Thursday, August 18, 2011

Thursday, August 18, 2011 *STARS KUKIPIGA NA ALGERIA JIJINI MWANZA SEPTEMBA 3 Katibu Mkuu wa Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania, Angetile Osiah. Mechi ya mchujo ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN) zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon katika ya timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Algeria (Desert Warriors) itachezwa Septemba 3 mwaka huu jijini Mwanza. Awali tulipanga mechi hiyo ichezwe Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Lakini uamuzi wa kuihamishia Mwanza umefanyika baada ya jana kupata barua kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ikitufahamisha kuwa Uwanja wa Taifa hautatumika tena kwa sasa. Kwa mujibu wa Wizara, uwanja huo utakuwa katika matengenezo baada ya kuharibika wakati wa michuano ya Kombe la Kagame iliyofanyika mwanzoni mwa mwezi uliopita. YANGA, SIMBA NAZO KUATHIRIKA Uamuzi huo wa uwanja kufungwa kwa ajili ya matengenezo pia umeziathiri klabu za Yanga na Simba ambazo zilikuwa zimekubaliwa timu zao zitumie kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom ambayo inaanza kutimua vumbi Agosti 20 mwaka huu. Tayari leo (Agosti 18 mwaka huu) tumeziandikia rasmi klabu za Simba na Yanga kuzifahamisha kuhusu uamuzi huo wa Wizara, hivyo kuzitaka zitafute viwanja vingine kwa ajili ya mechi zao za ligi. Hatua hiyo ya uwanja kufungwa, itailazimisha TFF ifanye mabadiliko kwenye ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom kwa kuzingatia viwanja ambavyo klabu za Yanga na Simba zitakuwa zimeamua kuvitumia. Mabadiliko hayo pia yataziathiri timu za African Lyon, Azam, JKT Ruvu, Moro United na Villa Squad ambazo licha ya kutumia Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam, zilipanga mechi zao za nyumbani dhidi ya Simba na Yanga zichezwe Uwanja wa Taifa. Kwa sasa msimamo wa wamiliki wa Uwanja wa Azam ni Yanga na Simba kutoutumia kwa vile uwezo wake wa kuchukua watazamaji ni mdogo. Boniface Wambura, Ofisa Habari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imewekwa na : MUHIDIN SUFIANI Muda: Thursday, August 18, 2011 0 idadi ya maoni Links to this post *BASI LA SABCO LAPATA AJALI IRINGA Basi la kampuni ya Sabco linalofanya safari zake Mbeya-Dar, lililokuwa likitoka Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya, kuja jijini Dar es Salaam limepata ajali eneo la Tanangozi wilaya ya Iringa vijijini baada ya tairi la basi hilo kupasuka. Imeelezwa kuwa katika ajali hiyo abiria kadhaa wamejeruhiwa. Mmoja wa abiri aliyekuwa akisafiri na Basi hilo, akijaribu kutafuta mawasiliano ya simu ili kutoa taarifa kwa ndugu na jamaa baada ya ajali hiyo. imewekwa na : MUHIDIN SUFIANI Muda: Thursday, August 18, 2011 0 idadi ya maoni Links to this post *BARAZA LA MAWAZIRI LAIHENYESHA EWURA MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Haruna Masebu,amehenyeshwa kwa kuhojiwa kwa undani na Baraza la Mawaziri kuhusu kuyumbisha bei ya mafuta. Baraza hilo lilitaka kujua kwa nini mamlaka hiyo imekuwa ikiyumbisha nchi na wananchi kuhusu bei za mafuta. Kwa zaidi ya saa moja, Masebu na wasaidizi wake waliwekwa kiti moto kuhusu bei zilizotangazwa na Ewura mwishoni mwa wiki, ambazo zimepanda kwa asilimia sita kutoka zile zilizotangazwa awali. Habari za kuaminika kutoka kwenye mkutano wa Baraza la Mawaziri uliofanyika jana kwenye Ukumbi wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, mjini Dodoma zinasema kuwa waziri mmoja baada ya mwingine alimhoji Masebu na wasaidizi wake kuhusu mwenendo usioridhisha wa bei za mafuta nchini. Habari zinasema kuwa Masebu ambaye aliingia kwenye ukumbi huo akionesha kujiamini, alianza kupoteza mwelekeo kwa kadri maswali yalivyokuwa yakimiminika kutoka kwa mawaziri. Hatimaye siyo yeye mwenyewe ama yoyote kati ya wasaidizi wake ambaye alikuwa na majibu ya kutosheleza ama hata ya kuwashawishi mawaziri kuhusu hatua hizo za Ewura na kwa kadri kikao hicho kilivyoendelea, Masebu na wenzake walionekana kukosa hoja. Habari zinasema kuwa Masebu na wasaidizi wake walitakiwa kujielezea mbele ya Baraza la Mawaziri ili kuliwezesha Baraza hilo, chini ya Uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete, kujiridhisha na mwenendo mzima wa bei mafuta. Baraza hilo lilitaka ufafanuzi kuhusu bei za petroli, mafuta ya taa na dizeli, nishati ambazo ukosefu wake nusura uiingize nchi katika zahama kubwa wiki iliyopita. Moja ya maswali ya awali kutoka kwa Baraza la Mawaziri ilikuwa ni kwa nini Masebu na Ewura walitangaza kupanda tena kwa bei za mafuta siku chache baada ya kuzishusha kwa asilimia 9.17 kwa petroli, asilimia 8.31 kwa dizeli na asilimia 8.70 kwa bei ya mafuta ya taa. Hatua hiyo ya Ewura kupunguza bei ya mafuta ilikuwa inatekeleza uamuzi na maagizo ya Serikali yaliyotangazwa na Waziri wa Fedha, Mustafa Mkullo Juni 22, mwaka huu, bungeni wakati alipowasilisha Bajeti ya Serikali. Katika bajeti hiyo, Mkullo alisema kuwa Serikali iliamua kuondoa kodi na tozo kadhaa kwenye bei ya mafuta yanayoingizwa nchini kwa nia ya kupunguza bei ya bidhaa hizo ili kumpungumzia makali ya maisha mwananchi. Hatua hiyo ya Mkullo, pamoja na ile ya Ewura kupunguza bei za mafuta ziliungwa mkono na Bunge na wananchi kwa kiwango kikubwa ambao walikiri kuwa hatua hiyo ilithibitisha jinsi gani Serikali yao inavyowajali. Hatua ya Ewura kupunguza bei ya mafuta ilipingwa na kampuni karibu zote kubwa za kuingiza mafuta nchini ambazo zilianzisha mgomo kupinga hatua hiyo hasa BP, Engen, Oilcom na Camel Oil. Baada ya siku moja ya mgomo huo, kampuni zingine nchini zilianza tena kuuza mafuta, lakini kampuni hizo nne zilikataa kufungua vituo vyao kuuza mafuta. Agosti 9, mwaka huu, Ewura ilitoa amri ya Kimahakama (Compliance Order), kwa kampuni hizo nne kuanza mara moja kutoa huduma katika maghala yao na katika vituo vya rejareja vikiwemo vile vilivyoko chini ya miliki zao. Katika amri hiyo, kampuni hizo zilitakiwa kuacha mara moja kusababisha upungufu wa makusudi wa mafuta ya petroli katika soko la Tanzania na kujieleza katika saa 24 kwa nini wasichukuliwe hatua za kisheria kwa kukiuka matakwa ya Sheria ya Mafuta na Utaratibu wa Ewura. Siku iliyofuata, kampuni tatu zilianza kutoa huduma lakini BP (T) Ltd iliendelea kukaidi amri ya Ewura. Bodi ya Ewura katika kikao chake cha Agosti 12, ilichukua hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kutoa onyo kali kwa kampuni za Oilcom, Camel Oil na Engen, na kuisitishia BP leseni ya biashara ya jumla ya mafuta kwa miezi mitatu na kuamuru Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo na mwenyekiti wake wa bodi wafikishwe kortini. Lakini katika muda wa saa 48 tu, baada ya hatua hiyo ambayo iliungwa mkono na nchi nzima, Ewura ilibadilisha msimamo na mwelekeo wake na kutangaza kupandisha tena bei ya mafuta hayo