Wednesday, January 22, 2014

ZIARA YA KAMATI YA BUNGE YA MAENDELEO YA JAMII KWA WILAYA YA KINONDONI NA ILALA

 WAZIRI SOPHIA SIMBA AKISEMA NENO
 WAJUMBE WA KAMTI HIYO WAKITAFAKARI RIPOTI MBOVU YA WILAYA YA ILALA
 Capt Joh Komba akiwa na Mh Obama wakijaribu kutaza ripoti kwa kina
 afisa maendeleo ya jamii wa kinondoni akiwa silisha mada


 maua daftarai na mkurugenzi wa manispaa ya kindoni
 mh mkulo
 naibu meya kinondo songolo

Kinondoni; Vijana wa kiume wazito kujitokeza katika huduma za mikopo

Na Humphrey Shao, Dar es Salaam
HALMASHAURI ya manispaa ya Kinondoni  kama ilivyo kwa halmashauri zote nchini imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa jamii ikiwemo kuwezesha vikundi vya wanawake na vijana kwa kuwapatia mikopo yenye masharti nafuu kupitia mifuko ya mikopo mbalimbali tangu mwaka 1995.
 Moja ya mifuko hiyo ni mfuko wa kuendeleza wanawake uitwao WDF mfuko ambao unatekelezwa kwa kushirikiana na wizara maendeleo ya jamii jinsia na watoto.
Wizara ambayo inakopesha fedha kwa manispaa nayo inakopesha kwa vikundi vya uchumi vya wanawake na kusimamia marejesho yake ikiwa na lengo la kumkomboa mwanamke aliye katika hali ya chini.
Hivi karibuni nilipata fursa ya kutembelea manispaa ya kinondoni nikiwa na kamati ya bunge inayoshugulika na huduma za jamii ikiongozwa na mwanamama mahiri D.k Maua Daftari akiwa kama mwenyekiti.

Dk Maua ambaye alichukua fursa yakuwapongeza viongozi wa manispaa hiyo kwa kazi ngumu wanayofanya na kuwataka kuongeza mkazo zaidi katika harakati za kumkomboa mwanamke kupitia mikopo inayotolewa na wizara.
Mara baada ya kusema hayo Dk Maua alimtaka kaimu afisa maendeleo wa jamii wa Manispaa ya kinondoni Mwajuma Magwiza kueleza ni namna gani walivyoweza kutumia mikopo ya awali kutoka serikalini kuwafikia wanawake.
Magwiza anasema kuwa kupitia mfuko wa WDF Manispaa ya kindoni ilipokea jumla ya kiasi cha shilingi milioni 18,84000.00.
Anasema fedha hizo ambazo zilitumika katika kukopesha vikundfi mbalimbali lakini kufika mwaka 2003 kiasi cha fedha shilingi 4,531338.00 hakikuweza kurejeshwa kutokana na sababu mbalimbali za wakopaji wa mfuko wa WDF.
Magwiza anasema kuwa katika kuendeleza mfuko huu wamekutana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya bahadhi ya wakopaji kutopatikana katika maeneo waliyokuwepo.
“Wananchi wengi wanaimani kuwa fedha hizi zinazotolewa kwa mkopo kwa lengo la kumsaidia wanawake azitakiwi kurudishwa jambo linalochangia kwa kiasi kikubwa kukwamisha mradi kukua kwa kasi iliyopangwa’’anasema Magwiza.
Anasema kuwa pia waliweza kutoa mikopo kupitia mfuko wa maendeleo ya wanawake na vijana ulionzishwa na tume ya jiji la Dar es Salaam.
Anasema katika mfuko huo Manispaa ya kinondoni iliweza kupata shilingi 56,380,000 ambazo zilianza kukopeshwa kwa vikundi vya ujasiliamali vya wanawake na vijana.
“Kwa ujumla hali ya utoaji na urejeshwaji wa mikopo kwa kila mwaka tangu mikopo ilipoanza mwaka 1998 hadi mwaka 2006 na fedha ya yote ya mtaji iliyokopeshwa ni shilingi 387,124,000.00 amabpo kiasi cha marejesho kilikuwa ni 157,469,346.00 huku kiasi kilichobaki kwa wadaiwa kilikuwa 231,654,654.00”anasema Magwiza.
Anasema kuwa mbali ya matatizo yote hayo jumla ya wakazi wa kinondoni wanawake kwa vijana walionufaika ni 9,752 huku kati ya hao wanawake walikuwa 7,250.

Anasema katika kufanikisha huduma hiyo ya utoaji mikopo kwa wananchi wake manispaa hiyo imeweza kuingia ubia na benki ya wananchi ya Dar es Salaam hili wananchi waweze kupata mikopo kupitia benki hiyo.
Mbali na mikopo ubia huo ulikwenda sambamba na kutoa elimu ya ujasiliamali kwa wanawake na vikundi vya hili waweze kuwa na nidhamu na fedha wanazokopa.
Anasema katika kutekeleza hilo Halmashauri ya Manispaa ya kinondoni imefungua mfuko wa akaunti ya mikopo  ya wanawake na vijana katika benki ya wananchi wa Dar es Salaam.
Anasema katika mwaka wa fedha wa 2011 mpaka 2014 jumla ya kiasi cha fedha cha shilingi milioni 440,000,000 zilitengwa kwa ajili ya mikopo ya Vijana na wanawake.
Anasema licha ya manispaa kutenga kiasi hicho cha fedha bado kuna kundi la Vijana wa kiume ambalo limekuwa zito kujitokeza kuomba mikopo hiyo ambayo inatolewa kwa vikundi na mtu mmoja mmoja.
Anasema kupiti utaratibu huo wameweza kupata mafanikio makubwa ikiwemo na kuimarisha na kukuza uhusiano na ushirikiano kati ya serikali na wakazi wa Manispaa ya kinondoni.
Anaweka wazi kuwa Halmashauri inakusudia kuendelea kutenga fedha za mikopo katika bajeti zijazo hili kuongeza thamani ya mfuko huo ambao umeonekana kuwa tija kwa wakazi wa kinondoni hivyo kiasi cha shilingi milioni 500,000,000 kitaongezwa ifikapo mwaka wa fedha wa 2015/2016.
Hivyo aliwataka vijana kuongeza juhudi za kupeleka maombi hasa wakiwa katika vikundi hili waweze kupatiwa fedha hizo kwa haraka kuliko vile wanavyofikiri kukaa vijiweni.
Anaweka wazi kuwa hiyo ndio fursa pekee ya kumkomba kijana wasasa ambaye anatakiwa kujikita katika ujasiliamali.
mwisho



No comments:

Post a Comment