Sunday, August 21, 2011

UTAWALA WA GADDAFI UMEANGUKA!


Kila chenye mwanzo kina mwisho. Blogu hii iliandika siku chache zilizopita juu ya kuwepo kwa taarifa za Ki-Intelijensia zilizotabainisha kuwa utawala wa Gaddafi ungeanguka ndani ya siku chache. Na imekuwa hivyo.

Usiku wa kuamkia leo wapiganaji waliokuwa wakipambana na vikosi vya Gadaffi hatimaye wameitwaa Tripoli.  Walibya kwa mamia  waaripotiwa kuingia mitaani kusheherekea ukombozi kutoka kwa utawala wa kidikteta na kikandamizaji. Watu wameonekana wakichoma moto picha za Gaddafi.

Inasemekana wana wa Gaddafi akiwamo Seif Islam ambaye alitarajiwa angemrithi baba yake wako sasa wamekamatwa na wapiganaji hao. Gaddafi mwenyewe hajulikani alipo. Uwanja wa ndege wa Libya kuna ndege mbili ambazo zinadhaniwa Gaddafi angezitumia kuondoka nchini akiwa na familia yake. Gaddafi angekimbilia wapi? Nchi za Zimbabwe na Angola zinatajwa kuwa zingeweza kuwa kimbilio la Gaddafi. Taarifa zaidi zitawajia kadri zitakavyopatikana.

No comments:

Post a Comment