Wednesday, August 24, 2011

*VODACM YATOA FURSA KWA WATANZANIA KUWAPIGIA KURA WASHIRIKI WA VODACM MISS TANZANIA

Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom, Tanzania imetoa fursa kwa Watanzania kuweza kupiga kura na kuchagua mrembo anayevutia zaidi kati ya warembo 30 wanaoshiriki  shindano la kumsaka Vodacom Miss Tanzania 2011.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Udhamini wa Vodacom ,George Rwehumbiza, alisema ili kupiga kura Watanzania watatakiwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno wenye neno MREMBO ukifuatiwa na namba ya mshiriki 'mfano  40'  kwenda 15550 ambapo gharama kwa kila ujumbe ni shilingi 150 tu .

Aidha Rwehumbiza, aliongeza kuwa kila ujumbe mfupi utakaotumwa utampatia Mtanzania pointi 10 ambapo wateja 20 watakaobahatika kuwa na pointi nyingi zaidi kila mmoja atajipatia TIKETI mbili za VIP zitakazomwezesha kwenda kushuhudia fainali ya shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, itakayofanyika tarehe 10 mwezi septemba katika ukumbi wa  Mlimani city jijini Dares salaam.

Pia kwa wale watakaohitaji kutoa maoni au mitazamo yao mbalimbali kuhusu Vodacom Miss Tanzania watapata fursa ya kutuma ujumbe mfupi wa maneno wenye neno MREMBO ukifuatiwa na maoni kwenda namba 15550.

Akisisitiza hili  Rwehumbiza, alisema ili kuwafahamu warembo wanaoshindania taji la Vodacom Miss Tanzania 2011, Watanzania wote wanaweza kuangalia kituo cha Televisheni cha STAR TV leo kuanzia muda wa saa moja jioni pamoja na CLOUDS TV muda wa saa tatu usiku kila siku pia soma magazeti ya Mtanzania, The African, Dimba, Rai na Bingwa.
.

BASATA YAHIMIZA MSHIKAMANO WA WASANII

Katibu wa Shirikisho la Filamu (TAFF) Wilson Makubi akizungumza na wadau wa Jukwaa la Sanaa kuhusu uzoefu wake katika Bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo iliyowasilishwa hivi karibuni. Wengine kulia kwake ni Katibu wa Shirikisho la Sanaa za Maonyesho Dennis Mango na Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufunfi, Adrian Nyangamale

Mkongwe wa muziki wa dansi nchini Kassim Mapili akieleza jinsi viongozi wa mashirikisho ya sanaa nchini walivyopata fursa ya kuongea na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda kuhusu umuhimu wa sekta ya sanaa wakati walipomtembelea bungeni Dodoma hivi karibuni.
Wadau wa Jukwaa la Sanaa wakiwa wamesimama kumkumbuka Msanii Mahadiya Ally aliyefariki Dunia Usiku wa kuamkia Jumapili na kuzikwa Jumatatu wiki hii Mkoani Tanga.
Na Mwandishi Wetu
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka wasanii kujenga ushirikiano kupitia vyama na mashirikisho yao ili kuhakikisha kunakuwa na mfumo rasmi na unaoeleweka wa uendeshaji wa tasnia ya sanaa nchini.
Rai hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego wakati akiliahirisha Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila Jumatatu kwenye Ukumbi wa Baraza hilo ambapo alisema kwamba,wasanii wamekuwa walalamishi tu pasipokuchukua hatua na kuleta mabadiliko ndani ya tasnia.
“Wasanii turudi nyuma katika vyama vyetu, tujiulize kama vyama vyetu viko hai na sisi tuko ndani. Tumekuwa tukilalamika sana, malalamiko mengine ni sahihi na mengine si sahihi. Wakati umefika  wa kuleta mabadiliko” alisema Materego.
Aliongeza kwamba,uwepo wa wasanii wengi hapa nchini pasipokuwa na mfumo unaowaunganisha na kuwaweka pamoja hakutakuwa na maana yoyote hivyo kuna kila sababu ya wasanii wenyewe kuamka na kuujenga mfumo huo.
“Hebu hapa tujiulize ni wasanii wangapi wako katika vyama? Sasa ni kwa vipi sauti yako itasikika wakati hauko katika umoja? Ni lazima turudi nyuma na tujipange katika vyama vyetu na kuyapa nguvu mashirikisho. Tusizungumzie mfumo wakati sisi wenyewe tuko nje ya mfumo” alitoa rai Materego.
Alizidi kueleza kwamba, BASATA katika mwaka huu wa fedha imejipanga kuendesha chaguzi za mashirikisho yote ya sanaa nchini na kuwataka wasanii kujipanga katika vyama vyao na kuhakikisha vinakuwa hai kwa ajili ya kujenga mfumo utakaoleta mageuzi ya maendeleo katika tasnia hii.
Aidha,alisikitishwa na tabia ya wasanii kutokuwa katika vyama na badala yake kukaa pembeni na kutupa lawama au kukosoa mwenendo wa tasnia pasipokuzingatia kwamba wao wanapaswa kuwa sehemu ya mabadiliko na kupaza sauti zao wakiwa ndani ya mfumo.
“Tuanze kujiuliza sauti zetu zinasikika katika vyama vyetu? Kama hauko katika chama wewe ndiye unayekwamisha ujenzi wa mfumo. Wakati umefika tusiwe watu wa kulalamika bali kuleta mabadiliko ya kweli tukiwa katika umoja wetu” alihitimisha Materego.
Awali katika program ya wiki hii,Viongozi wa mashirikisho ya wasanii nchini walipata fursa ya kuwasilisha uzoefu wao kuhusu bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo iliyosomwa bungeni hivi karibuni.

Monday, August 22, 2011

ULEVI KUPINDUKIA WASABABISHA AJALI ENEO LA MAMA JOHN MBEYA

Askari wa usalama barabarani mkoani Mbeya akitoa kibao cha namba ya gari lililopata ajali maeneo ya Mama John jijini mbeya, ajali hiyo imetokea jana usiku baada ya dereva wa gari hilo aina ya Toyota Corola kuzidiwa kilevi na kukosa mwelekeo na kutumbukia katika dalaja.
Huwezi amini hii gari imeingiaje hapa kwakweli madereva kuweni makini barabarani pombe ni hatari ukiona umelewa acha kuendesha gari
Baadhi ya wananchi wakiangalia gari iliyotumbukia darajani Mama John jijini Mbeya

Sunday, August 21, 2011

UTAWALA WA GADDAFI UMEANGUKA!


Kila chenye mwanzo kina mwisho. Blogu hii iliandika siku chache zilizopita juu ya kuwepo kwa taarifa za Ki-Intelijensia zilizotabainisha kuwa utawala wa Gaddafi ungeanguka ndani ya siku chache. Na imekuwa hivyo.

Usiku wa kuamkia leo wapiganaji waliokuwa wakipambana na vikosi vya Gadaffi hatimaye wameitwaa Tripoli.  Walibya kwa mamia  waaripotiwa kuingia mitaani kusheherekea ukombozi kutoka kwa utawala wa kidikteta na kikandamizaji. Watu wameonekana wakichoma moto picha za Gaddafi.

Inasemekana wana wa Gaddafi akiwamo Seif Islam ambaye alitarajiwa angemrithi baba yake wako sasa wamekamatwa na wapiganaji hao. Gaddafi mwenyewe hajulikani alipo. Uwanja wa ndege wa Libya kuna ndege mbili ambazo zinadhaniwa Gaddafi angezitumia kuondoka nchini akiwa na familia yake. Gaddafi angekimbilia wapi? Nchi za Zimbabwe na Angola zinatajwa kuwa zingeweza kuwa kimbilio la Gaddafi. Taarifa zaidi zitawajia kadri zitakavyopatikana.

