Wednesday, February 20, 2013



Umuhimu wa kutunza Kumbukumbu Tunapoelekea urasimishaji
NA HUMPHREY SHAO

MARA zote tasnia ya sanaa na wasanii wenyewe wamekuwa watu wa kutoa lawama serikalini bila kustadi nini wanatakiwa kufanya hili kuweza kufikia weredi kama ilivyo kwa wasanii wengine wa kimataifa.

Hali hiyo imeelezwa na  mkurugenzi wa utafiti na na mafufunzo kutoka BASATA Godfrey  Lebejo wakati kutoa muadhara katika jukwaa la sanaa linalo andaliwa na BASATA kwa kushirikiana na CAJA uunaofanyika kila jumatatu katika ukumbi wa BASATA juu ya umuhimu wa wasanii kutuinza kumbukumbu tunapoelekea urasimishaji.

Lebejo anaanza kwa kutaja nini kinachotakiwa kumfanya msanii aweze kufanya utafiti wa kazi zake.

Dhana hasa ya tafiti ni kutakiwa kujiuliza maswali ama kuuliza maswali watu wengine kama wanavyofanya wachezaji mpira huku kukiwa na lengo moja la kupata jibu lilo sahii katika kufanikisha kazi yako ya sanaa.

Anataja kuwa chamsingi kinachotakiwa katika kufanya tafiti hili kuweza kupata habari ya kweli kwa ajili ya kuziba pengo lililopo katika tasnia husika, hivyo kusisitiza kuwa kama kuna tafiti inafanyika alafu aishuki chini kwa walengwa hiyo aina maana katika maendeleo ya Tanzania.

“ kama kuna la msingi wasanii wanatakiwa kufanya ni hili hapa la kujiuliza maswali haya (1) Nifanyeje kazi yangu (2) Nani mlaji wa kazi yangu (3) wapi ntauza kazi yangu (4) Soko likoje” alisema Lebejo.

Anawasilisha kuwa tafiti zinatoa hali halisi ya kazi za sanaa na sanaa kwa ujumla kujua ikoje na kutoa majibu nini kifanyike hili matatizo yaweze kuondoka.

Aliongeza kuwa kama msanii lazima ajiulize matatizo  gani yanayo ikabili sanaa na kwa kipindi chote ambacho  msanii yupo sokoni na kama anataka kuingiza kazi sokoni.

Katika urasimishaji wa kazi za sanaa Lebejo alisema kuwa serikali imeamua kurasimisha kazi kwa kuanzia kwenye muziki na filamu kufuatia kuwepo kwa tafiti juu ya hali halisi ya faida za kazi hizi katika kukuza pato la Taifa.

“kwa miaka mingi serikali imeshindwa kutambua jinsi gani sanaa zilivyocghangia katika pato la taifa licha ya kuwepo vyombo mbalimbali vya kusimamia kazi za sanaa hapa nchini” alisema Lebejo.

Alisema kuwa hali hiyo imetokana na serikali kutoingiza urasimu wa kazi za sanaa kuwa rasmi na kupuzia    mchango wake na kutotilia manani.

Alitaja sanaa kama za uchoraji na uchongaji zimekuwa zikingizia taifa fedha nyingi za kigeni kuliko sanaa nyingine huku ufumaji na upikaji wa nguo kama batiki zikifuatia kutokana na wageni wengi wanaofika hapa nchini kupenda bidhaa hizo lakini kiasi chote hicho utambiwa nimapato ya utalii na kusahau umuhimu wa sanaa.

Anatanabaisha kuwa hali hiyo ilitokana na sera ya utamaduni kutotamka sanaa kama kazi kama zilivyo kazi nyingine na kupelekea michango yao kuto onekana.

Mara baada ya kuwepo kwa mkanganyiko na malalamiko mengi kutoka kwa wasanii hapa nchini ilipelekea serikali kufanya tafiti kupitia mtafiti kutoka Chuo kikuu Yehova nisi na kutanabaisha kuwa sanaa inalipa hali iliyopelekea serikali kurasimisha kazi hizo kuanzia julai mwaka huu.

Lebejo alieleza kuwa serikali imeamua kutatua matatizo yaliyopo katika sekta ya sanaa kupita urasimishaji hivyo kutokana na matokeo ya matatizo yaliyopo katika sanaa.

“licha ya kuwepo kwa urasimishaji wa kazi za sanaa lakini bado kuna jambo gumu sana linalo onekana kwa wasanii wengi wa Tanzania kuwa ni wagumu kutunza kumbukumbu za kazi zao na matokeo ya kazi hizo hali iliyosababisha kuwepo na mgogoro mkubwa juu ya swala zima la haki miliki” alisema Lebejo.

Alitaja kuwa waimbaji wengi watanzania wamekuwa wakitumia haki miliki za watu na za mataifa mengine katika nyimbo zao hivyo taifa litakapoingia katika mchakato wa urasimishaji wa kazi hakuna nyimbo ya mtu yenye midundo itakayopigwa hapa nchini.

Alitaja mfano kuwa nyimbo nyingi za muziki wa injili zimeelemea katika midundo ya Afrika kusini na mingine Makhirikhiri na kusahau kuwa hiyo ni haki ya watu na utamaduni wao hivyo sheria itawataka kutumia midundo za makabila ya watanzania.

  Alisema kuwa midundo na maanzari za nje ya nchi kubanwa hali hiyo itawafanya wasanii wa kitanzania na waandaaji wanaochipua kama uyoga kuwa wabunifu.

Hilo litakwenda sambamba na wasanii wenyewe kujitambua kwa kuweza kuandaa taharifa zao binafsi ‘cv’ hili kufanya kutambulika kirahisi na watu wakimataifa.

Hali hiyo ilikwenda sambamba na wachangiaji mbalimbali kutoa maoni yao juu ya mada hiyo katika kufikia malengo ya kimataifa kwa wasanii wa ndani.

Sacha Emanuel ni mwandishi wa script na katibu wa shirikisho la wandishi wa Muswada ‘script’ wilaya ya ilala alishangazwa na mashirikisho kuwa mstari wa nyuma katika kutoa elimu nakupokea mafunzo yanayotolewa na basata kuwafikishia wasanii.

“shida ipo sana hapa nchini kwani wandishi wa miswada na waongozaji ambao mara zote wamekuwa watu wa kukopi vitu kutoka nje ya nchi kutokana na kuwa wavivu wa kufanya tafiti” alisema Sacha.

Nae Amisa Sambwe alitaka wasanii kujiuliza na kujisomea hili kujua ni tafiti gani wanatakiwa kufanya na kwa wakati gani zifanyike.

No comments:

Post a Comment