ya petroli, dizeli na taa kwa asilimia tano. Hatua hiyo ya Ewura, ilisababisha hasira ya Serikali yenyewe, Bunge, wabunge na wananchi kwa jumla. “Ulichofanikiwa kufanya Masebu ni kuharibu kabisa mamlaka na madaraka ya Ewura. Hii ni taasisi ambayo ilikuwa imeanza kujijengea heshima kubwa kwa wananchi kwa kuchukua hatua mwafaka, na sasa mmevuruga kabisa heshima hiyo ya Ewura. “Kwa kuvuruga heshima ya taasisi hiyo mmezitia doa siasa za nchi yetu,” waziri mmoja alimwambia ana kwa ana Masebu katika mkutano huo. Masebu alijaribu kujitetea kwa kusema kuwa upandishaji huo wa bei ya mafuta uliofanywa na Ewura kwa mujibu wa Sheria na kwa mujibu wa makubaliano ya kuangalia upya bei kila baada ya wiki mbili kwa sababu mafuta huingizwa nchini kutoka Uarabuni kila baada ya wiki mbili. Lakini Masebu aliambiwa kuwa hakuna mafuta yoyote yaliyoingizwa nchini tangu mvutano ulipoanza kati ya Ewura na kampuni za mafuta baada ya tangazo la kupunguza bei ya mafuta la Agosti Mosi, mwaka huu. “Mheshimiwa Mwenyekiti ni mafuta yapi yameingia nchini kutoka Uarabuni katika wiki mbili zilizopita kwa sababu katika muda wote kwanza ulikuwepo mgomo wa kampuni za mafuta uliokolezwa zaidi na kampuni zile kubwa nne. “Katika kipindi hiki, hakuna mafuta yaliyoingia nchini kwa sababu mafuta yalikuwepo kwenye matangi ya maghala na hayakuuzwa. Sasa Mkurugenzi anatuambia mafuta haya mapya yametoka wapi?” Alihoji waziri mmoja na kuongeza; “Walichofanya Ewura ni kupandisha bei ya mafuta ambayo yalikuwa yamekwishafika nchini kabla ya mzozo kuanza mwanzoni mwa Agosti mwaka huu,” alisema waziri huyo. Masebu alipojaribu kujitetea kuwa kwa taratibu za Ewura ni lazima bei za mafuta zipitiwe upya kila baada ya wiki mbili, waziri mwingine aliingia kati na kumwuliza: “Mnapitia tu hata kama hakuna mafuta mapya yaliyoingizwa nchini kama ilivyotokea katika wiki mbili zilizopita? Mnafanya kazi kama mashine bila kutilia maanani hali halisi?” Alihoji. Waziri mwingine alionya kuwa vitendo vya Ewura katika wiki mbili zilizopita vililenga kuyumbisha nchi na kuipeleka pabaya bila sababu za msingi. “Inaelekea nyie Ewura mnahangaika zaidi kutetea maslahi ya wafanyabishara kuliko maslahi ya wananchi wetu,” alisema Waziri huyo. imewekwa na : MUHIDIN SUFIANI Muda: Thursday, August 18, 2011 0 idadi ya maoni Links to this post *WAREMBO WA VODACOM MISS TANZANIA WATEMBELEA HIFADHI YA TARANGIRE Warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2011, wakiwa katika hifadhi ya taifa ya Tarangire, mkoani Manyara jana walipokwenda kujionea wanyama na vivutio mbalimbali vya utalii katika hifadhi hiyo ya tano kwa ukubwa nchini. Warembo hao wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio vya utalii na kuhamasisha utalii wa ndani kwa watanzania. Katika hatua nyingine leo Miss Photogenic anataraji kutangwazwa na kujipatia tiketi ya kuingia katika nusu fainali ya shindano la Vodacom Miss Tanzania, ambapo Miss Photogenic atakuwa ni mrembo wa pili kuingia katika hatua hiyo ya 15 bora baada ya Top Model. Picha na Father Kidevu Blog Mshiriki wa Vodacom Miss Tanzania Zelulia Manoko, akizungumza kwa niaba ya wenzake baada ya kufika katika lango kuu la kuingilia hifadhi ya taifa ya Tarangire mkoani Manyara jana na kujionea wanyama wa aina mbalimbali. Warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2011, wakiingia katika lango Kuu la hifadhi ya taifa ya Tarangire mkoani