MSONDO YATOA TUZO ya the Best Rhumba Group katika East Africa Music



BENDI ya mziki ya msondo ngoma imepata TUZO ya the Best Rhumba Group katika East Africa Music Awards mashindano yariyofanyika Nairobi Kenya na kukusanyika kwa bendi za Afrika Mashariki na bendi ya msondo kuibuka Kidedea katika mashindano hayo akisibitisha ushindi uho meneja wa bendi Saidi KIbiriti alipokuwa akiongea na Msemaji wa Bendi hiyo, Rajabu Mhamila , Super D

Alisema wameshinda tuzo hiyo na watahakikisha wanaionesha kwa mashabiki wa bendi hiyo ili kudhirisha kuwa bendi ipo ng'ang'ari popote duniani mana bendi imekamilika kila idara alisema Super D (pichani)

Bendi hiyo itanza mazoezi siku ya jumatatu kwa ajili ya kujiandaa na sikukuu ya Iddi inayotarajia kufanyika wiki ijayo ambapo wanaingia kambini kusuka vibao vipya ikiwemo na kuvifanyia kazi vile vya Zamani

Super D alisema bendi hiyo siku ya Iddi Mosi itapiga katika viwanja vya TTC Chang'ombe ambapo mashabiki watapata kuona tuzo hiyo ya Afrika Mashariki walioitwaa hivi karibuni na kupata fulsa ya kupiga nayo picha katika viwanja hivyo

Bendi hiyo inayotamba na vibao vyake vipya vya Suluu uliotungwa na Shabani Dede na Nadhili ya Mapenzi uliotungwa na Juma Katundu




Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
Mob;+255787 406930
+255774406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

Friday, August 19, 2011


AY FT LAMYIA & ROMEO - SPEAK WITH YA BODY VIDEO

SPEAK WITH YA BODY
May be he should be Named "Ruler and Conquerer"...well he ruled Bongo for a long time and ended up conquering it. Any Objection?Naah, ofcoz there isn't any otherwise what would our boy be doing in the U.S and not even visiting, Woooorkiing!!! This is an International hit from ours truly, A.y featuring Lamyia and Romeo. Lamyia from Checkmate and Romeo from No Limit Record Label in the United States. For some Unusual Reasons No Limit got hold of AY Cd and liked the Vibe and decide to invite him in North America for couple of records with legend baby superstar Romeo formerly known as LIL ROMEO. The beat was sick already and what A.y and the rest did is taking the music to the I.C.U. We All have to admit this track makes u wanna press play again, n again n again.

Check out new video by AY on 
http://ay.co.tz/  or http://youtu.be/eH4-qHrb4Ms
CREDITS:

Song: SPEAK WIT YA’ BODY
Artist: AY FEAT. ROMEO AND LAMYIA
Written By: Ambwene Yesayah, Lamyia and Romeo
Ay Vocals Recorded By: Pancho Latino At B’Hits Studio 2,Dar Es Salaam.
Produced By:RILEY FROM CHECKMATE
Mixed and Mastered By: RILEY FROM CHECKMATE

MANAGER- HEMDEE
VIDEO BY OUTLIERS
DIRECTORS-WILLIAM TIKKI & SHAI
 
Hope Ya’ll going to have fun.
Life’s Too Short…Make The most of it.
Kuna Taarifa Za Ki-Intelijensia; Gaddafi Kuikimbia Libya Siku Chache Zijazo

| Friday, August 19, 2011

Kwa mujibu wa taarifa za Kiintelijensia zilizoripotiwa na Televisheni  ya NBC ya Marekani. Kanali Muammar
Gaddafi anapanga kuikimbia Tripoli akiwa na familia yake. Huenda akakimbilia Tunisia. Hii inatokana na matukio ya hivi karibuni kwenye medani ya kijeshi ambapo Gaddafi ameupoteza mji muhimu ki mkakati . Ni mji wa Zawiyah unaonekana pichani chini ambao sasa unapepea bendera ya Libya ya kabla ya ujio wa Gaddafi. Kutoka Zawiyah, vikosi vinavyopambana na Gaddafi sasa vimebaki na Tripoli kama target. Kuanguka kwa Zawiyah kutoka mikononi mwa Gaddafi kunaweza kuchochea  maasi  zaidi ndani ya jeshi la Gaddafi na hata kuwatia moyo Walibya walioko Tripoli kuamka na kumpinga Gaddafi wazi wazi. Na tusubiri tuone.
TTCL YAINGIA MKTABA WA KUUZA VOCHA KWA MTANDAO NA KAMPUNI YA MAXCOM AFRICA

Mkurugenzi wa TTCL Said Amri Said kulia akibadilishana hati za mkataba na Ahmed Lussasi Mkurugenzi wa Maxcom Africa, mara baada ya kusaini makubaliano ya kufanya biashara ya kuuza vocha za kampuni hiyo kwa kutumia mtandao, katika hafla iliyofanyika leo asubuhi katika makao makuu ya TTCL.
TTCL imeingia mkataba na kampuni ya MAXCOM AFRICA uwakala wa kuuza voucher za internet na simu za kawaida kwa njia ya mtandao (Electronic Voucher Distribution).
Wanachofanya wao ni kuwapa mawakala (agents) wao katika maeneo mbalimbali vifaa vya electroniki (Electronic Devices) vyenye uwezo wa kutoa vocher hizo.
Kwa maana nyingine ni kwamba hawatauza kadi za kawaida za TTCL kama ilivyo sasa, isipokuwa namba za kuongezea muda wa maongezi/internet (airtime PINs) zitakazochapishwa (printed) kwenye karatasi kutoka katika machine hizo.
Maxcom Africa wana mpango wa kupeleka huduma hii katika mikoa yote ndani ya nchi. Hili linatuongeze sisi TTCL matumaini zaidi katika kuboresha huduma kwa wateja wetu.
Mkurugenzi wa TTCL Said Amri Said ametoa angalizo kuwa pamoja na kuingia mkataba huu, bado vituo vyetu vya huduma kwa wateja na mawakala wetu wataendelea kuuza kadi/voucher kama kawaida.
Technologia hii ya kuuza kadi kwa mtandao inawawezesha kutoa huduma katika vituo vingi zaidi na maeneo tofauti hivyo kuwafikia wateja wetu katika maeneo mengi zaidi.
TTCL inaahidi kutoa ushirikiano wa hali ya juu katika kufanikisha utoaji wa huduma hii ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wateja pale itakapohitajika.
TTCL inayofurahia zaidi kwani ushiriki wa Maxcom katika kusambaza vocha zao kunatuhakikishia huduma bora, ya uhakika na ya karibu kwa wateja wake kwa muda mwingi zaidi.
Uzoefu wao katika biashara hii unwapa faraja zaidi kwani kunawahakikishia upatikanaji wa vocha za TTCL kupitia mtandao wa kuaminika. Mkurugenzi huyo amewaomba wateja wao wavitumie vituo vya Maxcom na wawe huru kuuliza mahali pote waonapo alama ya Maxcom na TTCL.

Thursday, August 18, 2011

MSEKWA APIGILIWA MSUMARI NA WABUNGE



BUNGE limeendelea kuwa chungu kwa vigogo CCM, baada ya Makamu Mwenyekiti wake (Bara), Pius Msekwa (pichani) kutuhumiwa kwamba amekuwa akiingilia watendaji wa Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro (NCAA), kwa kujihusisha na utoaji wa ofa kwa wafanyabiashara wanaotaka kujenga hoteli za kitalii akitumia wadhifa wake wa Mwenyekiti wa Bodi ya hifadhi hiyo.

