Sunday, May 13, 2012


HONGERA Taifa Queens kwa Ushindi mliouapata

Na Godlistern Shao

HIVI karibuni mashindano ya mchezo wa mpira wa pete kwa bara la Afrika  yamemalizika hapa nchini  mashindano ambayo yalzikutanisha takribani nchini nane na nchi ya Malawi ikatawazwa kuwa bingwa wa mashindano hayo ikufuatiwa na Tanzania.

Ushindi huo wa Tanzania kushika nafasi ya pili unadhidi kudhiirisha kuwa taifa letu limeweka vipaumble katika umuhimu wa michezo kwa jamii kwa kuenzi historia ya binadamu watanzania nao pia walikuwa wakishiriki katika michezo mbalimbali katika makabila yao.

kwani katika jamii yoyote ambayo imekamilika uwa inaungansishwa na mambo mengi moja wapo ni Michezo, michezo hii inasaidia wananchi kujenga kujiamini na kuwa utambulisho wa jamii fulani.

Kwa bahati mbaya kuna michezo ambayo aikupewa kipaumble katika taifa letu kiasi cha kutishia kupotea licha ya kuwa na masahbiki wengi na kukaa midomoni mwa watu kila siku.

Kwani katika taifa letu michezo ambayo imekuwa mdomoni mwa watu na inayoweza kugawa jinsia mbili tofauti za Me/Ke ni kati ya mchezo wa mpira wa miguu na Netbal.
    .

lakini baadae tukabahatika kuletewa Michezo mingine kutoka mataifa ya magharibi ,mchezo kama  ngumi, mpira wa meza, mpira wa mikono, mbio za baiskeli.

Mchezo wa netiboli ni moja kati ya michezo ilijichuklia umaharufu mkubwa hapa nchini kiasi cha kutwala kwenye michezo mingi ya mashule hapa nchini .

Mchezo huu ambao ulihasisiwa mnao mwaka 1890 nchini England na huchezwa kwa dakika 60 huku nchi za Autralia, New Zealand na England zikitawala kwa kucheza mchezo huo duniani.

Nchini Tanzania mchezo huo wa netiboli uliingia baada ya vita ya kwanza ya dunia wakati Tanzania ilipokuwa chini ya ukoloni wa mwingereza  na mchezo huo kupata umaarufu mkubwa nchini.

Mchezo huu ambao uliingia nchini kwa lengo la kujifurahisha tu hasa watu waliga kutoka kwa wageni makanisani na walimu wa seminari, lakini  baadaye ulianza kuchezwa kwenye shule za msingi na ndiyo maana katika kipindi cha nyuma karibu shule zote za msingi zilikuwa na viwanja vya mchezo wa netiboli.

Pia wachezaji wa timu mbalimbali za netiboli au wachezaji wa timu ya taifa walikuwa wakipatikana kuanzia katika ngazi za chini kabisa hapa nazungumzia kuanzia ngazi ya mashule hadi vyuoni.

Chama cha mchezo wa netiboli Tanzania CHANETA kiliweza kuhasisiwa mnamo mwaka  1966, ambapo mchezo huo ulipata umaarufu mkubwa sana kiasi cha kuwa na mvuto kwa kila mwanadada kutamani kuwa mchezaji mahiri wa netball .

Kipindi hicho ambacho kulikuwa na mashindano mengi ya mchezo huu nchini na kulikuwa na ligi yenye mvuto wa kipekee kwa mashabiki na wachezaji na timu zilikuwa zikishindana katika kiwango cha juu na kuwa na timu kali za netiboli kama Bandari, Posta, Bima na nyingine nyingizilizokuwa zikitamba kipindi hicho.

kuanzia miaka ya tisini  umaarufu wa mchezo wa netiboli nchini ulianza kupotea baada ya kufanyika ubinafsishaji wa mashirika ya umma na kupelekea timu nyingi za mashirika kufa na kupoteza hazina kubwa ya wachezaji wa mchezo huu. .

Hali hiyo ambayo ilikuja na uharibifu mkubwa wa miundo mbinu ya mchezo huo kutokana na kupoteza mvuto kiasi cha wadau kushindwa tena kujitokeza katika kuinua kiwango cha wachezaji chipukizi na hali ya ushindani kwenyeligi ikashuka.

