MAKAMU wa pili wa rais wa Zanzibar Baloz Seif Ali Idd anatayajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano wa kujadili changamoto mbalimbali zinazo husu sekta ya maji.
Mkutano huo wa siku nne utahudhuliwa na viongozi kutoka nchi mbalimbali za Afrika pamoja na wenyeji Tanzania katika hoteli ya Kunduchi Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali maji Silvester Matemu alisema katika mkutano huo mada 30 zitawasilishwa ikiwa ni pamoja na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi.
Alisema kutokana na ongezeko la binadamu sekta ya maji ni rasilimali muhimu kutokana na kuwa na mahitaji mengi hivyo ni lazima kuwe na uelewa ili kunusuru vyanzo vya maji visiharibiwe.
“Tunategemea wageni 40 kutoka nchi za Afrika na mada nyingi zitatoka hapa nchini lengo letu ni kufikia malengo ya milenia ya kuwa na huduma bora ya maji kwa kuvitumia vizuri vyanzo vya maji vilivyopo,”alisema Matemu.
Naye Mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya mpango wa maji katika nchi za Afrika Profesa James Ngana alisema mkutano huo utasaidia kujenga uelewa kwa wataalamu wa masuala ya maji, kutambua sera za maji pamoja na kutatua changamoto zilizopo.
No comments:
Post a Comment