Monday, July 4, 2011

Na Humphrey  Shao

WANANCHI wa ishio Kigamboni kata ya gazaulole wamehakikishiwa kupata huduma za kijamii katika mradi mpya wa upimaji viwanaja unao endeshwa na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa wilaya hiyo Bi. Chiku Galawa alipotembelea eneo hilo hili kutoa ufafanuzi kwa wakazi wa eneo hilo na kuwataoa hofu ya kuwa eneo hilo limeuzwa kwa watu kutoka nje ya nchi.

Mkuu Huyo alisema kuwa mradi huo wa upimaji viwanja unalengo la kuboresha makazi ya watu waishio eneo kwa kuweza kufikiwa na huduma muhimu za kijamii kwa urahisi na kuepukana na tatizo la makzi holela ambalo linaweza kutishia ustawi wa mji huo.

“Ni vema mkawa makini na kutoa ushirikiano kwa wapimaji pindi watakapo kuja na kuepuka maneno ya uchochezi ambayo yanaweza kuleta migogoro amabayo aina tija kwa maendeleo ya yenu na Temeke kwa ujumla”alisema Bi.Galawa.

Alisema kuwa mradi huo ambao unalengo la kumnufaisha mkazi wa gezaulole mojakwamoja kwa kupatiwa hati rasmi ya kiwanja mabacho kitapimwa hali itakayowapa fursa ya kuweza kuchukua mikopo sehemeu mbalimbali.

Pia alieleza kuwa wananchi ambao maeneo yao yatatwaliwa yatalipwa kuanzia Mazao,Kiwanja na nyumba ambazo zimejengwa katika shamaba husika pamoja na kupatiwa kiwanja kipya kilichopimwa.

Alisema kuwa zoezi hilo litakapokamilika kutasidia ukuaji kwa kasi wa eneo hilo kutokana idadi ya watu kuongezeka hali itakayofanya gharama za viwanja vyao kupanda na kuweza nyumba zao kupangishwa .

mwishoooo

No comments:

Post a Comment