Wednesday, February 20, 2013


NA HUMPHREY SHAO

JINA la Isike Samweli  sio jina geni kwa wale wapenzi tunaofatilia kwa karibu sana filamu za hapa nchini na hata kung’amua ni msani gani anafanya vizuri licha ya kutokuwa na jina kubwa katika tasnia hii ya filamu.

Hivi karibuni nilipata nafasi ya kutembelea maeneo ya kariakoo kumuona rafiki yangu mwenye asili ya kihindi nayefahamika kwa jina la Purteshi kwa wale wadau wa filamu wanamjua mtu huyu ndipo nilipopata fursa ya kumuona kijana huyu katika ofisi hizo bila kung’amua ni nani.

Sekunde chache baadae anawasili msanii wa filamu mwingine Lucknes Mokiwa ambaye ni rafiki yangu wa karibu na kunitambulisha kuwa huyu ndio Isike, mtayarishjai mdogo kulikoi wote hapa Tanzania  nilishtuka kwani yupo tofauti na jinsi jina lake nilivyokuwa nikilisoma katika filamu mbalimbali.

Kama ilivyozoeleka hapa nchini ni vigumukuamini kijana mdogo wa miaka 19 kuwa mtayarishaji wa filamu nyingi ambazo hata hao wasanii maharufu awajafikia.
 
Isike ambaye alizaliwa Septemba mwaka 1993 na kupata elimu ya msingi katika shule ya msingi Magomeni na badae aliweza kucahaguliwa kujiunga na sekondari ya goba ambayo wilaya kinondoni.

Anaeleza kuwa hapo awali aliweza kujiusiha na utangazaji wa vipindi vya watoto lakini alipokuwa darasa la saba aliweza kushawishika moja kwa moja kujiunga na sanaa ya uigizaji.




“kama kuna mtu mwenye bahati ni mimi kwani niliweza kuingia kwenye sanaa kwa mguu wa kulia katika kikundi cha shirikisho na mara baada ya miezi sita niliweza kuchaguliwa kucheza igizo la ukumu ya tunu ambalo liliweza kunitambulisha huku kampuni ya kwanza kufanya nao kazi ilikuwa ni Benchmark” Alisema Isike.

 Alinieleza akiwa na umri wa miaka 16  aliweza kuandaa filamu yake hapo akiwa na  kuwa kama mtayarishaji wa kwanza mtoto hapa nchini.

Akiwa kidato cha kwanza Filamu hiyo ilikwenda kwa jina la ‘2 sister’ iliweza kuwashirikisha wasanii kama Masinde, penina na Hidaya Njaidi kisha kufuatiwa na filamu iliyokwenda kwa jina la ‘Missed Call’ ambayo iliwashirikisha Hashimu Kambi ,Tekla Mjata, Komando Yoso.

Mara baada ya kufanikiwa kuuza filamu hizo huku akitumia njia ya kusambaza mwenyewe  aliweza kupata mafanikio makubwa ambayo kamwe hato ya sahau maisha ni mwake.

“kama nilivyo kueleza mimi nilifiwa na wazazi wangu wote wawili nikiwa darasa la nne hivyo fedha hizo ziliwezesha kuanza kujitegemea kwa kupanga chumba changu mwenyewe na kuanza kujilipia ada yangu ya shule na kuacha kukaa kwa mjomba yangu ambaye alikuwa akinilea kwani mtazamo wake na wangu ulikuwa tofauti katika sanaa” alisema Isike.


Anaeleza kipato hicho kilimfanya aweze kuisadia familia yake pia na muda mchache baadae mwaka 2010 aliweza kupata mkataba na kampuni ya KAPIKO na kutenegenza filamu iliyokwenda kwa jina la ‘Love in School’.

Filamu hii ambayo aliweza kumshirikisha Flora Mvungi, Hidaya Njaidi Iliweza kufanya vizuri sokoni kuliko alivyotegemea na kupewa nafasi ya kufanya filamu nyingine katika kampuni hiyo ya KAPIKO.

‘The impact’ ndo jina la filamu hiyo ambayo iliweza kumshirikisha mwanadada mahiri Jackline Wolper, Hashim Kambi, Flora Mvungi nayo iliweza kufanya vema na kumpeleka katika ukurasa mpya wa maisha ya sanaa.


Mara baada ya hapo aliweza kupumzika kwa kipindi cha miezi minne kwa ajili ya kujiandaa na mitihani ya kidato cha nne.

Anaeleza kuwa kila kazi inachangamoto yake hasa kwa wakati uliopo Isike anakiri kuwa aliweza kupata changamoto kubwa sana kwa kucheleweshewa malipo yake na


bahadhi ya kampuni alizoingia nazo mkataba kulingana na umri wake kiasi cha kumkera sana.

Lakini anakiri kuwa amekuwa akiheshimiwa na wasani wakubwa kuliko alivyotegemea hali inayomfanya ajisikiea bora zaidi kuliko hapo awali.


Anatanabaisha kuwa mara baada kumaliza mitihani yake ya kidato cha nne aliweza kujiunga na kampuni ya PAPAZI ambayo iliweza kusaini nae mkataba kisha kufanya nao kazi ambapo mwaka 2012 aliweza kutoka na filamu iliyokwenda kwa jina la ‘Ivan Tears’  na kufanya poa katika soko la filamu.

Alitaja filamu hiyo iliyiomshirikisha mwanadada shilole na baadae kutoa filamu ya ‘loose control’ ambayo ilimshirikisha Catty ,Tecla Mjata, Kojack na Steve wamaisha Plus hapo ndio ulikuwa mwisho wa kufanyakazi na PAPAZI.


Baadae alifanya filamu ya ‘Jealous’ iliyowashirikisha Mainda , Hashimu Kambi na Hidaya Njaidi ambayo iliweza kusambazwa na kampuni ya Pastor Muyamba.

Hata hivyo nyota ilizidi kung’ara kwa kijana huyu kufanikiwa kupata mkataba na Kampuni ya SPLASH kwa kuanza na filamu ya Oxygen ambayo mwanadada Elizabeth Michael ‘LULU’alicheza kama star.

Filamu hiyo iliyofanya vema sokoni ilimfanya kuongezewa muda wa kufanya filamu nyingine na kampuni hiyo ndipo mwezi janauri mwaka huu alitoka na filamu inayokwenda kwa jina la lonely.

Filamu ambayo amefanya na hemedi suleimani na wengine wengi kuwa gumzo katika mitaa yote ya jiji la Dar es Salaam.

Filamu nyingine ambazo ameweza kufanya ni kama ‘Sad Moment’ na kukiri kuwa nidhamu na uti ndio silaha ya mafanikio katika kazi zake za sanaa licha ya watu kuongea mengi na kusahau nini wanatakiwa kufanya.

“kiukweli nitakuwa mnafiki nisipo washukuru wasanii wenzangu kama Dotnata, Jackline Wolper, Lucknes Mokiwa na wengine wengi kwa kuwa msaada mkubwa kwangu kwani wao ndio wamekuwa watu wa kunitia moyo kila siku.

Anaeleza kuwa ndoto zake ni kufika mbali na kimataifa zaidi kwani tayari njia imepatikana na kikubwa anachojivunia ni umri wake ambao unamruhusu kufanya mambo makubwa.


No comments:

Post a Comment