Manyara jana walipofika kujionea wanyama na vivutio mbalimbali vya utalii katika hifadhi hiyo ambayo ni ya tano kwa ukubwa nchini. imewekwa na : MUHIDIN SUFIANI Muda: Thursday, August 18, 2011 0 idadi ya maoni Links to this post *SIMBA YAFUTA UTEJA YAIBAMIZA YANGA 2-0 MCHEZO WA NGAO YA HISANI Nahodha wa timu ya Simba, Juma Kaseja, akipokea na kuibusu Ngao ya Jamii, baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga, mchezo uliochezwa jana usiku kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo magoli yote yalipatikana kipindi cha kwanza huku goli la kwanza likifungwa na Kiungo wa timu hiyo, Haruna Moshi 'Boban' na la pili likiwekwa kimiani na Felix Sunzu kwa mkwaju wa penati baada ya Boban kuchezewa faulo eneo la hatari. Warembo wakibeba Ngao ya Jamii kupeleka jukwaani kwa ajili ya kukabidhi kwa timu mshindi Simba. Wachezaji wa Simba, wakimbeba mwenzao Patrick Mafisango na kumpongeza baada ya kutangazwa kuwa nyota wa mchezo huo, ambapo alikabidhiwa zawadi na Benki ya NMB. Mashabiki wa Yanga, wakishangilia huku wakiwa na picha yenye mchoro wa kuwakebehi watani wao wa Jadi Simba, kabla ya kuanza kwa mtanange huo. Mashabiki wa Simba, wakishangilia huku wakiburudika na miondoko ya Vuvuzela kabla ya kuanza kwa mtanange huo. Winga wa Yanga, Godfrey Taita (kushoto) akijipinda kupiga krosi huku akizuiwa na Patrick Mafisango, wakati wa mchezo huo. Mchezaji wa Yanga, Hamis Kiiza (kulia) akijaribu kumtoka beki wa Simba, Nasor Chollo, wakati wa mchezo huo. Kiiza aliingia kipindi cha pili na kufanya mambo makubwa huku akiwanyanyasa mabeki wa Simba akishirikiana na rashid Gumbo, ambapo walionekana kubadilisha kabisa sura ya mchezo huo. Haruna Niyonzima wa Yanga (kulia) akimtoka beki wa Simba Nasor Chollo. Mashabiki wa Simba wakishangilia baada ya timu yao kupata bao la kwanza. Beki wa Simba Victor Costa (kushoto) akimdhibiti, Keneth Asamoh wa Yanga. Haruna Niyonzima wa Yanga (kushoto) akiwatoka mabeki wa simba wakati wa mchezo huo. Mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete (kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa Simba, Victor Coster. Tegete, akienelea kumtesa Costa. Tegete, akijaribu kupenya katikati ya msitu wa mabeki wa Simba.... Boban, akitibiwa nje ya uwanja baada ya kuchezewa faulo iliyozaa penati, lakini katika CHUPA hii aliyoshika mkononi ni aina gani ya kinywaji anakunywa? Tazama kwa makini kisha nipe jibu, sijawahi ona maji yenye rangi hii bwana alaaah! Kipa wa Yanga Shaban Kado, akijaribu kuokoa mkwaju wa penati iliyopigwa na Felix Sunzu, ambayo hata hivyo ilitinga wavuni na kukataliwa na mwamuzi wa mchezo huo aliyeamuru kurudiwa kwa penati hiyo. Sunsu na Okwi, wakishangilia baada ya sunsu kufunga kwa penati. Mashabiki wa Simba wakiwa na furaha ya ushindi. Jerry Tegete, akiruka kupiga kichwa katikati ya mabeki wa Simba, lakini hata hivyo shuti hilo la kichwa lilipaa juu ya goli. Hamis Kiiza, akijipinda kupiga kichwa katikati ya msitu wa mabeki wa Simba. Furaha ya ushindi kwa mashabiki wa Simba. Hamis Kiiza wa Yanga (kulia) akichuana na beki wa Simba Nasor Chollo. Kiungo wa Yanga, Rashid Gumbo, akimfinya Amri Kiemba na kumtoka. Beki wa Simba, Nasor Chollo, akimdhibiti mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete. Boban akichanja mbuga (kulia) ni beki wa Yanga Shadrack Nsajigwa, akipiga hesabu za kumdhibiti. Hamis Kiiza akiomba dua kabla ya kuingia uwa


