Monday, July 11, 2011

JESHI LAPOLISI LA WATIA HATIANI WATUHUMIWA 32


Na Humphrey Shao

JESHI la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaamlimefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 32 kwa mokosa yakiwemo kwa kupatikana na silaha pamoja na watuhumiwa wa uhalifu wa kuiba na kuvunja nyumba.

Akizungumza na wandishi wa Habari jiji Dar es salaam jana Kamanda wa upelelezi wa kanda ACP Ahamedi Msangi alisema kuwa watuhumiw hao walikamatwa katika operesheni endelevu inayofanywa na kandamaalum ikiwa ni juhudi za kupambana na uhalifu na kuweka jiji katika hali ya usalama.

Alisema kuwa Mnamo tarehe02 julai 2011 majira ya saamoja na dakika kumi na tisa usiku huko maeneo ya Mbezi kwa yusuph wialaya ya kinondoni askari wa jeshi la Polisi wakiwa doria walifanikiwa kupata silaha aina ya Mark iv yenye namaba za usajili steven model58-d12GAS ikiwa imekatwa mtutu wake pia tulifanikiw akukamata silaha nyingine aina ya Short gunyenye namaba za usajili S.NO.MV-18733H maeneo ya pugu sekondari siku ya 5 julai 2011 amabayo ilitaka kutumika kupora bodaboda .
a
"pia tumefanikiw akukamata watuhumiwa wa ujambazi 6 kwa kutumia pikipiki pamoja na pikipiki 5 kutoka maeneo ya Temeke ,Ilala na Kinondoni na kuwaweka chini ya ulinzi kwa ajili ya uchunguzi zaidi "anaeleza Kamanda Msangi .

Alisema kuwa watuhumiwa hao ni Tito Mkasiogwa(30),John Ndogo(18),Ally Jumamosi(18) wengine ni Ibrahim Shabani (20),Mwalimu Omari(36) na Rashidi Kassim.

Katika tukio lingine kikosi cha kupambana na uwizi wa magari kanda ya Dar es salaam wamefanikiwa kukamata magari 10 ambayo yaliibiwa jijini na kupatikana katika miji ya Kahama na Shinyanga, ambapo magari hayo yalikuwa yameuzwa kwa watu binafsi.

Alitaja kuwa magari hayo ni Toyota Nadia yenye namba za usajili T889BJJ,Toyota RAV4 T488AYY,Premio Corona T.682AEB,Spacio T796 BLZ,Corola T170 ABD,Cresta GX100 T916AEE,

Hata hivyo jeshi lapolisi kupitia Kaimu kamanda wa kaanda maalumu Abdul Issa limewatahadharisha wakazi wa jiji na makampuni ambayo yanasafirisha pesa kiholela bila kusindikiwa na polisi kuwa inahatarisha uaslama wa fedha hizo .

Kamanda huyo amaeleza kuwa kutokana na tukio la kuibiwa fedha marakwa mara ni vem,a watu wakawa wa siri ama kufika jeshi la polisi hili kuweza kupata msaada wa kusindikizwa na huduma hiyo inatolewa bure na jeshi hili kuloko watu kurisk pesa hizo.

No comments:

Post a Comment