Mbali na Msekwa Kambi ya Upinzani Bungeni, jana pia ilihoji vigezo alivyotumia Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige kumteua Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM, Benno Malisa kuingia katika Kamati ya Kumshauri Waziri juu ya Sekta ya Vitalu vya Uwindaji.

Akiwasilisha maoni ya Kambi hiyo bungeni kuhusu bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2011/12, Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa alimtaja Msekwa kwamba ni mmoja wa wanaokwamisha maendeleo katika hifadhi ya Ngorongoro.

"Tuna ushahidi kuwa, Pius Msekwa ambaye ndiye Mwenyekiti wa Bodi hiyo, amegeuka kuwa mwenyekiti mtendaji anayefanya kazi ya kutoa ofa kwa wafanyabiashara wenye mahitaji ya kujenga hoteli za kitalii, huku akiwaelekeza maeneo hayo, kazi ambazo si zake,” alisema Mchungaji Msigwa.

Kutajwa kwa Msekwa na Benno, ni mwendelezo wa vigogo wa CCM kutajwa bungeni wakihusishwa na tuhuma mbalimbali baada ya juzi kambi hiyo ya upinzani kutaja orodha ya viongozi waandamizi wa zamani wa chama hicho na Serikali kwamba wamehodhi ardhi kubwa mkoani Morogoro.

Vigogo hao waliotajwa wakati wa Bajeti Kivuli ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka 2011/12 ni pamoja na Marais Wastaafu Benjamin Mkapa na Ali Hassan Mwinyi, Mawaziri Wakuu wastaafu, Frederick Sumaye na John Malecela, Katibu Mkuu mstaafu wa chama hicho, Philip Mangula na aliyekuwa Naibu wake, Tanzania Bara, Hassan Ngwilizi.

Waziri mwenye dhamana ya Ardhi, Profesa Anna Tibaijuka, akizungumzia madai ya viongozi hao kumiliki ardhi bila ya kuiendeleza alisema: “honeymoon is over" (fungate imekwisha).

Jana, Mchungaji Msigwa akifafanua tuhuma moja baada ya nyingine, aliliambia Bunge: “...Huu ni mgongano mkubwa sana wa kimaslahi na wenye madhara makubwa kwa hifadhi hii. Haiwezekani Mwenyekiti wa Bodi ya Ngorongoro, ambaye moja ya majukumu yake ni kukagua hali halisi ya hifadhi hiyo, ajiingize pia katika shughuli za utendaji tena zilizo nyeti kama hizo.”

Msemaji huyo wa upinzani mwenye dhamana ya maliasili na utalii, alisema Serikali inapaswa kuchukua hatua kali dhidi ya Msekwa kwa kukiuka mipaka ya majukumu yake na kwamba kambi ya upinzani ipo tayari kuipa ushirikiano kuhusiana na tuhuma hizo.

Kuhusu Malisa kuingizwa katika kamati hiyo ya kumshauri waziri juu ya sekta ya vitalu vya uwindaji, Mchungaji Msigwa alisema: “Kijana huyu hana vigezo vinavyotakiwa ikiwa ni pamoja na ujuzi na uzoefu kwenye masuala ya utawala unaohusiana na uwezeshaji wa kiuchumi.’’

Msigwa alisema kambi ya upinzani imeshtushwa na uteuzi wa Malisa pamoja na kada mwingine wa CCM, Daniel Nsanzungwako na kusisitiza kwamba hawana vigezo vinavyotakiwa.

Alisema Malisa, anafahamika kitaaluma kuwa ana elimu ya sheria lakini hana uzoefu wowote katika masuala ya utalii na mazingira zaidi ya kujihusisha tu na shughuli za UVCCM.

“Ni dhahiri waziri amekiuka Sheria ya Wanyamapori na vigezo vyake katika uteuzi huo. Kambi rasmi ya Upinzani inalitaka Bunge hili tukufu kupitia kamati yake husika, ichunguze sababu za Mheshimiwa Waziri wa Maliasili kukiuka sheria katika uteuzi huo ili kujua alifanya hivyo kwa maslahi ya nani.”

"Kwa kuwa uteuzi huo haukuwa wa wazi, haukufuata misingi ya utawala bora na ulikiuka vigezo vya kisheria, Kambi rasmi ya Upinzani, inataka kamati hiyo iliyoundwa na waziri ivunjwe yote mara moja na kuundwa nyingine."

Ufisadi wizarani
Kuhusu ufisadi wizarani, alisema kumekuwapo ufujaji wa rasilimali za umma unaofanywa kwa makusudi na baadhi ya watendaji wa umma, “kwa kisingizio cha udhaifu wa kimfumo.”

“Upembuzi wetu kuhusu ripoti na nyaraka za Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, umeonyesha mwaka wa fedha wa 2009/2010 pekee, wizara hii ilifanya ukiukwaji mkubwa wa Sheria na Kanuni za Fedha, wa jumla ya Sh9.2bilioni na kusababisha taifa lipate hasara ya moja kwa moja ya zaidi ya Sh1bilioni.”

Waziri kivuli huyo aliongeza: “Wizara hii kinyume kabisa na Sheria ya Misitu (CAP 323) na Kanuni za Misitu za mwaka 2007, ilipunguza tozo ya mrabaha wa mazao ya misitu tena bila kibali cha mamlaka husika ya misitu na kusababisha taifa lipate hasara ya Sh874.8 milioni.”

Alisema sehemu nyingine ni malipo ya posho ya samani kwa watumishi ambao hawakustahili wanaoishi kwenye nyumba zao binafsi, kinyume cha sheria na kwamba malipo hayo yalisababisha hasara ya Sh119.3 milioni, huku malipo ya mishahara ya watumishi hewa na wastaafu yakisababisha upotevu wa Sh10 milioni.

Msigwa alisema upo ulazima wa watumishi wote wa Wizara ya Maliasili na Utalii, waliohusika katika kukiuka sheria na kanuni za usimamizi wa fedha za umma na kulisababishia taifa hasara kuchukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria.

Ubadhirifu Tanapa
Kambi hiyo ya Upinzani ilisema ina taarifa za uhakika kuhusu matumizi makubwa ya fedha za umma yanayofanywa na Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) ikilinganishwa na fedha wanazokusanya.

“Kwa mwaka wa fedha 2008/2009, gharama za uendeshaji za Tanapa zilikuwa Sh66.0 bilioni wakati shirika lilikusanya kiasi cha Sh70.4 bilioni na katika kipindi hicho Tanapa ilitumia Sh3bilioni tu kwa ajili ya kusaidia jamii,” alisema Msigwa na kuongeza:

“Kwa hali hii, ni dhahiri kuwa mapato mengi ya Tanapa yanaishia kwenye kugharamia zaidi utawala wake kuliko kuingia serikalini na kusaidia jamii.”

Alisema lazima Serikali itekeleze jukumu lake la kuhakikisha inadhibiti matumizi makubwa yasiyo ya lazima ya fedha za umma yanayofanywa Tanapa.

Msigwa pia alizungumzia taarifa za amri ya Serikali kuitaka Tanapa kuhama katika jengo lake ili kupisha Mahakama ya Afrika.

