Wednesday, July 6, 2011

HABARI ZA SABASABA

EPZA yagundua gari la wagonjwa la kisasa

Na Humphrey Shao
MAMLAKA ya Ukanda maalum wa (EPZA)limezindua gari ndogo la miguu mitatu la kubebea wagonjwa lenye vifaaa mbalimbali vya huduma ya kwanza kabla a mgonjwa kufikishwa hospitali na thamani yake  ni sh milioni 10.

Ugunduzi wa gari hilo lilitokana na kuangalia changamoto katika sekta  ya afya  ambalo linahitaji jina halisi  la kitanzania  kama sehemu ya kuenzi kazi za ndani
Akizunhumza na Tanzania Daima  katika maonyesho ya saba saba Mhandisi Ismail Sadiq alisema kuwa gari hilo lina matairi matatu  ambalo linaweza  kuhimili hata katika maeneo tofauti katika miundombinu.

Sadiq alisema licha ya kuwepo kwa miundimbinu mibovu na kuweza kurahisha  mgonjwa kuwahishwa katika huduma za afya.

Mhandisi  Sadiq alisema kuwa, asilimia kubwa ya malighafi iliyotumika kutengeneza hilo imetoka hapa hapa nchini na kufanyiwa uunganishwaji na watanzania hali ambayo ni kupiga hatua katika tknolojia ya kisasa.

Alisema, lengo ni kurahisisha huduma za matibabu kabla ya mgonjwa kufikishwa hospitalini, jambo ambalo linaweza kupunguza idadi ya vifo ya wagonjwa haoi.
"Tumetengeneza gari hili la wagonjwa kwa kuzingatia miundombinu ya nchi yetu, kwa sababu wagonjwa wengi wanafariki kabla ya kufikishwa hospitalini kutokana na ubovu wa miundombinu pamoja na magari ya wagonjwa katika vituo vya afya na hospitali zetu,"alisema Sadiq.

Aliongeza, gari lina uwezo wa kubeba abiria wanane nyuma na mmoja mbele na kwamba linaweza kutembelea umbali wa kilomita 120 kwa saa katika barabara tofauti,hivyo basi serikalimawadau mbalimbali wanaotoa huduma za afya nchini inapaswa kuwasiliana nao ili waweze kununua na kuzisambaza kwenye hospitali na vituo vya afya.

Alisema,EPZA, wanatarajia kutengeneza aina tofauti za magar kwa ajili ya matumizi tofauti ili wananchi waondokane na uhaba wa usafiri katika maeneo yao, jambo ambalo wanaamini linaweza kupunguza tatizo la usafiri nchini.

Alisema,kutokana na hali hiyo wananchi wanapaswa kutambua kuwa, hapa nchini kuna watalaam mbalimbali ambao wanaweza kufanya kazi tofauti bila ya kutafuta watalaam wa nje, hivyo basi serikali inapaswa kushirikiana nao ili waweze kuongeza ujuzi.

Sadiq alisema ,wananchi wanapaswa kuwa wazalendo kwa kununua bidhaa au mali zinazolishwa na wazalendo wenzao ili waweze kukuza uchumi na kuinua kipato.

mwisho
Makampuni 7 kushindanishwa kujenga daraja la kigamboni -Dk.Dau


SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limesema  kati ya makampuni 16 yaliyojitokeza kwa ajili ya mchakato wa kutafuta mdhabuni wa  ujenzi wa daraja la Kigamboni zote ni za kigeni na hakuna kampuni hata moja ya kitanzania iliyoomba tenda hiyo.


Akizungumza na Waandisi wa habari katika Maonyesho ya 35 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere  Dar es Salaa, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dkt. Ramadhani Dau alisema kuwa kati ya kampuni hizo saba zimeteuliwa kwa ajili ya kushindanishwa.

"Kazi sasa tumeanza kutangaza  tenda kwa  kampuni kwa ajili ya ujenzi wa Kigamboni na  kampuni 16 yamejitokeza  kila mmoja kuomba kazi hiyo ua ujenzi, lakini tumeteua kampuni saba pekee ambazo tunazishindanisha itakayopatikana ndiyo itakayopewa kazi ya ujenzi huo,"alisema.

Alisema kuwa ifikapo Oktoba mwaka huu watakuwa wameshapata maamuzi ya nani atakayejenga na kwamba kabla ya mwisho wa mwaka huu ujenzi huo utakuwa umeanza na utachukua kati miaka miwili au miwili na nusu kukamilika kwake.

Dau alisema kuwa katika mchakato huo wa kutafuta mkandarasi kwa ajili ya ujenzi huo watakuwa makini kuakikisha kwamba yule anayepatikana ni mzoefu na ujenzi wa madaraja na wapi alikwishawai kujenga.

"Tutahakikisha kwamba tunafuatilia madaraja aliyojenga kama yamejengwa na kampuni yake, ni lazima tuwe makini katika uchaguzi kwani mradi huu ni mkubwa na wa kipekee nchini mwetu,"alisema.

