi ya mwaka mmoja ya makamanda katika chuo cha Polisi cha Rwanda na kuibuka kuwa mwanafunzi bora katika kozi hiyo.

Mlinzi huyo alitekwa Agosti 20, mwaka huu, saa 11 jioni kutoka hotelini kwake ambapo alikuwa anataka Skype  na kumfanya atoke chumbani kwake na kwenda sebuleni ili aweze kupata wireless internet.

Ghafla makomando watano wa jeshi la Rwanda wakiwa na bunduki za AK47 walimvamia na aliweza kupigana nao kwa muda mrefu na kuwafanya makomando hao kushindwa kumkamata kutokana na uzoefu wake wa kikomandoo.
Baada ya makomando hao wa Rwanda kupata kipigo walitoa ishara kwa wenzao ambao walikuwa katika gari lililopaki chini na kuja kuwasaidia na kuwafanya makomando wenye nguvu zaidi watatu zaidi kwenda kuwasaidia wenzao na kumuwekea kitambaa chenye dawa na kumbeba na kumuingiza kwenye gari.

Habari za Kiitelejensia zinasema kuwa Mutabazi alichukuliwa na gari lenye nambari UAK 551B na kukimbizwa hadi mpakani na kukabidhiwa kwa serikali ya Rwanda.

MWISHO