“Ni vyema ikakumbukwa kuwa huko nyuma, Tanapa walijenga jengo lao la kitega uchumi (commercial wing) mkabala na makao makuu, ambalo Mahakama hiyo ya Afrika walipangishwa, lakini leo taarifa tulizonazo ni kwamba wamepewa jengo hilo kwa nguvu na Rais na Tanapa wametakiwa kutafuta sehemu nyingine ya kupanga kwa ajili ya ofisi,” alisema Msigwa.

Msigwa alisema taarifa hizo zinasikitisha kwani zinathibitisha utayari wa Serikai kuyapokonya mashirika ya hapa nchini mali zake kwa sababu tu ya kuzibeba taasisi za nje.

“Taarifa za Serikali kutaka kuipokonya Tanapa jengo lake, inadhihirisha kuwa Serikali yetu haijui inakokwenda, kwani jengo hilo halikujengwa kwa ajili ya Mahakama ya Afrika, bali, lilijengwa kwa ajili ya Tanapa kwa malengo ya Tanapa,” alisema.

JK ATINGA DODOMA APOKELEWA NA WAZIRI MKUU

WAZIRI MKUU AKIWA BUNGENI DODOMA

 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na  Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda  baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Dodoma Augost 18, 2011.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na Naibu Waziri wa Maendeleo  ya Mifugo na Uvuvi  na Mbunge wa  Kiteto, Benedict Ole- Nangoro  (katikati) na Mbunge wa Mpanda  Mjini, Said  Arfi kwenye viwanja vya Bunge Mjini  
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na Naibu Waziri wa Maendeleo  ya Mifugo na Uvuvi  na Mbunge wa  Kiteto, Benedict Ole- Nangoro  (katikati) na Mbunge wa Mpanda  Mjini, Said  Arfi kwenye viwanja vya Bunge Mjini  
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akijibu maswali ya wabunge, Bungeni Mjini Dodoma  Augost

MSECHU AKUMBUKIA ENZI

ladyjaydee

MACHACHE TOKA KWA PETER MSECHU

Msechu akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa sekondari ya Nia Njema akiwahamasisha umuhimu wa kuifahamu lugha ya kiingereza.
Msechu akiwa ofisini kwa mazungumzo na mkuu wa sekondari ya Nia Njema, Anthony Nyenshile.
Msechu akiwa na baadhi ya marafiki zake aliosoma nao shuleni hapo ambao walimsindikiza katika ziara hiyo.

Msechu akiwa na baadhi ya walimu wa NIa Njema High School



MMOJA kati ya washindi wa shindano la Tusker la Tusker All Stars 2011 Mtanzania Peter Msechu amewaasa wanafunzi nchini kutilia mkazo wa lugha ya Kiingereza kwani inasaidia katika kupata mafanikio.
Msechu amesema hayo leo jumatano wakati alipotembelea Shule ya Sekondari ya Nia Njema iliyopo mjini Bagamoyo ambayo aliwahi kusoma kidato cha kwanza hadi cha nne.
Alisema kufahamu lugha hiyo ni kitu muhimu kwani kumemsaidia kwa kiasi kikubwa kutwaa taji hilo ambalo litamuwezesha kufanya kazi na wasanii mbalimbali wakubwa duniani.
“Napenda niwaambie lugha ya kiingereza ni mkuhimu katika kusaka mafanikio ya kitu…mimi nilipokuwa nasoma hapa niliona kama mwalimu wangu ananionea baada ya kuniadhibu kutokana na kutoifahamu vema, lakini sasa nimeona hawakuwa wakikosea,”Alisema.
Aliongeza kuwa, tangu alipoanza mchakato wa kushiriki shindano hilo kwa mara ya kwanza alikutana na changamoto ya lugha hali iliyomfanya aombe msaada wa kufunzwa zaidi na walimu wake hali iliyomsaidia kuchanja mbuga.
“Asikwambie mtu kiingereza ndiyo kila kitu kwani bila hivyo ningeona aibu kujifunza na kuishia njiani…nawasihi wadogo zangu kuitilia mkazo lugha hii,”Aliongeza.
Aidha, Msechu aliwashuku walimu wa shule hiyo kwani ndiyo chachu ya mafanikio yake kutokana na shule hiyo kutilia mkazo lugha hiyo kama lugha kuu ya mawasiliano shuleni hapo.
Naye mkuu wa shule hiyo, Anthony Nyenshile alimpongeza msanii huyo kwa kukiendeleza kipaji chake sambamba na kujibidiisha hali ambayo imemfikisha hapo alipo.
“Kwa kweli kijana huyu alikuwa mchapakazi na anayependa sana sanaa…tunakupongeza kwa hatua uliyofikia hivyo tunakutakia kila lka heri katika harakati zako za kimuziki,”Alisema.
Msechu, pamoja na wenzake wawili Alfa wa Burundi na Davis wa Uganda walitwaa ushindi wa shindano hilo lililofikia tamati mwishoni mwa wiki iliyopita huko Nairobi, Kenya.
Kwa ushindi huo wasanii hao watapata fursa ya kupanda jukwaani na wasanii mbalimbali wakubwa toka nchini Marekani ambao wanatarajiwa kwenda nchini Kenya.

MAMBO YA MUSTAFA HASSANALI

 

MAMBO YA MUSTAFA HASSANALI






Mbunifu wa Kiafrika, Mustafa Hassanali nchini Botswana, Gaborone
Mbunifu Mustafa Hassanali,ndio alikua mtanzania pekee aliealikwa kuwakilisha nchi yake katika wiki ya kwanza ya Fashion Botswana , iliyofahamika kama Color in the desert fashion week.
Hafla hii,iliudhuliwa na wabunifu mbalimbali wa kimataifa na wenyeji.Baadhi ya wabunifu wa kiafrika walioudhulia walikua , Taibo Bacar (Mozambique), David Tlale,na Thula Sindi kutoka Afrika kusini, Moo Cow (Kenya), Joyse Nyasha Chimanye( Zimbabwe). Kauli mbiu ya Fashion week mwaka huu,ilikua "Kuongeza tija na maendeleo ya fani ya ubunifu wa mavazi na viwanda vya nguo Botswana "
Mustafa Hassanali alisema "Kutokana na uzoefu wangu,Botswana ni nchi yangu ya kumi na moja kiafrika na ya kumi na tatu kidunia kufanya maonesho ya ubunifu,Na nnajisikia faraja na kujivunia kuwa mmoja wa walioudhulia week ya kwanza ya fashion Botswana,na pia kuwa mmoja wa kuendeleza uhusiano mzuri kati ya Tanzania na Botswana kupitia Fashion "