 

*BASI LA SABCO LAPATA AJALI IRINGA

 Basi la kampuni ya Sabco linalofanya safari zake Mbeya-Dar, lililokuwa likitoka Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya, kuja jijini Dar es Salaam limepata ajali eneo la Tanangozi wilaya ya Iringa vijijini baada ya tairi la basi hilo kupasuka. 
Imeelezwa kuwa katika ajali hiyo abiria kadhaa wamejeruhiwa.
Mmoja wa abiri aliyekuwa akisafiri na Basi hilo, akijaribu kutafuta mawasiliano ya simu ili kutoa taarifa kwa ndugu na jamaa baada ya ajali hiyo.

*BARAZA LA MAWAZIRI LAIHENYESHA EWURA


MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Haruna Masebu,amehenyeshwa kwa kuhojiwa kwa undani na Baraza la Mawaziri kuhusu kuyumbisha bei ya mafuta. 

Baraza hilo lilitaka kujua kwa nini mamlaka hiyo imekuwa ikiyumbisha nchi na wananchi kuhusu bei za mafuta. 

Kwa zaidi ya saa moja, Masebu na wasaidizi wake waliwekwa kiti moto kuhusu bei zilizotangazwa na Ewura mwishoni mwa wiki, ambazo zimepanda kwa asilimia sita kutoka zile zilizotangazwa awali. 

Habari za kuaminika kutoka kwenye mkutano wa Baraza la Mawaziri uliofanyika jana kwenye Ukumbi wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, mjini Dodoma zinasema kuwa waziri mmoja baada ya mwingine alimhoji Masebu na wasaidizi wake kuhusu mwenendo usioridhisha wa bei za mafuta nchini. 

Habari zinasema kuwa Masebu ambaye aliingia kwenye ukumbi huo akionesha kujiamini, alianza kupoteza mwelekeo kwa kadri maswali yalivyokuwa yakimiminika kutoka kwa mawaziri. 

Hatimaye siyo yeye mwenyewe ama yoyote kati ya wasaidizi wake ambaye alikuwa na majibu ya kutosheleza ama hata ya kuwashawishi mawaziri kuhusu hatua hizo za Ewura na kwa kadri kikao hicho kilivyoendelea, Masebu na wenzake walionekana kukosa hoja. 

Habari zinasema kuwa Masebu na wasaidizi wake walitakiwa kujielezea mbele ya Baraza la Mawaziri ili kuliwezesha Baraza hilo, chini ya Uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete, kujiridhisha na mwenendo mzima wa bei mafuta. 

Baraza hilo lilitaka ufafanuzi kuhusu bei za petroli, mafuta ya taa na dizeli, nishati ambazo ukosefu wake nusura uiingize nchi katika zahama kubwa wiki iliyopita. 

