GRAND MALT YAZINDUA TUZO ZA “EXCEL WITH GRAND MALT 2012”.
Kinywaji
maarufu cha Grand Malt leo kimezindua tuzo kwa wanafunzi wa elimu ya
juu zijulikanazo kama “Excel with Grand Malt”, huu ukiwa ni mwaka wa
pili kwa tuzo hizi kutolewa.
Akizungumzia
tuzo hizo, meneja wa kinywaji cha Grand Malt Bi. Consolata Adam
alisema; Excel with Grand Malt ni tuzo za aina yake ambazo zimelenga
kutambua na kuthamini mchango wanaoonesha wanafunzi katika fani
mbalimbali nje ya masomo ya darasani. Tunatambua kuwa kazi kubwa ya
mwanafunzi anapokuwa chuoni ni kuhudhuria vipindi vya darasani na kupata
elimu, bali tunapenda pia kuwatambua wale wachache ambao wanakwenda
mbali zaidi na kufanya mambo ya maendeleo katika mazingira yao ya chuo.
Tuzo
hizi zilianzishwa mwaka jana ambapo tuliweza kufika katika mikoa sita
na kufikia vyuo vipatavyo ishirini. Kwa mwaka huu mchakato utaanza mwezi
Aprili hadi June, na Mikoa itakayohusika ni pamoja na Dar es salaam,
Morogoro, Iringa, Dodoma, Kilimanjaro na Mwanza ambapo vyuo vipatavyo 21
vitashiriki. Kama ilivyokuwa mwaka jana, fani zitakazoshindanishwa ni
Ubunifu (Innovation), Michezo (sports), Utamaduni na burudani (Culture
& Entertainment) na Mazingira na Huduma za jamii (Environment &
social responsibilities). Kama ilivyo ada, washindi katika fani hizi
watajipatia zawadi mbalimbali toka Grand Malt ikiwa ni pamoja na pesa za
kununulia vitabu na vyeti vya ushindi.
Kwa
sasa natangaza rasmi kuwa tunzo hizi zimezinduliwa rasmi na mkoa wa
kwanza utakuwa ni Morogoro ambapo tunatarajia kufanya tamasha kubwa
kwenye viwanja vya chuo kikuu cha SUA siku ya jumamosi kisha jumapili
tutafanya tamasha la ufunguzi kwenye Viwanja vya chuo cha CBE mkoani
Dodoma na kutakuwa na burudani zitakazoongozwa na nguli wa Hip hop
nchini Joh Makini ,zawadi nyingi na zaidi kutakuwa na GrandMalt baridi
na hakutakuwa na kiingilio chochote. Alisema Bi. Consolata.
Akielezea
umuhimu wa Tuzo hizo, meneja masoko wa TBL Bw. Fimbo Butallah alisema;
Tunafurahi sana kuona vyuo vyote vilipokea tuzo hizi kwa furaha kubwa,
hii ni kwa sababu wanatambua umuhimu wake. Kupitia tuzo hizi ambazo
zitakuwa zikitolewa kila mwaka, Grand Malt inatoa changamoto kwa vijana
walio vyuoni kuona umuhimu wa kujituma na kufanya mambo mengi na makubwa
zaidi ya kufaulu mitihani ya darasani tu. Tunaomba viongozi wa serikali
za wanafunzi na viongozi wa vyuo kuendelea kutoa ushirikiano kama
walivyofanya mwaka jana ili kuleta ufanisi zaidi katika tuzo za mwaka
huu. Kama ilivyo kawaida, utaratibu utakuwa ule ule ambapo wanchuo
watapendekeza majina ya vijana wanaoamini kuwa wamefanya mambo makubwa
ndani ya vyuo vyao katika tasnia zilizotajwa hapo awali, kisha kufuatiwa
na kipindi cha kupiga kura ambapo washindi watapatikana. Alimaliza Bw.
Butallah
Kwa
upande wake meneja mahusiano na mawasiliano wa Tbl Bi Edith Mushi
Alisema GrandMalt kwa kuzingatia umuhimu wa juhudi za serikali katika
kuhamasisha jamii kutunza mazingira kwa kupanda miti mwaka huu Grand
Malt itafanya zoezi maalum kwenye kila chuo kwa kupanda miti imara
itakayosaidia kutunza na kuboresha mazingira ya vyuo hivyo ili kuandaa
mazingira bora ya kusomea ya wanafunzi wa sasa na wa vizazi vijavyo
ambapo mkoani Dodoma zoezi hilo litafanyika jumatatu May 07,2012 katika
vyuo vya UDOM na CBE tawi la Dodoma na Mkoani Morogoro zoezi hilo
litafanyika kwenye vyuo vya SUA na Mzumbe siku ya jumanne May 08,2012
asubuhi, kisho zoezi hilo litaendelea katika mikoa ya
Iringa,kilimanjaro,Mwanza na Dar Es Salaam.
No comments:
Post a Comment