Thursday, August 18, 2011 *STARS KUKIPIGA NA ALGERIA JIJINI MWANZA SEPTEMBA 3 Katibu Mkuu wa Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania, Angetile Osiah. Mechi ya mchujo ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN) zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon katika ya timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Algeria (Desert Warriors) itachezwa Septemba 3 mwaka huu jijini Mwanza. Awali tulipanga mechi hiyo ichezwe Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Lakini uamuzi wa kuihamishia Mwanza umefanyika baada ya jana kupata barua kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ikitufahamisha kuwa Uwanja wa Taifa hautatumika tena kwa sasa. Kwa mujibu wa Wizara, uwanja huo utakuwa katika matengenezo baada ya kuharibika wakati wa michuano ya Kombe la Kagame iliyofanyika mwanzoni mwa mwezi uliopita. YANGA, SIMBA NAZO KUATHIRIKA Uamuzi huo wa uwanja kufungwa kwa ajili ya matengenezo pia umeziathiri klabu za Yanga na Simba ambazo zilikuwa zimekubaliwa timu zao zitumie kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom ambayo inaanza kutimua vumbi Agosti 20 mwaka huu. Tayari leo (Agosti 18 mwaka huu) tumeziandikia rasmi klabu za Simba na Yanga kuzifahamisha kuhusu uamuzi huo wa Wizara, hivyo kuzitaka zitafute viwanja vingine kwa ajili ya mechi zao za ligi. Hatua hiyo ya uwanja kufungwa, itailazimisha TFF ifanye mabadiliko kwenye ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom kwa kuzingatia viwanja ambavyo klabu za Yanga na Simba zitakuwa zimeamua kuvitumia. Mabadiliko hayo pia yataziathiri timu za African Lyon, Azam, JKT Ruvu, Moro United na Villa Squad ambazo licha ya kutumia Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam, zilipanga mechi zao za nyumbani dhidi ya Simba na Yanga zichezwe Uwanja wa Taifa. Kwa sasa msimamo wa wamiliki wa Uwanja wa Azam ni Yanga na Simba kutoutumia kwa vile uwezo wake wa kuchukua watazamaji ni mdogo. Boniface Wambura, Ofisa Habari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imewekwa na : MUHIDIN SUFIANI Muda: Thursday, August 18, 2011 0 idadi ya maoni Links to this post *BASI LA SABCO LAPATA AJALI IRINGA Basi la kampuni ya Sabco linalofanya safari zake Mbeya-Dar, lililokuwa likitoka Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya, kuja jijini Dar es Salaam limepata ajali eneo la Tanangozi wilaya ya Iringa vijijini baada ya tairi la basi hilo kupasuka. Imeelezwa kuwa katika ajali hiyo abiria kadhaa wamejeruhiwa. Mmoja wa abiri aliyekuwa akisafiri na Basi hilo, akijaribu kutafuta mawasiliano ya simu ili kutoa taarifa kwa ndugu na jamaa baada ya ajali hiyo. imewekwa na : MUHIDIN SUFIANI Muda: Thursday, August 18, 2011 0 idadi ya maoni Links to this post *BARAZA LA MAWAZIRI LAIHENYESHA EWURA MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Haruna Masebu,amehenyeshwa kwa kuhojiwa kwa undani na Baraza la Mawaziri kuhusu kuyumbisha bei ya mafuta. Baraza hilo lilitaka kujua kwa nini mamlaka hiyo imekuwa ikiyumbisha nchi na wananchi kuhusu bei za mafuta. Kwa zaidi ya saa moja, Masebu na wasaidizi wake waliwekwa kiti moto kuhusu bei zilizotangazwa na Ewura mwishoni mwa wiki, ambazo zimepanda kwa asilimia sita kutoka zile zilizotangazwa awali. Habari za kuaminika kutoka kwenye mkutano wa Baraza la Mawaziri uliofanyika jana kwenye Ukumbi wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, mjini Dodoma zinasema kuwa waziri mmoja baada ya mwingine alimhoji Masebu na wasaidizi wake kuhusu mwenendo usioridhisha wa bei za mafuta nchini. Habari zinasema kuwa Masebu ambaye aliingia kwenye ukumbi huo akionesha kujiamini, alianza kupoteza mwelekeo kwa kadri maswali yalivyokuwa yakimiminika kutoka kwa mawaziri. Hatimaye siyo yeye mwenyewe ama yoyote kati ya wasaidizi wake ambaye alikuwa na majibu ya kutosheleza ama hata ya kuwashawishi mawaziri kuhusu hatua hizo za Ewura na kwa kadri kikao hicho kilivyoendelea, Masebu na wenzake walionekana kukosa hoja. Habari zinasema kuwa Masebu na wasaidizi wake walitakiwa kujielezea mbele ya Baraza la Mawaziri ili kuliwezesha Baraza hilo, chini ya Uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete, kujiridhisha na mwenendo mzima wa bei mafuta. Baraza hilo lilitaka ufafanuzi kuhusu bei za petroli, mafuta ya taa na dizeli, nishati ambazo ukosefu wake nusura uiingize nchi katika zahama kubwa wiki iliyopita. Moja ya maswali ya awali kutoka kwa Baraza la Mawaziri ilikuwa ni kwa nini Masebu na Ewura walitangaza kupanda tena kwa bei za mafuta siku chache baada ya kuzishusha kwa asilimia 9.17 kwa petroli, asilimia 8.31 kwa dizeli na asilimia 8.70 kwa bei ya mafuta ya taa. Hatua hiyo ya Ewura kupunguza bei ya mafuta ilikuwa inatekeleza uamuzi na maagizo ya Serikali yaliyotangazwa na Waziri wa Fedha, Mustafa Mkullo Juni 22, mwaka huu, bungeni wakati alipowasilisha Bajeti ya Serikali. Katika bajeti hiyo, Mkullo alisema kuwa Serikali iliamua kuondoa kodi na tozo kadhaa kwenye bei ya mafuta yanayoingizwa nchini kwa nia ya kupunguza bei ya bidhaa hizo ili kumpungumzia makali ya maisha mwananchi. Hatua hiyo ya Mkullo, pamoja na ile ya Ewura kupunguza bei za mafuta ziliungwa mkono na Bunge na wananchi kwa kiwango kikubwa ambao walikiri kuwa hatua hiyo ilithibitisha jinsi gani Serikali yao inavyowajali. Hatua ya Ewura kupunguza bei ya mafuta ilipingwa na kampuni karibu zote kubwa za kuingiza mafuta nchini ambazo zilianzisha mgomo kupinga hatua hiyo hasa BP, Engen, Oilcom na Camel Oil. Baada ya siku moja ya mgomo huo, kampuni zingine nchini zilianza tena kuuza mafuta, lakini kampuni hizo nne zilikataa kufungua vituo vyao kuuza mafuta. Agosti 9, mwaka huu, Ewura ilitoa amri ya Kimahakama (Compliance Order), kwa kampuni hizo nne kuanza mara moja kutoa huduma katika maghala yao na katika vituo vya rejareja vikiwemo vile vilivyoko chini ya miliki zao. Katika amri hiyo, kampuni hizo zilitakiwa kuacha mara moja kusababisha upungufu wa makusudi wa mafuta ya petroli katika soko la Tanzania na kujieleza katika saa 24 kwa nini wasichukuliwe hatua za kisheria kwa kukiuka matakwa ya Sheria ya Mafuta na Utaratibu wa Ewura. Siku iliyofuata, kampuni tatu zilianza kutoa huduma lakini BP (T) Ltd iliendelea kukaidi amri ya Ewura. Bodi ya Ewura katika kikao chake cha Agosti 12, ilichukua hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kutoa onyo kali kwa kampuni za Oilcom, Camel Oil na Engen, na kuisitishia BP leseni ya biashara ya jumla ya mafuta kwa miezi mitatu na kuamuru Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo na mwenyekiti wake wa bodi wafikishwe kortini. Lakini katika muda wa saa 48 tu, baada ya hatua hiyo ambayo iliungwa mkono na nchi nzima, Ewura ilibadilisha msimamo na mwelekeo wake na kutangaza kupandisha tena bei ya mafuta hayo ya petroli, dizeli