Wizara zatakiwa kutengea bajeti michezo
Na Humphey Shao
MKUU wa Wilaya ya Tanga, Ibrahim Msengi amezitaka Wizara mbalimbali hapa nchini kuhakikisha zinatenga bajeti za michezo mahali pa kazi ili kuweza kuwapa fuksa wafanyakazi wao kushiriki kikamilifu katika mashindano ikiwemo ya Mei Mosi.
Msengi alitoa kauli hiyo juzi wakati wa ufunguzi Mashindano ya Mei Mosi ambapo alisema suala la bajeti ni ubunifu na umakini hivyo wanapotaka kufanya mambo yao lazima wajipange.
Aidha aliwataka washiriki katika mashindano hayo kucheza kwa nidhamu na kufuata taratibu ambazo zimewekwa ikiwemo na kuzitaka timu shiriki kutumia wachezaji ambao ni wafanyakazi na kuacha kutumia wachezaji ambao ni mamluki.
Mashindano hayo yanashirikisha timu 18 ambazo ni Wizara ya Afya,Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Ulinzi,Wizara ya Mambo ya Ndani,Wizara ya fedha, Wizara ya Habari,Wizara ya Maliasili,Ras Tanga, TTPL, Mamlaka ya Ustawishaji Dodoma CDA,Wizara ya Uhamiaji, Mapinduzi, Polisi Tanzania na AICC.
Mkuu wa wilaya huyo alisema michezo licha ya kujenga afya na undugu pia huchangia kutangaza kampuni, bishara au taasisi ambapo Mashindano hayo msimu huu yamebeba kauli mbiu isemayo "Michezo ni hali ya mfanyakazi bajeti isiwe kisingizio cha kushiriki".
Ufunguzi wa Mashindano hayo ulianza kwa maandamano ambayo yalianzia nje ya uwanja wa kuingia uwanjani kwa washiriki kujipanga mistari ambapo waliingia uwanjani na kujipanga kwa ajili ya kumsikiliza mgeni rasmi.
Katika mechi ya ufunguzi,timu ya Ras Tanga iliweza kukubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Wizara ya Ulinzi mechi iliyochezwa kwenye dimba la Mkwakwani mjini Tanga.
Mabao ya Wizara ya Ulinzi yalifungwa na Ndauka John katika dakika ya 35 na 89 ambapo mchezaji huo alipachika mabao yote mawili kwenye mechi hiyo.
Kwenye mechi ya Kuvuta kamba kwa upande wa Wanaume,Wizara ya Afya na Wizara ya Mambo ya Ndani zilishindwa kutambiana baada ya kulazimishana sare ya kufungana seti 1-1.
Kwa upande wa Wanawake, Timu ya Uchukuzi ilikukubali kichapo baada ya kufungwa seti 1-0 na Wizara ya Mambo ya Ndani.
XXXXX
Diamond awataka chipukizi wachangamkie shoo ya Kili mikoani
Dar es Salaam
MWIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya, Nassibu Abdulmalick, maarufu kwa jina ‘Diamond’ amewataka wasanii wachanga kuchangamkia nafasi ya ziara ya tuzo za Kili mikoani.
Ziara hiyo inatarajiwa kuanza Aprili 22 kwa usaili wa wasanii wachanga, kwa ajili ya kufanya shoo ya pamoja na washindi wa tuzo za Kili, Aprili 28, mjini Dodoma.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Diamond alisema kwa wasanii wachanga, kufanya shoo ni nzuri, maana wanajiweka karibu na wadau.
Alisema ni jukumu la kila msanii mchanga kujiandaa vyema kwa ajili ya shoo hiyo, hasa watakapofanikiwa kujumuishwa ndani yake.
“Nawaomba kila msanii mchanga atakayepata nafasi ya kufanya shoo hiyo ya ziara ya tuzo za Kili, kufanya vyema zaidi ili wajitangaze.
“Naamini Mungu atawasaidia, maana wengi wao tumetoka huko na tulikubali usumbufu wa kila aina, tukiwa na lengo moja la kufanikiwa kama walivyokuwa wasanii wengine Tanzania,” alisema.
Washindi wa tuzo za Kili wameandaliwa ziara hiyo kwa ajili ya kuwashukuru mashabiki wao, ikiandaliwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), chini ya bia yake ya Kilimanjaro.
XXXXX
Na Humphrey shao
MSANII wa muziki wa bongo fleva nayetamba na nyimbo ya hakunaga Ismail Sadiki almaharufu kama Sumalee amefikishwa katika mahakama ya kindoni kw autapeli wa shilingi milioni moja na laki nane ambazo ni malipo ya wali ya shoo ya geita na kahama kutoka kampuni ya Island Promotion.
Akizungumza na gazeti hili meneja matukio wa kampuni hiyo Amer Kombo alieleza kuwa uongozi wa kampuni ya island promotion ulimlipa Sumalee kiasi cha shilingi shilingi milioni moja na laki nane taslimu kama malipo ya awali kwa jaili ya kufanya shoo katika miji ya Kahama siku ya jumamosi tarehe 7april 2012 geita siku ya jumapili ya pasaka tarehe 8 april 2012 na mwanza siku ya jumatatu ya pasaka pamoja na kukatiwa tiketi ya kwenda na kurudi katika shoo hiyo .
Komboa alieleza kuwa Sumalee alipigiwa simu na mkurugenzi wa kampuni ya Island Promotion siku ya jumapili ya tarehe 1 april 2012 kwa ajili ya kupewa taharifa ya kukabidhiw atiketi za sfari siku ya jumatatu tarehe 2april 2012 na msani huyoa likubali lakini baada ya hapo akupokea tena simu .
Alieleza kuwa mara baada ya kuona hivyo mkurugenzi wa masoko wa kampuni hiyo aliamua kushikisha wadau wengine wa muziki waweze kumpigia simu na alikubali kukutana na event manger wa island na kukubaliana kuwa atasafiri kwenye maonyesho hayo laikini sumalee akutokea kahama wala geita na kusababisha usumbufu mkubwa kwenye ziara hiyo.
Alieleza kuwa kampuni ya island inawaomba radi mashabiki wake wa muziki wa kizazi kipya wa maeneo ya kahama ,Geita na Mwanza na uongozi mzima wa Villa Park .
Pia laisema kuwa iwe fundisho kwa msanii Sumalee na wasanii wengine wenye Tabia kama zake hivyo usma athitajika kulipa gharama za shoo alizolipwa pamoja na hasara na usumbufu aliouletea kampuni ya island na gharama za kesi zitakuw aju yake .
Ends
No comments:
Post a Comment