MKUTANO MKUU WA NGUMI ZA KULIPWA
Siku ya
terehe 1 ya mwezi wa pili katika ukumbi wa vijana hall kinondoni KUANZIA SAA
TATU NA NUSU ,kutakuwepo na mkutano mkubwa wa wanamasumbwi wote ulioitishwa na
orgnaizesheni ya ngumiza kulipwa Tanzania (TPBO) kwa lengo la kuwakutanisha mapromota
wote,mabondia na makocha wa ngumi wote
kwa lengo la kujadili ngumi za kulipwa zinapoelekewa,kujuana na kuelimishana
sheria za ngumi za kulipwa zinavyotumika
kinyume na sasa ,sheria nyingi zinafungiwa macho na kutumia uzoefu zaidi
kuendesha mgumi nchini. Mkutano huo
ulioitishwa na Rais wa TPBO bw Yasin
Abdallah akishirikiana na Ibrahim kamwe
na Mapromota wa ngumi chini ya ufadhili wa kitwe Traders unatarajiwa kuwa mkutano wa kwanza kuwakutanisha mapromota wote pamoja na mabondia wa ngumi za kulipwa wa hapa nchini ili kuboresha ngumi
na kuhamasisha wadhamini na makampuni wajitokeze kuudhamini mchezo huo ,ambao
ndio mchezo unaoliletea mataji na sifa Tanzania
katika medani za kimataifa lakini hauna udhamini wowote ,mpaka sasa ni mchezo ambao unaojiendesha wenyewe kwa nguvu za wadau wachache wachovu na mabondia wenyewe ambao uwezo wao ni mdogo
sana kukikidhi matakwa kamili ya mchezo wenyewekam ilivyo kwa wenzetu,ni mchezo
ambao una huduma nyingi zinazohitaji
nguvu ya wadhamini ili uendelee kuboreka
zaidi.
Akizungumza
na vyombo vya habari katibu wa ngumi za kulipwa nchini bw Ibrahim kamwe ,
amesema imewaalika viongozi wa baraza la michezo (BMT), na viongozi wengine
wote wa ngumi za kulipwa watakuwepo kama vile Emmanuel mlundwa,names kavishe, makaranga,Onesmo ngowi,kinyogoli, matumla, Zuwena kibena(mama zugo) na viongozi wadau
wa karibu na ngumi wamealikwa kuhudhulia mkutano huo ambao utafanyika Siku ya
terehe moja ya mwezi wa pili katika ukumbi wa vijana hall kinondoni. hivyo kamwe
alimaliza kwa kuwaomba kila anaejijua kuwa yeye ni bondia wa ngumi za kulipwa
na promota wangumi ahudhurie bila kukosa
mkutano huu muhimu sana kwa wamasumbwi ya nchi yetu.
No comments:
Post a Comment