Alisema kuwa hao mradi huo, pindi utakapoanza utatoa ajira kwa Watanzania na wale wengi watakaoshiriki katika ujenzi huo watapata uzoefu na kusisitiza kwamba Kampuni za Tanzania hazikujitokeza kuomba tenda hiyo kwa sababu hawana uzoefu na kwamba nchi zilizojitokeza zina uzoefu kwa sababu wana madaraka katika nchi zao.

Dkt. Dau alisema kuwa miaka 50  ya Uhuru, NSSF wamefanya mambo mengi na Kusini mwa Jangwa la Sahara ni Shirika pekee lililofanya hivyo na wanachama sasa wanachukua mafao siku 14 badala ya 30 kama ilivyokuwa nyakati za nyuma.

Alisema kuwa Kauli mbiu ya Maonyesho haya mwaka huu ni sherekea miaka 50 ya uhuru na wanajikita vipi katika kilimo Kwanza , ambapo alisisitiza kwamba NSSF itaendelea kuunga mkono Kilimo Kwanza katika maeneo mbalimbali.

Mwisho
IKIWA imebakia siku moja kumalizika kwa Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara (sabasaba) wananchi wanaotembelea maonyesho hayo waliutaka Uongozi wa Tan Trade kuongeza siku tatu ili waweze kuendelea kujionea bidhaa mablimbali zilipo katika maonyesho.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili wananchi hao waliokutembea maonyesho hayo waliofurika katika banda la Maliasili walisema siku nane azitoshi kwa maonyesho ya sabasaba.
Mkazi wa Ubungo Enock Yusin alisemaMaonyesho ya sabasaba ni makubwa Tan Trda walitakuwa kuyatengea muda wa siku 14 ili kila Mwananchi aweze kuja kujionea .
"Leo ni tarehe sita imebakia siku ya kesho na kesho kutwa kitu ambacho ni wananchi wachache watapata nafasi ya kuja kutembelea moanyesho hayo lakini yangeweza kuongezwa siku yakiwa kama wiki mbili maamini wananchi waliopo mikoani wangeweza kupata nafasi ya kufika na kujionea"alisema Yusini
Yusin alisema kwa maonyesho kama hayo mtu ambae atapata nafasi ya kutembelea ni vigumu sana kufika katika maonyesho hayo na kuweza kutembelea katika mabanda mbalimbali yaliyopo katika maonyesho.
"Uhalisia wa watu waliofika kwa muda huu katika banda la Mali asili naamini atakapo rudi nyumbani atweza kudisikia na kusabisha wengine kuvutiwa kuja kujionea hali kuwa maonyesho yameisha"alisema
Naye Mwananchi aliyetembelea katika maonyesho hayo Elizabeth Swai aliyetembelea maonyesho hayo pamoja na familia yake aliishauri Mamlaka ya Biashara Tanzania (Tan Trade) kutafuta uwezekanao wa Maonyesho hayo kufanyika katika mikoa mingine ya Tanzania tofauti na Dar es Salaam.
Alisema Maonyesho ya sabasaba yanawakutanisha watu wengi ikiwemo wafanyabiashar na wajasiliamali kwa kutumia nafasi hiyo Tan Trde ingechukua majukumu ya Maonyesho hayo kufanyika na mikoa mingine.
"Naamini maonyesho hayo yangeweza kufanyika kama Dodoma,Mbeya Arusha naamini katika kilio cha wananchi wanaotegemea kujiajiri kisingekuwepo"alisema Swai
Maonyesho hayo yaliyohudhuriwa na nchi 17,kampuni 1200,tasisi binafsi 28,tasisi za umma 68 yanatarajia kufikia kilele chake siku ya Ijumumaa amabpo yatafungwa na balozi kutoka katika nchi moja iliyoshiriki maonyesho hayo.
MWISHO
Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), chombo kinachoziunganisha halmashauri zote 133 za  Tanzania bara, jana imetangaza mpango dhabiti ukaosaidia kuzitetea, kuziwakilisha na kuzipa huduma Halmashauri hizo ili ziweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kasi.
Mpango huo kabamba umetangazwa rasmi na Katibu Mkuu wa ALAT, Habraham Shamumoyo katika maonyesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea mjini Dar es Salaam (DITF). ALAT imeungana na waonyeshaji  na watoa huduma mbalimbali katika maonyesho hayo ambayo ufanyika kila mwaka katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.
Akiongea katika maonyesho hayo, Katibu Mkuu wa ALAT alieleza ya kwamba wamejipanga kushiriki kikamilifu katika maonyesho ya kimataifa, kwa sababu ya dhamana kubwa walionayo ALAT na wanachama wake katika kusimamia utelekelezaji wa mipango ya maendeleo ya kitaifa nchin inzima.
“ALAT na halmashauri wanayo kila sababu ya kushiriki ili kuelimisha wananchi, wadau na wafanyabiashara wa ndani na nje juu, majukumu ya Jumuiya na namna inavyofanya kazi,” alisema Shamumoyo.
Aliongeza kwamba mbali hilo, ushiriki wao katika maonyesho utasaidia watu kuelewa mpango dhabiti wa ALAT wenye lengo la kusaidia Halmashauri zote nchini ili ziweze kusimamia na kutelekeleza majukumu yao kwa udhabiti kwa lengo la kuharakisha maendeleo kwa Tanzania, ambao wengi wao wanaichi katika lindi kubwa la umaskini.
Kwa mujibu wa Katibu wa ALAT, ili kuweka ukaribu na wananchi, jumuiya hiyo imewakaribisha baadhi ya wanachama wake katika maonyesho hayo  ili kuweza kuonyesha huduma wanazotoa kwa wananchi na kuweza kupokea malalamiko na ushauri mbalimbali kutoka kwa wananchi.
Hata hivyo, aliongeza, halmashauri zinazoshiriki katika maonyesho haya, zinapata faida nyingi, na kuzitaja baadhi ya faida kama vile kujitangaza na kutangaza fursa zilizopo za uwekezaji ndani na nje ya nchi, kuwasiliana na mashirika mbalimbali yaliyoshiriki kutoka  afrika ya mashariki, kati na kusini na hata duniani kote ili kuweza kupata fursa za kujiendeleza katika nyanja mbalimbali, kuwawezesha wajasiliamali wa Halmashauri kupata fursa ya kuonyesha na kuuza bidhaa zao na kutengeneza mahusiano na wadau mbalimbali na hatimaye  kufanya majadiliano ya kibiashara.
“Faida nyingine kama vile kuiwezesha Halmashauri kupata fursa ya masoko ya nje ya bidhaa zinazozalishwa katika Halmashauri  hasa katika nchi za Afrika Mashariki kati na Kusini, kutoa fursa ya pekee kwa wajasiliamali na wafanyabiashara katika Halmashauri kuweza kukutana na wenzao kutoka kwingineko duniani katika kubadilishana ujuzi na uzoefu wa kibiashara,” alisema katika wa ALAT.
Katika maonyesho haya Halmashauri za Ilala, Temeke, Kibaha mji na Tandahimba zimeshiriki pamoja na wajasiriamali wao, kwa mujibu ya taarifa iliyotolewa na ALAT jana katika maonyesho.
 Mwisho