 Hata hivyo hiyo aikuwa sumu ya kutosha kuumaliza mchezo huo kwani uliweza kufufuka tena na kushika kaasi ya ajabu  lakini ulikumbwa na  migogoro katika safu ya uongozi ya chama cha mchezo huo CHANETA.

hata migogoro hiyo amabyo aikuweza kudumu kwa muda mrefu ,ilipotea na bade kujitokeza wadau ambao walijitoa kusaidia mchezo huu kwa hari na mali ,hapa sitosita kumtaja ,Mama Anna Bayi,Anna Kibira ,Da Rose Mkisi na wengine wengi amabo walijifunga kibwebwe kuhakikisha kuwa mchezo huu unarudi katika hadhi yake .

Kwa kufanya hilo CHANETA wameweza kuwa wenyeji wa michuano ya kimataifa mara mbili mfululuzo ,kwa kuandaa michuano ya Afrika amabyo imemelizika hivi karibuni katika uwanja wa Taifa.

Mwishoni mwa mwaka Juzi na serikali ilimleta kocha wa kigeni kutoka Australia, Simone Macknnis kwa ajili ya kufundisha timu ya taifa ya mchezo wa netiboli, lakini aliifundisha kwa miezi michache na kuondoka kwa sababu hakuridhishwa na huduma alizokuwa akipewa.

Lakini hata hivyo mchezo wa netiboli nchini uliendelea kuchezwa na hivi karibuni tumeshuhudia wake wa viongozi wa ngazi za juu serikalini wakijitolea kwa hali na mali kuhamasisha wadau kusaidia timu iweze kuwafanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.

Nichukue nafasi hii kuwapongeza Mama Tunu Pinda,Salma Kikwete na Mama Asha Bilal kwa kuweza kuitia hamasa timu yetu na kuweza kushika nafasi ya pili katika mashindano haya makubwa ya kimataifa yaliyofanyika katika Ardhi yetu.

 Licha ya kukosekana kwa wadhamini wa kuendesha mashindano hayo, Chaneta kwa kushirikiana na wadau mbalimbali waliweza kuandaa mashindano hayo ambayo yamemalizika kwa uasalama kabisa bila ya wachezaji kuwa na malalamiko yoyote yale .
 

Na katika kuthibitisha hili timu yetu ya taifa ya Taifa Queens imeweza kutufuta machozi kwa kushika nafasi ya pli katika mashindano ya Afrika huku nafasi ya kwanza ikishikwa na malwai hivyo tunakila sababu ya kuwapongeza dada zetu.
 
Kwa mujibu wa viongozi wa Chaneta mashindano hayo ndio yanayotumika kupanga ni nafasi gani timu inatakiwa kukaa kwenye viwango vya kimataifa .

Chaneta ili weza kupata wachezaji kutoka katika timu za vilabu lakini bado kuna changamoto ya ushiriki mchache wa timu za mtaani kucheza mchezo huo kama ilivyokuwa zamani.

Kwani hata yale mashirika ya umma ambayo yalikuwa yakitoa timu hivi sasa hayana timu tena na badala yake zimebakia timu za majeshi na tasisi chache amabzo zimejifunga kibwebwe kuendeleza mchezo huu.

kwa ustadi huu na kusababisha kuwapo na timu za majeshi nyingi kama ,JKT Mbweni, Jeshi Stars, Hamambe Mbeya, Polisi Dsm, Polisi Arusha, Polisi Mwanza, Polisi Pwani, Tamisemi, Uhamiaji, Magereza, JKT Ruvu, Filbert Bayi na CMTU Dsm.

Timu za Jeshi ambazo kila mwaka zimekuwa mstali wa mbele katika kuonyesha umahiri wake mwaka huu ziliendelea kutoa wachezaji wa timu ya taifa na tumaini la kuwepo timu katika vitongoji vyetu kufutika.

Kwa hili sio la kuilaumu CHANETA,bali ni mfumo wa mitaala uliowekwa katika shule zetu za msingi hadi sekondari kwa kumkosesha motto kupata fursa ya kujifunza michezo .

Timu kama JKT Mbweni ambayo inaongozwa na mfungaji mahiri   Mwanaidi Hassan ambaye ameweza kuwa msaada mkubwa katika timu yetu ya taifa kutokana na umahiri wake wa kufunga magoli na kutumia vizuri mwili wake pindi anapokuwa uwanjani. 

 
Timu kama Filbert Bayi amabyo uwa inaundwa na wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari za Filbert Bayi bado aitoshi kuwa timu ya mtaani kuzalisha wachezaji watakaocheza timu ya taifa .

 Hivyo ni vema serikali ikaangalia utaraitibu mwingine wakuhakikisha kuwa mchezo huu unarudi katika nafasi yake kama ilivyokuw awali kwani kuna wachezaji wa kutosha mtaani ambao awajapata fursa.

mwishooo

No comments:

Post a Comment