Mlinzi wa kagame mbaroni
ALIYEKUWA mlinzi mkuu
(bodyguard) wa Raisi wa Rwanda, Paul Kagame, Luteni Joel Mutabazi, ametekwa na
kikosi cha jeshi la Uganda na kukabidhiwa kwa Serikali ya Rwanda.
Taarifa za Kiitelejensia zinasema kuwa Luteni Mutabazi ambaye alikuwa akiishi nchini Uganda kwa hati maalumu ya ukimbizi ya Umoja wa Mataifa baada ya kutoroka nchini Rwanda pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya nchi hiyo, Faustin Kayumba Nyamwasa.
Luteni Mutabazi alitorokea nchini Uganda Oktoba 2011, baada ya kutoroka jela yenye ulinzi mkali ya kijeshi ya Kami nje ya Mji wa Kigali akishutumiwa akihusishwa na kutoroka kwa mkuu huyo wa majeshi na kukimbilia Afrika Kusini. Alikuwa mlinzi mkuu wa Rais Kagame mpaka mwaka 2010 alipotoroka na kukimbilia Uganda.
Mlinzi huyo pia
anashutumiwa na Serikali ya Rwanda kwa kutoa siri kwa Kikosi Maalumu cha Umoja
wa Mataifa chini ya Majeshi ya Umoja ya Kulinda Amani Kongo, (MONUSCO) na
kuwezesha kuchakazwa na kushindwa kwa kikosi cha M23.
Tayari Serikali ya Uganda
imemsimamisha kazi Mkuu wa Intelejensia katika jeshi la Polisi, Joel Aguma,
ambaye alihusika ka kumteka na kumkabidhi Luteni Mutabazi kwa Serikali ya
Rwanda kwa kutii amri ya Rwanda kwa kukubali hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa
mlinzi huyo.
Tayari Serikali ya Rwanda imekiri
kumkamata Luteni Mutabazi na kuzuiliwa katika jela maalumu ya kijeshi ya nchi
hiyo mjini Kigali.
Msemaji wa Polisi wa
Rwanda, Damas Gatare amesema kuwa huu ni mpango endelevu wa Rwanda na Uganda wa
kukabiliana na maasi na majasusi kutoka sehemu mbali mbali duniani na kuwa
sheria itachukua mkondo wake.
Serikali ya Rwanda imesema
kuwa Luteni Mutabazi atashitakiwa kwa kosa la ujasusi na uhaini na kuwa hakuna
mtu yoyote nchini humo ambaye atafanikiwa kutoroka mkono wa sheria na kuwa
itaendelea kuwasaka na kuwarejesha nchini wahalifu wote kutoka nchin hiyo.
Mkuu wa Polisi wa Uganda
aliyesimamishwa kazi na ambaye amehusika katika utekaji na kumrudisha Rwanda,
Luteni Mutabazi alirudi Uganda Oktoba mwaka huu, baada ya kuhudhuria kozi ya
mwaka mmoja ya makamanda katika chuo cha Polisi cha Rwanda na kuibuka kuwa
mwanafunzi bora katika kozi hiyo.
Mlinzi huyo alitekwa Agosti
20, mwaka huu, saa 11 jioni kutoka hotelini kwake ambapo alikuwa anataka Skype na kumfanya atoke chumbani kwake na kwenda
sebuleni ili aweze kupata wireless internet.
Ghafla makomando watano wa
jeshi la Rwanda wakiwa na bunduki za AK47 walimvamia na aliweza kupigana nao
kwa muda mrefu na kuwafanya makomando hao kushindwa kumkamata kutokana na
uzoefu wake wa kikomandoo.
Baada ya makomando hao wa
Rwanda kupata kipigo walitoa ishara kwa wenzao ambao walikuwa katika gari
lililopaki chini na kuja kuwasaidia na kuwafanya makomando wenye nguvu zaidi
watatu zaidi kwenda kuwasaidia wenzao na kumuwekea kitambaa chenye dawa na
kumbeba na kumuingiza kwenye gari.
Habari za Kiitelejensia
zinasema kuwa Mutabazi alichukuliwa na gari lenye nambari UAK 551B na
kukimbizwa hadi mpakani na kukabidhiwa kwa serikali ya Rwanda.
MWISHO
No comments:
Post a Comment