Na Humphrey Shao.
IMEELEZWA kuwa tatizo la mimba za utotoni na utoro mashuleni katika mkoa wa Ruvuma unasababishwa na hali ya umasikini wa kipato cha wananchi wa mkoa huo.
Hayo yamesemwa na wadau na wanaharakati wa mkoa wa ruvuma ambao walihudhuria Warsha ya siku nne iliyo andaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) Mkoani hapo katika taharifa yao iliyotumwa katika vyombo vya habari jana.
Wameeleza kuwa Pia tatizo hili linasababishwa na wananafunzi kutembea umbali mkubwa kutoka nyumbani kwenda shuleni na Wanafunzi kukosa huduma muhimu na hasa chakula cha mchana shuleni na kuwasababishia kukutana na vishawishi wakati wakitafuta chakula .
"Sisi wanajamii kutoka katika Mashirika yasiyo ya kiserikali na Taasisi nyingine za kutetea Haki za Binadamu na Usawa wa Kijinsia, tumeshiriki warsha ya uraghibishi ya kujenga nguvu ya pamoja iliyoendeshwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kuanzia tarehe 28 Juni hdi 1 Julai,2011, na kuibua mambo mbalimbali yanayoikumba jamii ya mkoa wetu Kwa pamoja tunaitaka serikali kusikiliza kilio chetu juu ya changamoto zinazoukumba mkoa wetu na kuchukua hatua za haraka"walieleza wanaharakati hao.
Pia wameitaka serikali kuangalia upya na kufutatilia kwa umakini suala la ugawaji wa pembejeo za kilimo ili zipatikane kwa wakati na usawa kwa kila mmoja kama wakulima na kushughulikia pembejeo zipatikane kwa wakati unaofaa badala ya kuechelewa.
Pia waliitaka Serikali kuhakikisha kuwa mbolea inaletwa mwezi wa nane hadi wa kumi ili tunapokwenda mashambani kulima tuwe tumeshapata mbolea na tunaitaka serikali kufuaatilia zoezi zima la ugawawaji wa mbolea na ujazwaji kwenye mifuko kwani kuna baadhi ya mifuko inakuwa pungufu ipo chini ya kilo.50, mingine inachanganywa na mbolea ya minjingu.
Aidha waliipongeza serikali lakini kwa kuwa imejitahidi kwa kiasi kikubwa kuhamasisha Kilimo kwa nguvu zote kwa ajili ya kuzalisha chakula cha kutosha na kuweka wazi kuwa zoezi hilo limefanikiwa na sasa mkoa wa Ruvuma umeweza kuwa miongoni mwa mikoa michache inayoweza kulisha chakula nchi nzima na hata nje ya nchi.
Mbali na hayo yote wameeleza changamoto kubwa kwa wakulima wadogo Ruvuma ambazo ni Serikali itutafutie masoko ya kueleweka ambapo baada ya kuvuna wakulima waweze kuuza mazao yao kwa haki bila kulanguliwa.
Walimaliza kwa kuelaza kuwa ni vema Serikali idhibiti walanguzi wanaopita mashambani kununua mazao na kuhakikisha inadhibiti bei za chakula masokoni ili mkulima apate faida ya kile alichovuna na asiingie hasara kubwa na kusema kuwa Soko la sodeco bei zake bado haziendani na hali halisi ya bei za chakula hali inayo fanya wakulima tumekuwa tukilanguliwa na kulazimishwa kuuza kwa bei kidogo.
Mwishoooooo
No comments:
Post a Comment