na taa kwa asilimia tano. Hatua hiyo ya Ewura, ilisababisha hasira ya Serikali yenyewe, Bunge, wabunge na wananchi kwa jumla. “Ulichofanikiwa kufanya Masebu ni kuharibu kabisa mamlaka na madaraka ya Ewura. Hii ni taasisi ambayo ilikuwa imeanza kujijengea heshima kubwa kwa wananchi kwa kuchukua hatua mwafaka, na sasa mmevuruga kabisa heshima hiyo ya Ewura. “Kwa kuvuruga heshima ya taasisi hiyo mmezitia doa siasa za nchi yetu,” waziri mmoja alimwambia ana kwa ana Masebu katika mkutano huo. Masebu alijaribu kujitetea kwa kusema kuwa upandishaji huo wa bei ya mafuta uliofanywa na Ewura kwa mujibu wa Sheria na kwa mujibu wa makubaliano ya kuangalia upya bei kila baada ya wiki mbili kwa sababu mafuta huingizwa nchini kutoka Uarabuni kila baada ya wiki mbili. Lakini Masebu aliambiwa kuwa hakuna mafuta yoyote yaliyoingizwa nchini tangu mvutano ulipoanza kati ya Ewura na kampuni za mafuta baada ya tangazo la kupunguza bei ya mafuta la Agosti Mosi, mwaka huu. “Mheshimiwa Mwenyekiti ni mafuta yapi yameingia nchini kutoka Uarabuni katika wiki mbili zilizopita kwa sababu katika muda wote kwanza ulikuwepo mgomo wa kampuni za mafuta uliokolezwa zaidi na kampuni zile kubwa nne. “Katika kipindi hiki, hakuna mafuta yaliyoingia nchini kwa sababu mafuta yalikuwepo kwenye matangi ya maghala na hayakuuzwa. Sasa Mkurugenzi anatuambia mafuta haya mapya yametoka wapi?” Alihoji waziri mmoja na kuongeza; “Walichofanya Ewura ni kupandisha bei ya mafuta ambayo yalikuwa yamekwishafika nchini kabla ya mzozo kuanza mwanzoni mwa Agosti mwaka huu,” alisema waziri huyo. Masebu alipojaribu kujitetea kuwa kwa taratibu za Ewura ni lazima bei za mafuta zipitiwe upya kila baada ya wiki mbili, waziri mwingine aliingia kati na kumwuliza: “Mnapitia tu hata kama hakuna mafuta mapya yaliyoingizwa nchini kama ilivyotokea katika wiki mbili zilizopita? Mnafanya kazi kama mashine bila kutilia maanani hali halisi?” Alihoji. Waziri mwingine alionya kuwa vitendo vya Ewura katika wiki mbili zilizopita vililenga kuyumbisha nchi na kuipeleka pabaya bila sababu za msingi. “Inaelekea nyie Ewura mnahangaika zaidi kutetea maslahi ya wafanyabishara kuliko maslahi ya wananchi wetu,” alisema Waziri huyo. imewekwa na : MUHIDIN SUFIANI Muda: Thursday, August 18, 2011 0 idadi ya maoni Links to this post *WAREMBO WA VODACOM MISS TANZANIA WATEMBELEA HIFADHI YA TARANGIRE Warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2011, wakiwa katika hifadhi ya taifa ya Tarangire, mkoani Manyara jana walipokwenda kujionea wanyama na vivutio mbalimbali vya utalii katika hifadhi hiyo ya tano kwa ukubwa nchini. Warembo hao wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio vya utalii na kuhamasisha utalii wa ndani kwa watanzania. Katika hatua nyingine leo Miss Photogenic anataraji kutangwazwa na kujipatia tiketi ya kuingia katika nusu fainali ya shindano la Vodacom Miss Tanzania, ambapo Miss Photogenic atakuwa ni mrembo wa pili kuingia katika hatua hiyo ya 15 bora baada ya Top Model. Picha na Father Kidevu Blog Mshiriki wa Vodacom Miss Tanzania Zelulia Manoko, akizungumza kwa niaba ya wenzake baada ya kufika katika lango kuu la kuingilia hifadhi ya taifa ya Tarangire mkoani Manyara jana na kujionea wanyama wa aina mbalimbali. Warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2011, wakiingia katika lango Kuu la hifadhi ya taifa ya Tarangire mkoani Manyara jana walipofika kujionea wanyama na vivutio mbalimbali vya utalii katika hifadhi hiyo ambayo ni ya tano kwa ukubwa nchini. imewekwa na : MUHIDIN SUFIANI Muda: Thursday, August 18, 2011 0 idadi ya maoni Links to this post *SIMBA YAFUTA UTEJA YAIBAMIZA YANGA 2-0 MCHEZO WA NGAO YA HISANI Nahodha wa timu ya Simba, Juma Kaseja, akipokea na kuibusu Ngao ya Jamii, baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga, mchezo uliochezwa jana usiku kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo magoli yote yalipatikana kipindi cha kwanza huku goli la kwanza likifungwa na Kiungo wa timu hiyo, Haruna Moshi 'Boban' na la pili likiwekwa kimiani na Felix Sunzu kwa mkwaju wa penati baada ya Boban kuchezewa faulo eneo la hatari. Warembo wakibeba Ngao ya Jamii kupeleka jukwaani kwa ajili ya kukabidhi kwa timu mshindi Simba. Wachezaji wa Simba, wakimbeba mwenzao Patrick Mafisango na kumpongeza baada ya kutangazwa kuwa nyota wa mchezo huo, ambapo alikabidhiwa zawadi na Benki ya NMB. Mashabiki wa Yanga, wakishangilia huku wakiwa na picha yenye mchoro wa kuwakebehi watani wao wa Jadi Simba, kabla ya kuanza kwa mtanange huo. Mashabiki wa Simba, wakishangilia huku wakiburudika na miondoko ya Vuvuzela kabla ya kuanza kwa mtanange huo. Winga wa Yanga, Godfrey Taita (kushoto) akijipinda kupiga krosi huku akizuiwa na Patrick Mafisango, wakati wa mchezo huo. Mchezaji wa Yanga, Hamis Kiiza (kulia) akijaribu kumtoka beki wa Simba, Nasor Chollo, wakati wa mchezo huo. Kiiza aliingia kipindi cha pili na kufanya mambo makubwa huku akiwanyanyasa mabeki wa Simba akishirikiana na rashid Gumbo, ambapo walionekana kubadilisha kabisa sura ya mchezo huo. Haruna Niyonzima wa Yanga (kulia) akimtoka beki wa Simba Nasor Chollo. Mashabiki wa Simba wakishangilia baada ya timu yao kupata bao la kwanza. Beki wa Simba Victor Costa (kushoto) akimdhibiti, Keneth Asamoh wa Yanga. Haruna Niyonzima wa Yanga (kushoto) akiwatoka mabeki wa simba wakati wa mchezo huo. Mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete (kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa Simba, Victor Coster. Tegete, akienelea kumtesa Costa. Tegete, akijaribu kupenya katikati ya msitu wa mabeki wa Simba.... Boban, akitibiwa nje ya uwanja baada ya kuchezewa faulo iliyozaa penati, lakini katika CHUPA hii aliyoshika mkononi ni aina gani ya kinywaji anakunywa? Tazama kwa makini kisha nipe jibu, sijawahi ona maji yenye rangi hii bwana alaaah! Kipa wa Yanga Shaban Kado, akijaribu kuokoa mkwaju wa penati iliyopigwa na Felix Sunzu, ambayo hata hivyo ilitinga wavuni na kukataliwa na mwamuzi wa mchezo huo aliyeamuru kurudiwa kwa penati hiyo. Sunsu na Okwi, wakishangilia baada ya sunsu kufunga kwa penati. Mashabiki wa Simba wakiwa na furaha ya ushindi. Jerry Tegete, akiruka kupiga kichwa katikati ya mabeki wa Simba, lakini hata hivyo shuti hilo la kichwa lilipaa juu ya goli. Hamis Kiiza, akijipinda kupiga kichwa katikati ya msitu wa mabeki wa Simba. Furaha ya ushindi kwa mashabiki wa Simba. Hamis Kiiza wa Yanga (kulia) akichuana na beki wa Simba Nasor Chollo. Kiungo wa Yanga, Rashid Gumbo, akimfinya Amri Kiemba na kumtoka. Beki wa Simba, Nasor Chollo, akimdhibiti mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete. Boban akichanja mbuga (kulia) ni beki wa Yanga Shadrack Nsajigwa, akipiga hesabu za kumdhibiti. Hamis Kiiza akiomba dua kabla ya kuingia uwa


