Mafanikio yanahitaji uvumilivu Mdau wa jirushe ni mwandishi wa habari kutoka New Habari Anapatikana kwa namba 0716 772231 ,Email -humphreyshao@ymail.com/shaohumphrey58@gmail.com kwa mahitaji yoyote ya kuhabarisha ,makala,matukio, picha za harusi na kuandaa event mbalimbali nitwangie
Saturday, January 25, 2014
Dk. Ali Shein kumnadi mgombea Kiembesamaki
Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki-Januari 26.
Dk. Ali Mohamed Shein, atakuwa mgeni rasmi na kumandi Mahomoud Thabit Kombo
Dk. Ali Shein kumnadi mgombea Kiembesamaki
Na Andrew Chale, Zanzibar
MAKAMO Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar
ambaye pia ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi,
Dk. Ali Mohammed Shein kesho Januari 26, anatrajiwa kumnadi mgombea wa Uwakilishi wa
jimbo la Kiembesamaki, Mahmoud Thabit Kombo, katika uchaguzi mdogo unaoendelea
kwenye jimbo hilo.
Katika tarifa yake, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai
Ali Vuai alisema kuwa, Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk Shein atakuwa mgeni rasmi kwenye mkutano
huo wa nne wa hadhara kwenye kampeni hizo zinazoendelea.
Na kuongeza kuwa, Dk. Shein atawahutubia wananchi sambamba
na kumnadi, Mgombea huyo wa nafasi ya uwakilishi, Mahmoud Thabit Kombo,
anayewania nafasi hiyo kwenye jimbo hilo la Kiembesamaki.
Vuai aliwataka wananchi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi
ilikusikiliza sera na ilani za chama hicho katika utekelezaji wake
iliwakichague chama cha Mapinduzi kwa misingi imara ya kuwaletea maendeleo.
Aidha, kwa upande wake,
Mahmoud Thabit Kombo aliwaomba wananchi wa jimbo hilo, kumpigia kura
hiyo Februari mbili, ili akawawakilishe kwenye Baraza la Wawakilishi.
“Nawaomba Wanakiembesamaki, kutumia fursa ya kipekee ya
kunichagua ilikuweza kuwawakilisha kwenye BAraza, hakika chama chetu ni sikivu na daima kipo na
wananchi katika kuwatetea na kuwaletea maendeleo” alisema, Mahmoud.
Kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Kiembesamaki, zilianza
Januari 21, ambapo zinatarajia kumalizika Februari Mosi, mwaka huu huku
wananchi wakitarajia kupiga kura ya chaguzi huo, Februari mbili.
Mwisho
Thursday, January 23, 2014
EU YAPIGA JEKI WATOTO TANZANIA
EU1: Mkuu wa Ushirikiano
kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya Tanzania Eric Beaume (kushoto)
akibadilishana hati ya makubaliano ya Mradi wa Kupambana na Ukatili kwa
Watoto na Mwakilishi wa UNICEF hapa nchini Jama Gulaid, kutoka kushoto
ni Mkurugenzi Mkazi wa Plan International Tanzania Jorgen Haldorsen,
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid na Mkurugenzi Mkazi
wa Save the Children International Tanzania Steve Thome wakishuhudia
makabidhiano ya hati hiyo jana jijini Dar es Salaam
U4: Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Seif Rashid (aliyeko mstari wa mbele katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa Mradi wa kutokomeza Ukatili kwa Watoto mara baada ya kutia saini msaada kutoka Umoja wa nchi za Ulaya jana jijini Dar es Salaam.
U4: Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Seif Rashid (aliyeko mstari wa mbele katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa Mradi wa kutokomeza Ukatili kwa Watoto mara baada ya kutia saini msaada kutoka Umoja wa nchi za Ulaya jana jijini Dar es Salaam.
