Sunday, May 13, 2012


FID Q mama akupenda niwe mwanamuziki
Na Godlistern Shao
KITU chochote kile kinaweza kuchukuliwa kama kazi ya sanaa, ila inategemea mtazamo wa hadhira ukoje juu ya kitu au kazi husika. Kwa upande mwingine, historia  hasa za jamii au vikundi vya jamii vilivyokuwa na vinavyoendelea kukandamizwa kwa namna moja au nyingine  husema vingine.
Sanaa imekuwa ni mojawapo ya zana zinazotumiwa kufungua macho na fikra za watu kwenye jamii mbalimbali, katika vipindi tofauti. Mfano mzuri ni ndugu zetu wa Afrika Kusini. Wakati wa utawala wa kibaguzi , watu waliokuwa wanaangaliwa kama viongozi walikuwa hawaruhusiwi kukutana au kuongea na mtu zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. Lakini harakati zao hazikugota; waligeukia sanaa  wakatumia kazi za sanaa kuamsha watu.
Kwa hapa nyumbani, historia sio tofauti sana. Wazazi wetu waliokuwa kwenye harakati za kuusaka Uhuru walitumia mpaka ngonjera za mashuleni kuwasilisha sera za TANU, ASP na vyama vingine vya siasa.
Kizazi chetu, cha vijana wa sasa, kina changamoto zake. Na bahati nzuri Fid Q analitambua hilo. Yeye aliamua kutumia sanaa kuwaamsha vijana, tangu alipoingia kwenye Hip Hop takribani miaka 15 iliyopita.
Miaka nenda rudi, anaendelea kufanya anachodhani ni sahihi na inabidi kifanywe. Ametoka mbali.
Tulifanikiwa kulonga naye, na hakusita kuongelea jinsi alivyoanza, kazi zake kwa ujumla na mipango yake ya hapo baadae.
 “Fid Q dot com’ ni wimbo ambao ulinifungulia njia kwa roho safi na kunifanya nipewe heshima iliyoniendeleza mpaka hapa nilipo. Kabla ya ‘Fid Q dot com’ nilitoa ‘Huyu na Yule’ ambayo nilimshirikisha Mr. Paul na Squeezer, nitakuwa mchoyo wa fadhila kama nitasita kusema hii ilinitambulisha vyema kwenye medani ya muziki wetu.
Tofauti iliyopo kati ya ‘dot com’ na ‘Huyu na Yule’ ni kuwa, ‘dot com’ ilikuwa ni kama kitu kipya zaidi masikioni mwa watu, na kitu kipya mara zote husisimua! Ni wimbo ambao nitatumbuiza kwenye tamasha la kesho na kesho kutwa, na bado watu wakaruka nayo utadhani imetoka jana tu.
 Ngoma hii ilinipa, na bado inanipa, heshima kwa wapenzi wa muziki, hata emcees niliowakuta na mpaka waliofuatia ,Ni moja kati ya nyimbo chache ambazo zimebahatika kutochuja, na kama tukisema zinazeeka basi sio vibaya kama nikiifananisha na muwa. Namaanisha, itazeeka na utamu wake”.Alileza Fid Q

Analeza kuwa Siku zote wasanii chipukizi ’ huwaambia wasijaribu kuwa mimi, kwa sababu hata hapa nilipo sipo ninapohitaji kubakia. Na kinachonifanya niendelee kuwepo ni kile kiburi changu cha kutohofia kupitwa ilimradi muda usiniache.
“Na pia Paul Robeson ameshawahi kunena haya: “Sanaa kazi yake si kuonesha tu hali ya dunia ilivyo sasa tu; bali inavyopaswa kuwa na itakavyokuwa baadae.”
Sababu hiyo ya msingi imempelekea kuamini ya kwamba wanamuziki na wasanii wote kwa ujumla tuna jukumu la kuwa wajenzi wa  kesho njema kuliko hata wanaotutawala.
 Anaweka wazi kuwa  mama yake  hakupenda awe mwanamuziki. Na alipopata ruksa ya kutembelea studio alikutana na vikwazo ambavyo kila msanii anayefanya hip hop yenyewe lazima atakuwa ameshakutana navyo.
Vikwazo hivyo ni pamoja na kuambiwa apunguze ukali wa maneno au kufanya mashairi mepesi yasiyoumiza vichwa vya wasikilizaji’.
Kwa kweli, kwa kupitia vipingamizi hivi, vimfanya kujifunza uandishi fulani hivi. Yaani kwa mfano hata kama anakosoa jambo fulani, hatahakikisha linaruka kwa kasi ya kifaru aliyejeruiwa lakini linatua kiulaini kama sponji.
Ndio maana anaweza kutoka na ngoma inayoongelea matatizo na bado watu wakaiimba na kucheza wakiwa vilabuni na kwenye madisko mbalimbali.