 

*BASI LA SABCO LAPATA AJALI IRINGA

 Basi la kampuni ya Sabco linalofanya safari zake Mbeya-Dar, lililokuwa likitoka Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya, kuja jijini Dar es Salaam limepata ajali eneo la Tanangozi wilaya ya Iringa vijijini baada ya tairi la basi hilo kupasuka. 
Imeelezwa kuwa katika ajali hiyo abiria kadhaa wamejeruhiwa.
Mmoja wa abiri aliyekuwa akisafiri na Basi hilo, akijaribu kutafuta mawasiliano ya simu ili kutoa taarifa kwa ndugu na jamaa baada ya ajali hiyo.

*BARAZA LA MAWAZIRI LAIHENYESHA EWURA


MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Haruna Masebu,amehenyeshwa kwa kuhojiwa kwa undani na Baraza la Mawaziri kuhusu kuyumbisha bei ya mafuta. 

Baraza hilo lilitaka kujua kwa nini mamlaka hiyo imekuwa ikiyumbisha nchi na wananchi kuhusu bei za mafuta. 

Kwa zaidi ya saa moja, Masebu na wasaidizi wake waliwekwa kiti moto kuhusu bei zilizotangazwa na Ewura mwishoni mwa wiki, ambazo zimepanda kwa asilimia sita kutoka zile zilizotangazwa awali. 

Habari za kuaminika kutoka kwenye mkutano wa Baraza la Mawaziri uliofanyika jana kwenye Ukumbi wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, mjini Dodoma zinasema kuwa waziri mmoja baada ya mwingine alimhoji Masebu na wasaidizi wake kuhusu mwenendo usioridhisha wa bei za mafuta nchini. 

Habari zinasema kuwa Masebu ambaye aliingia kwenye ukumbi huo akionesha kujiamini, alianza kupoteza mwelekeo kwa kadri maswali yalivyokuwa yakimiminika kutoka kwa mawaziri. 

Hatimaye siyo yeye mwenyewe ama yoyote kati ya wasaidizi wake ambaye alikuwa na majibu ya kutosheleza ama hata ya kuwashawishi mawaziri kuhusu hatua hizo za Ewura na kwa kadri kikao hicho kilivyoendelea, Masebu na wenzake walionekana kukosa hoja. 

Habari zinasema kuwa Masebu na wasaidizi wake walitakiwa kujielezea mbele ya Baraza la Mawaziri ili kuliwezesha Baraza hilo, chini ya Uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete, kujiridhisha na mwenendo mzima wa bei mafuta. 

Baraza hilo lilitaka ufafanuzi kuhusu bei za petroli, mafuta ya taa na dizeli, nishati ambazo ukosefu wake nusura uiingize nchi katika zahama kubwa wiki iliyopita. 

Moja ya maswali ya awali kutoka kwa Baraza la Mawaziri ilikuwa ni kwa nini Masebu na Ewura walitangaza kupanda tena kwa bei za mafuta siku chache baada ya kuzishusha kwa asilimia 9.17 kwa petroli, asilimia 8.31 kwa dizeli na asilimia 8.70 kwa bei ya mafuta ya taa. 

Hatua hiyo ya Ewura kupunguza bei ya mafuta ilikuwa inatekeleza uamuzi na maagizo ya Serikali yaliyotangazwa na Waziri wa Fedha, Mustafa Mkullo Juni 22, mwaka huu, bungeni wakati alipowasilisha Bajeti ya Serikali. 

Katika bajeti hiyo, Mkullo alisema kuwa Serikali iliamua kuondoa kodi na tozo kadhaa kwenye bei ya mafuta yanayoingizwa nchini kwa nia ya kupunguza bei ya bidhaa hizo ili kumpungumzia makali ya maisha mwananchi.

Hatua hiyo ya Mkullo, pamoja na ile ya Ewura kupunguza bei za mafuta ziliungwa mkono na Bunge na wananchi kwa kiwango kikubwa ambao walikiri kuwa hatua hiyo ilithibitisha jinsi gani Serikali yao inavyowajali. 

Hatua ya Ewura kupunguza bei ya mafuta ilipingwa na kampuni karibu zote kubwa za kuingiza mafuta nchini ambazo zilianzisha mgomo kupinga hatua hiyo hasa BP, Engen, Oilcom na Camel Oil. 

Baada ya siku moja ya mgomo huo, kampuni zingine nchini zilianza tena kuuza mafuta, lakini kampuni hizo nne zilikataa kufungua vituo vyao kuuza mafuta. 

Agosti 9, mwaka huu, Ewura ilitoa amri ya Kimahakama (Compliance Order), kwa kampuni hizo nne kuanza mara moja kutoa huduma katika maghala yao na katika vituo vya rejareja vikiwemo vile vilivyoko chini ya miliki zao. 

Katika amri hiyo, kampuni hizo zilitakiwa kuacha mara moja kusababisha upungufu wa makusudi wa mafuta ya petroli katika soko la Tanzania na kujieleza katika saa 24 kwa nini wasichukuliwe hatua za kisheria kwa kukiuka matakwa ya Sheria ya Mafuta na Utaratibu wa Ewura. 

Siku iliyofuata, kampuni tatu zilianza kutoa huduma lakini BP (T) Ltd iliendelea kukaidi amri ya Ewura. Bodi ya Ewura katika kikao chake cha Agosti 12, ilichukua hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kutoa onyo kali kwa kampuni za Oilcom, Camel Oil na Engen, na kuisitishia BP leseni ya biashara ya jumla ya mafuta kwa miezi mitatu na kuamuru Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo na mwenyekiti wake wa bodi wafikishwe kortini. 

Lakini katika muda wa saa 48 tu, baada ya hatua hiyo ambayo iliungwa mkono na nchi nzima, Ewura ilibadilisha msimamo na mwelekeo wake na kutangaza kupandisha tena bei ya mafuta hayo ya petroli, dizeli na taa kwa asilimia tano. Hatua hiyo ya Ewura, ilisababisha hasira ya Serikali yenyewe, Bunge, wabunge na wananchi kwa jumla. 

“Ulichofanikiwa kufanya Masebu ni kuharibu kabisa mamlaka na madaraka ya Ewura. Hii ni taasisi ambayo ilikuwa imeanza kujijengea heshima kubwa kwa wananchi kwa kuchukua hatua mwafaka, na sasa mmevuruga kabisa heshima hiyo ya Ewura. 

“Kwa kuvuruga heshima ya taasisi hiyo mmezitia doa siasa za nchi yetu,” waziri mmoja alimwambia ana kwa ana Masebu katika mkutano huo. 

Masebu alijaribu kujitetea kwa kusema kuwa upandishaji huo wa bei ya mafuta uliofanywa na Ewura kwa mujibu wa Sheria na kwa mujibu wa makubaliano ya kuangalia upya bei kila baada ya wiki mbili kwa sababu mafuta huingizwa nchini kutoka Uarabuni kila baada ya wiki mbili. 