MKUTANO MKUU WA NGUMI ZA KULIPWA
MKUTANO MKUU WA NGUMI ZA KULIPWA
Siku ya
terehe 1 ya mwezi wa pili katika ukumbi wa vijana hall kinondoni KUANZIA SAA
TATU NA NUSU ,kutakuwepo na mkutano mkubwa wa wanamasumbwi wote ulioitishwa na
orgnaizesheni ya ngumiza kulipwa Tanzania (TPBO) kwa lengo la kuwakutanisha mapromota
wote,mabondia na makocha wa ngumi wote
kwa lengo la kujadili ngumi za kulipwa zinapoelekewa,kujuana na kuelimishana
sheria za ngumi za kulipwa zinavyotumika
kinyume na sasa ,sheria nyingi zinafungiwa macho na kutumia uzoefu zaidi
kuendesha mgumi nchini. Mkutano huo
ulioitishwa na Rais wa TPBO bw Yasin
Abdallah akishirikiana na Ibrahim kamwe
na Mapromota wa ngumi chini ya ufadhili wa kitwe Traders unatarajiwa kuwa mkutano wa kwanza kuwakutanisha mapromota wote pamoja na mabondia wa ngumi za kulipwa wa hapa nchini ili kuboresha ngumi
na kuhamasisha wadhamini na makampuni wajitokeze kuudhamini mchezo huo ,ambao
ndio mchezo unaoliletea mataji na sifa Tanzania
katika medani za kimataifa lakini hauna udhamini wowote ,mpaka sasa ni mchezo ambao unaojiendesha wenyewe kwa nguvu za wadau wachache wachovu na mabondia wenyewe ambao uwezo wao ni mdogo
sana kukikidhi matakwa kamili ya mchezo wenyewekam ilivyo kwa wenzetu,ni mchezo
ambao una huduma nyingi zinazohitaji
nguvu ya wadhamini ili uendelee kuboreka
zaidi.
Akizungumza
na vyombo vya habari katibu wa ngumi za kulipwa nchini bw Ibrahim kamwe ,
amesema imewaalika viongozi wa baraza la michezo (BMT), na viongozi wengine
wote wa ngumi za kulipwa watakuwepo kama vile Emmanuel mlundwa,names kavishe, makaranga,Onesmo ngowi,kinyogoli, matumla, Zuwena kibena(mama zugo) na viongozi wadau
wa karibu na ngumi wamealikwa kuhudhulia mkutano huo ambao utafanyika Siku ya
terehe moja ya mwezi wa pili katika ukumbi wa vijana hall kinondoni. hivyo kamwe
alimaliza kwa kuwaomba kila anaejijua kuwa yeye ni bondia wa ngumi za kulipwa
na promota wangumi ahudhurie bila kukosa
mkutano huu muhimu sana kwa wamasumbwi ya nchi yetu.
mapambano ya ngumi mbagal azak hem
Bondia Abuu Abas kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Abdul Zugo wakati wa uhamasishaji wa tuzo za PSPF Boxing Award zilizofanyika katika viwanja vya Zakhem Mbagala Dar es salaam tuzo hizo zinafika tamati january 25 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Zugo alishinda kwa K,o ya raundi ya pili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Wednesday, January 22, 2014
ASUTWA USIKU KUCHWA KWA KUMNYANYASA MDOGO WAKE WA MIAKA SABA
USAJILI WA OKWI YANGA WAZUIWA
USAJILI WA OKWI YANGA WAZUIWA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesimamisha usajili wa mshambuliaji
Emmanuel Okwi kutoka Uganda katika timu ya Yanga wakati likisubiri
ufafanuzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF iliyokutana leo (Januari 22
mwaka huu) kupitia masuala mbalimbali, imesimamisha usajili huo baada ya
kubaini kuwa Okwi aliruhusiwa kuichezea SC Villa ya Uganda kwa kibali
maalumu kutoka FIFA.
Okwi
ambaye aliingia mgogoro na klabu yake ya Etoile du Sahel ya Tunisia
aliruhusiwa na FIFA kuchezea SC Villa kwa kibali maalumu (provisional
permit) cha miezi sita ili kulinda kiwango chake wakati suala lake dhidi
ya Etoile du Sahel likishughulikiwa na shirikisho hilo la kimataifa.
Katika
FIFA kuna kesi tatu kuhusiana na suala la mchezaji huyo. Wakati Okwi
ameishitaki klabu hiyo FIFA kwa kutomlipa mshahara, Etoile du Sahel
imemshitaki mchezaji huyo kwa utoro. Nayo Simba imeishitaki Etoile du
Sahel kwa kushindwa kuilipa ada ya mauzo ya mchezaji huyo ambayo ni dola
za Marekani 300,000.