Moja ya maswali ya awali kutoka kwa Baraza la Mawaziri ilikuwa ni kwa nini Masebu na Ewura walitangaza kupanda tena kwa bei za mafuta siku chache baada ya kuzishusha kwa asilimia 9.17 kwa petroli, asilimia 8.31 kwa dizeli na asilimia 8.70 kwa bei ya mafuta ya taa. 

Hatua hiyo ya Ewura kupunguza bei ya mafuta ilikuwa inatekeleza uamuzi na maagizo ya Serikali yaliyotangazwa na Waziri wa Fedha, Mustafa Mkullo Juni 22, mwaka huu, bungeni wakati alipowasilisha Bajeti ya Serikali. 

Katika bajeti hiyo, Mkullo alisema kuwa Serikali iliamua kuondoa kodi na tozo kadhaa kwenye bei ya mafuta yanayoingizwa nchini kwa nia ya kupunguza bei ya bidhaa hizo ili kumpungumzia makali ya maisha mwananchi.

Hatua hiyo ya Mkullo, pamoja na ile ya Ewura kupunguza bei za mafuta ziliungwa mkono na Bunge na wananchi kwa kiwango kikubwa ambao walikiri kuwa hatua hiyo ilithibitisha jinsi gani Serikali yao inavyowajali. 

Hatua ya Ewura kupunguza bei ya mafuta ilipingwa na kampuni karibu zote kubwa za kuingiza mafuta nchini ambazo zilianzisha mgomo kupinga hatua hiyo hasa BP, Engen, Oilcom na Camel Oil. 

Baada ya siku moja ya mgomo huo, kampuni zingine nchini zilianza tena kuuza mafuta, lakini kampuni hizo nne zilikataa kufungua vituo vyao kuuza mafuta. 

Agosti 9, mwaka huu, Ewura ilitoa amri ya Kimahakama (Compliance Order), kwa kampuni hizo nne kuanza mara moja kutoa huduma katika maghala yao na katika vituo vya rejareja vikiwemo vile vilivyoko chini ya miliki zao. 

Katika amri hiyo, kampuni hizo zilitakiwa kuacha mara moja kusababisha upungufu wa makusudi wa mafuta ya petroli katika soko la Tanzania na kujieleza katika saa 24 kwa nini wasichukuliwe hatua za kisheria kwa kukiuka matakwa ya Sheria ya Mafuta na Utaratibu wa Ewura. 

Siku iliyofuata, kampuni tatu zilianza kutoa huduma lakini BP (T) Ltd iliendelea kukaidi amri ya Ewura. Bodi ya Ewura katika kikao chake cha Agosti 12, ilichukua hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kutoa onyo kali kwa kampuni za Oilcom, Camel Oil na Engen, na kuisitishia BP leseni ya biashara ya jumla ya mafuta kwa miezi mitatu na kuamuru Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo na mwenyekiti wake wa bodi wafikishwe kortini. 

Lakini katika muda wa saa 48 tu, baada ya hatua hiyo ambayo iliungwa mkono na nchi nzima, Ewura ilibadilisha msimamo na mwelekeo wake na kutangaza kupandisha tena bei ya mafuta hayo ya petroli, dizeli na taa kwa asilimia tano. Hatua hiyo ya Ewura, ilisababisha hasira ya Serikali yenyewe, Bunge, wabunge na wananchi kwa jumla. 

“Ulichofanikiwa kufanya Masebu ni kuharibu kabisa mamlaka na madaraka ya Ewura. Hii ni taasisi ambayo ilikuwa imeanza kujijengea heshima kubwa kwa wananchi kwa kuchukua hatua mwafaka, na sasa mmevuruga kabisa heshima hiyo ya Ewura. 

“Kwa kuvuruga heshima ya taasisi hiyo mmezitia doa siasa za nchi yetu,” waziri mmoja alimwambia ana kwa ana Masebu katika mkutano huo. 

Masebu alijaribu kujitetea kwa kusema kuwa upandishaji huo wa bei ya mafuta uliofanywa na Ewura kwa mujibu wa Sheria na kwa mujibu wa makubaliano ya kuangalia upya bei kila baada ya wiki mbili kwa sababu mafuta huingizwa nchini kutoka Uarabuni kila baada ya wiki mbili. 