Lakini Masebu aliambiwa kuwa hakuna mafuta yoyote yaliyoingizwa nchini tangu mvutano ulipoanza kati ya Ewura na kampuni za mafuta baada ya tangazo la kupunguza bei ya mafuta la Agosti Mosi, mwaka huu. 

“Mheshimiwa Mwenyekiti ni mafuta yapi yameingia nchini kutoka Uarabuni katika wiki mbili zilizopita kwa sababu katika muda wote kwanza ulikuwepo mgomo wa kampuni za mafuta uliokolezwa zaidi na kampuni zile kubwa nne. 

“Katika kipindi hiki, hakuna mafuta yaliyoingia nchini kwa sababu mafuta yalikuwepo kwenye matangi ya maghala na hayakuuzwa. Sasa Mkurugenzi anatuambia mafuta haya mapya yametoka wapi?” Alihoji waziri mmoja na kuongeza;

 “Walichofanya Ewura ni kupandisha bei ya mafuta ambayo yalikuwa yamekwishafika nchini kabla ya mzozo kuanza mwanzoni mwa Agosti mwaka huu,” alisema waziri huyo. Masebu alipojaribu kujitetea kuwa kwa taratibu za Ewura ni lazima bei za mafuta zipitiwe upya kila baada ya wiki mbili, waziri mwingine aliingia kati na kumwuliza: 

“Mnapitia tu hata kama hakuna mafuta mapya yaliyoingizwa nchini kama ilivyotokea katika wiki mbili zilizopita? Mnafanya kazi kama mashine bila kutilia maanani hali halisi?” Alihoji. Waziri mwingine alionya kuwa vitendo vya Ewura katika wiki mbili zilizopita vililenga kuyumbisha nchi na kuipeleka pabaya bila sababu za msingi. 

“Inaelekea nyie Ewura mnahangaika zaidi kutetea maslahi ya wafanyabishara kuliko maslahi ya wananchi wetu,” alisema Waziri huyo.

*WAREMBO WA VODACOM MISS TANZANIA WATEMBELEA HIFADHI YA TARANGIRE

 Warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2011, wakiwa katika hifadhi ya taifa ya Tarangire, mkoani Manyara jana walipokwenda kujionea wanyama na vivutio mbalimbali vya utalii katika hifadhi hiyo ya tano kwa ukubwa nchini. 
Warembo hao wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio vya utalii na kuhamasisha utalii wa ndani kwa watanzania. 
Katika hatua nyingine leo Miss Photogenic anataraji kutangwazwa na kujipatia tiketi ya kuingia katika nusu fainali ya shindano la Vodacom Miss Tanzania, ambapo Miss Photogenic atakuwa ni mrembo wa pili kuingia katika hatua hiyo ya 15 bora baada ya Top Model. Picha na Father Kidevu Blog
 Mshiriki wa Vodacom Miss Tanzania Zelulia Manoko, akizungumza kwa niaba ya wenzake baada ya kufika katika lango kuu la kuingilia hifadhi ya taifa ya Tarangire mkoani Manyara jana na kujionea wanyama wa aina mbalimbali.   
Warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2011, wakiingia katika lango Kuu la hifadhi ya taifa ya Tarangire mkoani Manyara jana walipofika kujionea wanyama na vivutio mbalimbali vya utalii katika hifadhi hiyo ambayo ni ya tano kwa ukubwa nchini. 

*SIMBA YAFUTA UTEJA YAIBAMIZA YANGA 2-0 MCHEZO WA NGAO YA HISANI

 Nahodha wa timu ya Simba, Juma Kaseja, akipokea na kuibusu Ngao ya Jamii, baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga, mchezo uliochezwa jana usiku kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo magoli yote yalipatikana kipindi cha kwanza huku goli la kwanza likifungwa na Kiungo wa timu hiyo, Haruna Moshi 'Boban' na la pili likiwekwa kimiani na Felix Sunzu kwa mkwaju wa penati baada ya Boban kuchezewa faulo eneo la hatari. 
 Warembo wakibeba Ngao ya Jamii kupeleka jukwaani kwa ajili ya kukabidhi kwa timu mshindi Simba.
 Wachezaji wa Simba, wakimbeba mwenzao Patrick Mafisango na kumpongeza baada ya kutangazwa kuwa nyota wa mchezo huo, ambapo alikabidhiwa zawadi na Benki ya NMB.
 Mashabiki wa Yanga, wakishangilia huku wakiwa na picha yenye mchoro wa kuwakebehi watani wao wa Jadi Simba, kabla ya kuanza kwa mtanange huo.
 Mashabiki wa Simba, wakishangilia huku wakiburudika na miondoko ya Vuvuzela kabla ya kuanza kwa mtanange huo.
 Winga wa Yanga, Godfrey Taita (kushoto) akijipinda kupiga krosi huku akizuiwa na Patrick Mafisango, wakati wa mchezo huo.
 Mchezaji wa Yanga, Hamis Kiiza (kulia) akijaribu kumtoka beki wa Simba, Nasor Chollo, wakati wa mchezo huo. Kiiza aliingia kipindi cha pili na kufanya mambo makubwa huku akiwanyanyasa mabeki wa Simba akishirikiana na rashid Gumbo, ambapo walionekana kubadilisha kabisa sura ya mchezo huo.
 Haruna Niyonzima wa Yanga (kulia) akimtoka beki wa Simba Nasor Chollo.
 Mashabiki wa Simba wakishangilia baada ya timu yao kupata bao la kwanza.
 Beki wa Simba Victor Costa (kushoto) akimdhibiti, Keneth Asamoh wa Yanga.
 Haruna Niyonzima wa Yanga (kushoto) akiwatoka mabeki wa simba wakati wa mchezo huo.
 Mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete (kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa Simba, Victor Coster.
 Tegete, akienelea kumtesa Costa.
 Tegete, akijaribu kupenya katikati ya msitu wa mabeki wa Simba....
 Boban, akitibiwa nje ya uwanja baada ya kuchezewa faulo iliyozaa penati, lakini katika CHUPA hii aliyoshika mkononi ni aina gani ya kinywaji anakunywa? Tazama kwa makini kisha nipe jibu, sijawahi ona maji yenye rangi hii bwana alaaah!
 Kipa wa Yanga Shaban Kado, akijaribu kuokoa mkwaju wa penati iliyopigwa na Felix Sunzu, ambayo hata hivyo ilitinga wavuni na kukataliwa na mwamuzi wa mchezo huo aliyeamuru kurudiwa kwa penati hiyo.
 Sunsu na Okwi, wakishangilia baada ya sunsu kufunga kwa penati.
 Mashabiki wa Simba wakiwa na furaha ya ushindi.
 Jerry Tegete, akiruka kupiga kichwa katikati ya mabeki wa Simba, lakini hata hivyo shuti hilo la kichwa lilipaa juu ya goli.
 Hamis Kiiza, akijipinda kupiga kichwa katikati ya msitu wa mabeki wa Simba.
 Furaha ya ushindi kwa mashabiki wa Simba.
 Hamis Kiiza wa Yanga (kulia) akichuana na beki wa Simba Nasor Chollo.
 Kiungo wa Yanga, Rashid Gumbo, akimfinya Amri Kiemba na kumtoka.
 Beki wa Simba, Nasor Chollo, akimdhibiti mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete.
 Boban akichanja mbuga (kulia) ni beki wa Yanga Shadrack Nsajigwa, akipiga hesabu za kumdhibiti.
 Hamis Kiiza akiomba dua kabla ya kuingia uwanjani na kuwanyanyasa mabeki wa Simba.
Wachezaji wa Simba wakishangilia. "Raha ya ushindi Bao"........baada ya mchezo huo kumalizika.