Thursday, November 14, 2013



Na Jennifer Ullembo

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, anatarajia kuachia albamu yake ya kwanza, Januari au Februari mwakani.

Akizungumza na Rai jana, msanii huyo alisema, albamu hiyo ni ya kwanza tangu, alipoanza kujihusisha na masuala ya muziki wa bongo fleva.

Alisema albamu hiyo itakuwa na nyimbo 10, huku nyimbo zake zote zilizoweza kutamba na kumtambulisha zikiwa ndani yake.

“Nilianza na Nainai, hata zile zilizofatia na hizi za sasa hivi, zitakuwemo kwenye albamu yangu hii, mpya mbayo ni mara kwanza kuachia kwa kipindi kirefu,”alisema Ommy Dimpoz.

Msanii huyo alisema, anatarajia kumuachia jukumu la kutafuta jina la albamu, meneja wake Mubenga, ambapo kama albamu hiyo itachelewa haitavuka siku ya Valentine mwakani.


Na Jennifer Ullembo

MSANII wa muziki wa kizazi kipya,  Sunday Mangu ‘Linex’, anatarajia kutambulisha, msanii mpya  ambaye ametokea, kwenye kundi lake la Sauti za Afrika ‘VOA’.

Akizungumza na Rai jana, Linex alisema, msanii huyo atajulikana kama Ssen Lubi na tayari amefanikiwa kufanya wimbo wake, alioupa jina la ‘Kiroho Safi’.

Linex alisema, Lubi ni msanii mpya , ambaye amekuzwa na kupewa mafunzo zaidi, kupitia kundi lao la VOA.

“Msanii huyu ni mpya, najivunia kuvumbua kipaji hichi, anatarajia kuachia wimbo wake mpya wa Kiroho Safi, ambao amemshirikisha Chege Chigunda,”alisema Linex.
  
 Msanii huyo alisema, anaowamba wadau wa muziki kukipokea kipaji kipya, huku akihahidi kuendelea kuibua vipaji vya wasanii wengine wachanga.

Na Jennifer Ullembo
WASANII wa muziki wa kizazi kipya, Chege Chugunda ‘Chege’ na  ‘Temba’, wanatarajia kuachia wimbo wao mpya, uliopewa jina la ‘Kama Kasuku’.

Akizungumza na Rai jana, mmoja wa wasanii hao Chege, alisema kuwa tayari wameingia studio juzi, kuandaa kazi hiyo inayotarajiwa kuachiwa, kabla ya kumalizika kwa mwaka.

Chege alisema, ushirikiano ambao wamekuwa, wakiufanya kwa pamoja na Temba, umeweza kuwaongezea umaarufu zaidi, kwenye kazi zao.

“Tumepanga kumaliza mwaka huu, kwa kuachia wimbo wetu mpya wa Kama Kasuku, mashabiki wajiande kusikia kazi nzuri kutoka kwetu,”alisema Chege.

Msanii huyo aliendelea kusema, mbali na kuachia kazi hiyo ya Kama Kasuku, wanatarajia kufanya shoo mbalimbali za mwisho wa mwaka, ambapo tayari wameanza kupokea  maombi kutoka kwa mashabiki.

No comments:

Post a Comment