Lakini Masebu aliambiwa kuwa hakuna mafuta yoyote yaliyoingizwa nchini tangu mvutano ulipoanza kati ya Ewura na kampuni za mafuta baada ya tangazo la kupunguza bei ya mafuta la Agosti Mosi, mwaka huu. 

“Mheshimiwa Mwenyekiti ni mafuta yapi yameingia nchini kutoka Uarabuni katika wiki mbili zilizopita kwa sababu katika muda wote kwanza ulikuwepo mgomo wa kampuni za mafuta uliokolezwa zaidi na kampuni zile kubwa nne. 

“Katika kipindi hiki, hakuna mafuta yaliyoingia nchini kwa sababu mafuta yalikuwepo kwenye matangi ya maghala na hayakuuzwa. Sasa Mkurugenzi anatuambia mafuta haya mapya yametoka wapi?” Alihoji waziri mmoja na kuongeza;

 “Walichofanya Ewura ni kupandisha bei ya mafuta ambayo yalikuwa yamekwishafika nchini kabla ya mzozo kuanza mwanzoni mwa Agosti mwaka huu,” alisema waziri huyo. Masebu alipojaribu kujitetea kuwa kwa taratibu za Ewura ni lazima bei za mafuta zipitiwe upya kila baada ya wiki mbili, waziri mwingine aliingia kati na kumwuliza: 

“Mnapitia tu hata kama hakuna mafuta mapya yaliyoingizwa nchini kama ilivyotokea katika wiki mbili zilizopita? Mnafanya kazi kama mashine bila kutilia maanani hali halisi?” Alihoji. Waziri mwingine alionya kuwa vitendo vya Ewura katika wiki mbili zilizopita vililenga kuyumbisha nchi na kuipeleka pabaya bila sababu za msingi. 

“Inaelekea nyie Ewura mnahangaika zaidi kutetea maslahi ya wafanyabishara kuliko maslahi ya wananchi wetu,” alisema Waziri huyo.

*WAREMBO WA VODACOM MISS TANZANIA WATEMBELEA HIFADHI YA TARANGIRE

 Warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2011, wakiwa katika hifadhi ya taifa ya Tarangire, mkoani Manyara jana walipokwenda kujionea wanyama na vivutio mbalimbali vya utalii katika hifadhi hiyo ya tano kwa ukubwa nchini. 
Warembo hao wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio vya utalii na kuhamasisha utalii wa ndani kwa watanzania. 
Katika hatua nyingine leo Miss Photogenic anataraji kutangwazwa na kujipatia tiketi ya kuingia katika nusu fainali ya shindano la Vodacom Miss Tanzania, ambapo Miss Photogenic atakuwa ni mrembo wa pili kuingia katika hatua hiyo ya 15 bora baada ya Top Model. Picha na Father Kidevu Blog
 Mshiriki wa Vodacom Miss Tanzania Zelulia Manoko, akizungumza kwa niaba ya wenzake baada ya kufika katika lango kuu la kuingilia hifadhi ya taifa ya Tarangire mkoani Manyara jana na kujionea wanyama wa aina mbalimbali.   
Warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2011, wakiingia katika lango Kuu la hifadhi ya taifa ya Tarangire mkoani Manyara jana walipofika kujionea wanyama na vivutio mbalimbali vya utalii katika hifadhi hiyo ambayo ni ya tano kwa ukubwa nchini. 