Anasema kuwa moja ya vitu ambavyo vilimtia moyo aendelee kufanya mziki siku aliyosikia mama yake mzazi akisema anaipenda nyimbo yake ya  ‘Usinikubali Haraka’  na kumlazimu atenge masaa matatu ya kujiuliza alifikiria nini mpaka akaandika ule wimbo.Na pili, je ni kweli mama yangu kaliona hilo?
“ Unajua siku zote unapofanya kazi yenye malengo ya kuigusa dunia, huwa inafikia kipindi ile dunia nayo huwa inataka kukugusa wewe mhusika mkuu. Fid Q ni msanii kama wasanii wengine, hivyo na mimi huwa nakutana na mikasa mbalimbali katika maisha, lakini pale linapokuja suala la kutafuta mwenza wa kuishi naye kwenye raha na shida, ndipo huwa najikuta  nina kuwa mzito”
 Na kueleza kuwa watu wengi upenda  kuwa na tabia ya kuhukumu vitu kama tulivyo na sio kama vilivyo, hivyo basi amegundua hiyo tabia ipo kwenye mapenzi pia.
 Na kusema kuwa mtu upendwa kwa kile alichokuwa nacho na sio yeye kama yeye na hicho kinapelekea wapendanao wengi kuuziana kanyaboya. Na kunipa  msemo wa haraka haraka haina baraka, ili muda zaidi upate kutengwa kwa ajili ya kitu chenye manufaa.
Wimbo wake wa pili anaoupenda  ni Propaganda… wazo lilomjia baada ya kughairi kutoka na Darwin’s Naitmea  na alifurahishwa na jinsi alivyoweza kucheza karibu na mada ya kwanza kabisa.

Wa tatu ni Fei. “Ukiusikiliza vizuri utagundua upendo nilionao juu ya mwanangu, na pia historia fupi ya mahusiano yaliyopo kati yangu na baba yangu mzazi.”

Aliweka wazi Maslahi ndio kitu pekee kinachowaumiza watu wengi lakini  hipo siku watu watatambua nini wanatakiw akufanya katika muziki wa hippop hapa nchini .Miaka kumi ijayo hip hop ya Bongo itakuwa kubwa zaidi ya vile ilivyo hivi sasa, na ningependa ipewe kipaumbele zaidi kwa sababu ni hii hii hip hop ndio ina uwezo wa kupunguza au kuondoa ujinga kwa asilimia 50 au hata 70, kama wanafunzi walioko mashuleni wataendelea kulega kwenye masomo yao ya kila siku.

Fid Q ambaye ameonekana kuwa na taswira tofauti ya swala la msanii kuw anaalbamu na kueleza kuwa  albamu kwake  huwa naichukulia kama “audio book”… Yaani sio suala la kukusanya nyimbo  tu kupeleka kwa sokoni kwa mashabiki .
Na kusema kuwa hali hiyo inatokea mara nyingi sana ; unakuta mtu anatoka na albumu, ngoma ya kwanza inasema ‘Umeniacha’, ya pili ‘Sikutaki Tena’ ya tatu ‘Nataka Mpenzi’, ya nne ‘Unanichosha’. Halafu unakuta album labda inaitwa ‘Toba’.
 KitaaOLOJIA ni albamu mpya ya Fid Q ambayo imekusanya kuanzia album ya kwanza ambayo ni ‘Vina Mwanzo Kati na Mwisho’ na ya pili ambayo ni ‘Propaganda’, sasa Kitaa inakuja kukamilisha ule uprofesa wake wa chuo kikuu cha ghetto, kwa kuwaletea simulizi na mafunzo niliyokutana nayo mitaani… kwa kupitia mambo yaliyompata uzoefu katika maisha yake binafsi.
Alabamu ambayo anatarajia kuipakua Augosti 13 mwaka huu na kusema soko la bongo liko tayari kuipokea na lishakaa mkao wa kula kwa ajili ya albamu hiyo.
 Fid Q ambaye ameamua kuja kivingine katika kuhakikisha kuwa mziki wa Hippop unakuwa kwa kuandaa kipindi cha televisheni kitakacho tambulika kama FidStlye Friday .
Anaeleza kuwa FidStyle Friday itaanza kurushwa kwenye kituo kimoja cha televisheni hapa nyumbani. Na pia yupo katika maongezi na mmiliki mmoja wa televisheni ya kujitegemea iliyopo nchini Ujerumani kwa kuwa hata na wao wamevutiwa na yaliyomo kwenye FidStyle Friday.
Halikadhalika alitoa wito kwa mashabiki waendelee kusikiliza kwa umakini, wawe wadadisi ikiwezekana wafanye utafiti wa kila kauli itakayowavutia kwenye tungo za hip hop kwa sababu hiyo ndio njia pekee ya kuelewa uwezo wa msanii.
Anaeleza kuwa  yeye ni mshabiki namba moja wa Prof. J… Mpaka leo bado anajivunia kununua ile album yake ya ‘Machozi, Jasho na Damu Huwa haimchoshi kuisikiliza na ameridhika nayo kabisa. Kiasi kwamba huwa aoni kama jamaa anakosea kwa kunata kwenye midundo ya kapuka na mingineyo.
 Msanii mwingine ni Hasheem Dogo. Nikki Mbishi Mc pekee ambaye anamshangaza kila siku kwa ubunifu wake, na One The Incredible,kwa matumizi yaek ya Kiswahili fasaha na ule uandishi wake wa kugushi kushoto kisha anaelekea kulia mwingine ni  Stereo pamoja na Jay Mo.  


No comments:

Post a Comment