Hivyo,
TFF imeiandikia FIFA kutaka kujua iwapo mchezaji huyo anaweza kucheza
Ligi nchini Tanzania wakati Etoile du Sahel ikiwa imefungua kesi katika
shirikisho hilo la kimataifa ikidai Okwi bado ni mchezaji wake.
MECHI ZA TANZANIA PRISONS YAZASOGEZWA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesogeza mbele mechi za raundi ya 14
na 15 zinazoihusu timu ya Tanzania Prisons zilizokuwa zichezwe Januari
25 na 29 mwaka huu.
Awali
Tanzania Prisons ilitakiwa kutafuta uwanja mwingine wa kuchezea mechi
hizo dhidi ya Ruvu Shooting na JKT Ruvu kutokana na Uwanja wa Kumbukumbu
ya Sokoine kutokuwa tayari kwa Ligi Kuu ya Vodacom wikiendi hii.
Mechi hizo sasa zitachezwa kati ya Februari 6 na 8 mwaka huu kwenye uwanja huo huo wa Kumbukumbu ya Sokoine.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
- 1 Attachment
sherehe za kumpongeza naibu waziri wa maliasili katika hoteli ya traventine
ZIARA YA KAMATI YA BUNGE YA MAENDELEO YA JAMII KWA WILAYA YA KINONDONI NA ILALA
WAZIRI SOPHIA SIMBA AKISEMA NENO
WAJUMBE WA KAMTI HIYO WAKITAFAKARI RIPOTI MBOVU YA WILAYA YA ILALA
Capt Joh Komba akiwa na Mh Obama wakijaribu kutaza ripoti kwa kina
afisa maendeleo ya jamii wa kinondoni akiwa silisha mada
maua daftarai na mkurugenzi wa manispaa ya kindoni
mh mkulo
naibu meya kinondo songolo
WAJUMBE WA KAMTI HIYO WAKITAFAKARI RIPOTI MBOVU YA WILAYA YA ILALA
Capt Joh Komba akiwa na Mh Obama wakijaribu kutaza ripoti kwa kina
afisa maendeleo ya jamii wa kinondoni akiwa silisha mada
maua daftarai na mkurugenzi wa manispaa ya kindoni
mh mkulo
naibu meya kinondo songolo
Kinondoni; Vijana
wa kiume wazito kujitokeza katika huduma za mikopo
Na Humphrey
Shao, Dar es Salaam
HALMASHAURI
ya manispaa ya Kinondoni kama ilivyo kwa
halmashauri zote nchini imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa jamii ikiwemo
kuwezesha vikundi vya wanawake na vijana kwa kuwapatia mikopo yenye masharti
nafuu kupitia mifuko ya mikopo mbalimbali tangu mwaka 1995.
Moja ya mifuko hiyo ni mfuko wa kuendeleza
wanawake uitwao WDF mfuko ambao unatekelezwa kwa kushirikiana na wizara
maendeleo ya jamii jinsia na watoto.
Wizara
ambayo inakopesha fedha kwa manispaa nayo inakopesha kwa vikundi vya uchumi vya
wanawake na kusimamia marejesho yake ikiwa na lengo la kumkomboa mwanamke aliye
katika hali ya chini.
Hivi
karibuni nilipata fursa ya kutembelea manispaa ya kinondoni nikiwa na kamati ya
bunge inayoshugulika na huduma za jamii ikiongozwa na mwanamama mahiri D.k Maua
Daftari akiwa kama mwenyekiti.
Dk Maua
ambaye alichukua fursa yakuwapongeza viongozi wa manispaa hiyo kwa kazi ngumu
wanayofanya na kuwataka kuongeza mkazo zaidi katika harakati za kumkomboa
mwanamke kupitia mikopo inayotolewa na wizara.
Mara baada
ya kusema hayo Dk Maua alimtaka kaimu afisa maendeleo wa jamii wa Manispaa ya
kinondoni Mwajuma Magwiza kueleza ni namna gani walivyoweza kutumia mikopo ya
awali kutoka serikalini kuwafikia wanawake.
Magwiza
anasema kuwa kupitia mfuko wa WDF Manispaa ya kindoni ilipokea jumla ya kiasi
cha shilingi milioni 18,84000.00.
