Monday, July 11, 2011

judo KUNA PENGO LA MILIONI 12

Na MWANDISHI WETU

ZIKIWA zimebaki siku tano kufanyika kwa mashindano ya kanda tano Afrika Mashariki ya mchezo wa judo chama cha mchezo wa judo nchini (JATA), kimesema kinahitaji kiasi cha sh.milioni 12 ili kuweza kukamilisha maandalizi ya mashindano hayo.

Mashindano yanatarajia kufanyika Julai 17 hadi 18 katika ukumbi wa Land Mark uliopo Ubungo Dar es Salaam ambapo jumla ya nchi sita zitashiriki ambazo ni Burundi, Kenya, Uganda, Zanzibar ambayo itashiriki kama nchi pekee, Zambia na Tanzania ambao ndio wenyeji.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu mkuu wa JATA Kashinde Shabani alisema, fedha hizo ni kwa ajili ya mahitaji muhimu ya kimashindano ikiwa ni pamoja kuhudumia timu hizo zitakazoshiriki.

"Tukiwa kama wenyeji tunajukumu la kuhakikisha mashindano haya yanafanyika kikamilifu ikiwa ni kwa ajili ya kulinda hadhi ya nchi na heshima ya kupewa hadhi ya kuwa wenyeji hivyo tunaomba Serikali na wadau mbalimbali kuchangia kupatikana kwa fedha hizo ili kufanikisha mashindano hayo," alisema Shabani.

Katibu huyo alisema, maandalizi mengine kwa ajili ya timu ikiwa ni pamoja na vifaa vya michezo yameisha kamalika kwani kwa upande wa vifaa wamealazimika kukusanya vifaa vilivyopo katika klabu mbalimbali za mchezo huo nchini kwa ajili ya kufanyia mashindano hayo baada ya vile vilivyopo bandari kutokujilikana hatma hadi sasa licha ya juhudi mbalimbali za Serikali kufanyika.

Mwisho

No comments:

Post a Comment