Tigo waachangia katika sekta ya Elimu
Kampuni ya simu za mkononi, Tigo itafanya kampeni maalum ya kuchangia elimu inayofahamika kama ‘Tigo tuchange’ itakayofanyika Julai 9, 2011 jijini Dar es Salaa.
Akiongea jijini Dar Es Salaam, afisa Uhusiano wa Tigo Jackson Mmbando alisema kwamba kampeni hiyo itahwausisha wateja wote wa Tigo wanaotumia huduma ya Tigo Rusha ambapo watanunua muda wa maongezi kupitia huduma hiyo.
Kampeni kwa muda wa saa moja kuanzia saa tatu  asubuhi mpaka saa nne. “Ukinunua muda wa maongezi kwa kutumia huduma ya Tigo Rusha ambao utazidi kiasi cha shilingi mia tano tayari utakuwa umechangia kusiadia elimu hapa nchini,” alisema Mmbando.
Halikadhalika alisema kuwa ukinunua muda wa maongezi utazawadiwa mara mbili ya muda wa maongezi wa kiasi ualichonunua. Kiasi cha pesa kitakachopatikana kitatumika kununulia vitabu ambavyo vitaenda kusaidia katika shule za msingi hapa nchini.
Alisema kwamba Tigo wameamua kufanya utaratibu huo wa kusaidia sekta ya elimu baada ya kugundua kuwa sekta ya elimu bado kuna huitaji wa vitabu katika baadhi ya shule za msingi hapa nchini.
Baada ya kukusanya pesa Tigo itashirikiana na Taasisi ya Elimu Tanzania ambao ndiyo watatoa orodha ya shule ambazo zinahitaji msaada wa vitabu. “Tumefurahishwa na hili wazo lenu na tunaahidi kuwaunga mkono hadi mwisho na wazo lenu limekuja waka muafaka ambao kweli watoto wetu wanahitaji vitabu,” alisema Charles Mapima Meneja wa elimu TEA
Mbali na vitabu, Mapima alisema kwamba kuna matatizo mengi ndani ya sekta ya elimu kama ukosefu wa mabweni ya wasichana katika na  vitabu kwa shule za msingi na sekondari. 
“Tigo imeonyesha kuwa na nia yakusaidia shule za msingi na kuwapa vitabu. Tuna takwimu kwamba kila kitabu inatumika na wanafunzi hamsini katika shule ya msingi mmoja,”   alienda kusema Mapima 
End

No comments:

Post a Comment