Anasema
fedha hizo ambazo zilitumika katika kukopesha vikundfi mbalimbali lakini kufika
mwaka 2003 kiasi cha fedha shilingi 4,531338.00 hakikuweza kurejeshwa kutokana
na sababu mbalimbali za wakopaji wa mfuko wa WDF.
Magwiza
anasema kuwa katika kuendeleza mfuko huu wamekutana na changamoto mbalimbali
ikiwemo ya bahadhi ya wakopaji kutopatikana katika maeneo waliyokuwepo.
“Wananchi
wengi wanaimani kuwa fedha hizi zinazotolewa kwa mkopo kwa lengo la kumsaidia
wanawake azitakiwi kurudishwa jambo linalochangia kwa kiasi kikubwa kukwamisha
mradi kukua kwa kasi iliyopangwa’’anasema Magwiza.
Anasema kuwa
pia waliweza kutoa mikopo kupitia mfuko wa maendeleo ya wanawake na vijana
ulionzishwa na tume ya jiji la Dar es Salaam.
Anasema
katika mfuko huo Manispaa ya kinondoni iliweza kupata shilingi 56,380,000
ambazo zilianza kukopeshwa kwa vikundi vya ujasiliamali vya wanawake na vijana.
“Kwa ujumla
hali ya utoaji na urejeshwaji wa mikopo kwa kila mwaka tangu mikopo ilipoanza
mwaka 1998 hadi mwaka 2006 na fedha ya yote ya mtaji iliyokopeshwa ni shilingi
387,124,000.00 amabpo kiasi cha marejesho kilikuwa ni 157,469,346.00 huku kiasi
kilichobaki kwa wadaiwa kilikuwa 231,654,654.00”anasema Magwiza.
Anasema kuwa
mbali ya matatizo yote hayo jumla ya wakazi wa kinondoni wanawake kwa vijana walionufaika
ni 9,752 huku kati ya hao wanawake walikuwa 7,250.
Anasema katika
kufanikisha huduma hiyo ya utoaji mikopo kwa wananchi wake manispaa hiyo
imeweza kuingia ubia na benki ya wananchi ya Dar es Salaam hili wananchi waweze
kupata mikopo kupitia benki hiyo.
Mbali na
mikopo ubia huo ulikwenda sambamba na kutoa elimu ya ujasiliamali kwa wanawake
na vikundi vya hili waweze kuwa na nidhamu na fedha wanazokopa.
Anasema
katika kutekeleza hilo Halmashauri ya Manispaa ya kinondoni imefungua mfuko wa
akaunti ya mikopo ya wanawake na vijana
katika benki ya wananchi wa Dar es Salaam.
Anasema
katika mwaka wa fedha wa 2011 mpaka 2014 jumla ya kiasi cha fedha cha shilingi milioni
440,000,000 zilitengwa kwa ajili ya mikopo ya Vijana na wanawake.
Anasema
licha ya manispaa kutenga kiasi hicho cha fedha bado kuna kundi la Vijana wa
kiume ambalo limekuwa zito kujitokeza kuomba mikopo hiyo ambayo inatolewa kwa
vikundi na mtu mmoja mmoja.
Anasema kupiti
utaratibu huo wameweza kupata mafanikio makubwa ikiwemo na kuimarisha na kukuza
uhusiano na ushirikiano kati ya serikali na wakazi wa Manispaa ya kinondoni.
Anaweka wazi
kuwa Halmashauri inakusudia kuendelea kutenga fedha za mikopo katika bajeti
zijazo hili kuongeza thamani ya mfuko huo ambao umeonekana kuwa tija kwa wakazi
wa kinondoni hivyo kiasi cha shilingi milioni 500,000,000 kitaongezwa ifikapo
mwaka wa fedha wa 2015/2016.
Hivyo
aliwataka vijana kuongeza juhudi za kupeleka maombi hasa wakiwa katika vikundi
hili waweze kupatiwa fedha hizo kwa haraka kuliko vile wanavyofikiri kukaa
vijiweni.
Anaweka wazi
kuwa hiyo ndio fursa pekee ya kumkomba kijana wasasa ambaye anatakiwa kujikita
katika ujasiliamali.
mwisho
Subscribe to:
Posts (Atom)