*SIMBA YAFUTA UTEJA YAIBAMIZA YANGA 2-0 MCHEZO WA NGAO YA HISANI

 Nahodha wa timu ya Simba, Juma Kaseja, akipokea na kuibusu Ngao ya Jamii, baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga, mchezo uliochezwa jana usiku kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo magoli yote yalipatikana kipindi cha kwanza huku goli la kwanza likifungwa na Kiungo wa timu hiyo, Haruna Moshi 'Boban' na la pili likiwekwa kimiani na Felix Sunzu kwa mkwaju wa penati baada ya Boban kuchezewa faulo eneo la hatari. 
 Warembo wakibeba Ngao ya Jamii kupeleka jukwaani kwa ajili ya kukabidhi kwa timu mshindi Simba.
 Wachezaji wa Simba, wakimbeba mwenzao Patrick Mafisango na kumpongeza baada ya kutangazwa kuwa nyota wa mchezo huo, ambapo alikabidhiwa zawadi na Benki ya NMB.
 Mashabiki wa Yanga, wakishangilia huku wakiwa na picha yenye mchoro wa kuwakebehi watani wao wa Jadi Simba, kabla ya kuanza kwa mtanange huo.
 Mashabiki wa Simba, wakishangilia huku wakiburudika na miondoko ya Vuvuzela kabla ya kuanza kwa mtanange huo.
 Winga wa Yanga, Godfrey Taita (kushoto) akijipinda kupiga krosi huku akizuiwa na Patrick Mafisango, wakati wa mchezo huo.
 Mchezaji wa Yanga, Hamis Kiiza (kulia) akijaribu kumtoka beki wa Simba, Nasor Chollo, wakati wa mchezo huo. Kiiza aliingia kipindi cha pili na kufanya mambo makubwa huku akiwanyanyasa mabeki wa Simba akishirikiana na rashid Gumbo, ambapo walionekana kubadilisha kabisa sura ya mchezo huo.
 Haruna Niyonzima wa Yanga (kulia) akimtoka beki wa Simba Nasor Chollo.
 Mashabiki wa Simba wakishangilia baada ya timu yao kupata bao la kwanza.
 Beki wa Simba Victor Costa (kushoto) akimdhibiti, Keneth Asamoh wa Yanga.
 Haruna Niyonzima wa Yanga (kushoto) akiwatoka mabeki wa simba wakati wa mchezo huo.
 Mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete (kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa Simba, Victor Coster.
 Tegete, akienelea kumtesa Costa.
 Tegete, akijaribu kupenya katikati ya msitu wa mabeki wa Simba....
 Boban, akitibiwa nje ya uwanja baada ya kuchezewa faulo iliyozaa penati, lakini katika CHUPA hii aliyoshika mkononi ni aina gani ya kinywaji anakunywa? Tazama kwa makini kisha nipe jibu, sijawahi ona maji yenye rangi hii bwana alaaah!
 Kipa wa Yanga Shaban Kado, akijaribu kuokoa mkwaju wa penati iliyopigwa na Felix Sunzu, ambayo hata hivyo ilitinga wavuni na kukataliwa na mwamuzi wa mchezo huo aliyeamuru kurudiwa kwa penati hiyo.
 Sunsu na Okwi, wakishangilia baada ya sunsu kufunga kwa penati.
 Mashabiki wa Simba wakiwa na furaha ya ushindi.
 Jerry Tegete, akiruka kupiga kichwa katikati ya mabeki wa Simba, lakini hata hivyo shuti hilo la kichwa lilipaa juu ya goli.
 Hamis Kiiza, akijipinda kupiga kichwa katikati ya msitu wa mabeki wa Simba.
 Furaha ya ushindi kwa mashabiki wa Simba.
 Hamis Kiiza wa Yanga (kulia) akichuana na beki wa Simba Nasor Chollo.
 Kiungo wa Yanga, Rashid Gumbo, akimfinya Amri Kiemba na kumtoka.
 Beki wa Simba, Nasor Chollo, akimdhibiti mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete.
 Boban akichanja mbuga (kulia) ni beki wa Yanga Shadrack Nsajigwa, akipiga hesabu za kumdhibiti.
 Hamis Kiiza akiomba dua kabla ya kuingia uwanjani na kuwanyanyasa mabeki wa Simba.
Wachezaji wa Simba wakishangilia. "Raha ya ushindi Bao"........baada ya mchezo huo kumalizika.

No comments:

Post a Comment