Saturday, January 25, 2014

Dk. Ali Shein kumnadi mgombea Kiembesamaki

Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki-Januari 26.
Dk. Ali Mohamed Shein, atakuwa mgeni rasmi na kumandi Mahomoud Thabit Kombo


Dk. Ali Shein kumnadi mgombea Kiembesamaki
Na Andrew Chale, Zanzibar
MAKAMO Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi,  Dk. Ali Mohammed Shein  kesho Januari 26, anatrajiwa kumnadi mgombea wa Uwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki, Mahmoud Thabit Kombo, katika uchaguzi mdogo unaoendelea kwenye jimbo hilo.
Katika tarifa yake, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema kuwa, Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,  Dk Shein atakuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo wa nne wa hadhara kwenye kampeni hizo zinazoendelea.
Na kuongeza kuwa, Dk. Shein atawahutubia wananchi sambamba na kumnadi, Mgombea huyo wa nafasi ya uwakilishi, Mahmoud Thabit Kombo, anayewania nafasi hiyo kwenye jimbo hilo la Kiembesamaki.
Vuai aliwataka wananchi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi ilikusikiliza sera na ilani za chama hicho katika utekelezaji wake iliwakichague chama cha Mapinduzi kwa misingi imara ya kuwaletea maendeleo.
Aidha, kwa upande wake,  Mahmoud Thabit Kombo aliwaomba wananchi wa jimbo hilo, kumpigia kura hiyo Februari mbili, ili akawawakilishe kwenye Baraza la Wawakilishi.
“Nawaomba Wanakiembesamaki, kutumia fursa ya kipekee ya kunichagua ilikuweza kuwawakilisha kwenye BAraza, hakika  chama chetu ni sikivu na daima kipo na wananchi katika kuwatetea na kuwaletea maendeleo” alisema, Mahmoud.
Kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Kiembesamaki, zilianza Januari 21, ambapo zinatarajia kumalizika Februari Mosi, mwaka huu huku wananchi wakitarajia kupiga kura ya chaguzi huo, Februari mbili.
Mwisho



No comments:

Post a Comment