Monday, February 20, 2012

NA MWANDISHI WETU Vijana nje ya shule Duniani kote na Tanzania ni miongoni mwa makundi yaliyo katika hatari zaidi ya kuambukizwa V.V.U.Sababu hasa zinatokana na mazingira wanayoishi.Lakini pia vijana wanatumia muda mwingi nje ya familia zao na kutokana na kutokuwa na mbinu na uelewa wa kutosha wa kupambana na changamoto za makuzi yao.Matokeo ya hayo yote ni maambukizi ya V.V.U. Kadili vijana wanavyoambukizwa V.V.U na kuwa wagonjwa ndivyo familia zao zinavyozidi kupoteza nguvu kazi. Suluhisho la haya yote ni kuwapa vijana stadi za kukabiliana na changamoto za kila siku katika makuzi yao.Kwa maneno mengine kuwapa vijana elimu ya stadi za maisha. TEYODEN Programu ya vijana nje ya shule ni mradi uliofahiliwa UNICEF na kutekelezwa na wilaya 19 nchini Tanzania, Temeke ikiwa ni moja kati ya wilaya hizo.Mwaka 2001 TEYODEN ilianzishwa kama matokeo ya programu hiyo. TEYODEN ni kifupi cha maneno Temeke Youth Development Network.TEYODEN ilisajiliwa chini ya Majina ya Makampuni mwaka 2003 na mwaka 2007 imesajiliwa katika Ofisi ya Makamo wa Raisi.Mtandao unaratibu kazi zake katika vituo 24 vya vijana Manispaa ya Temeke. Kwa sasa Manispaa ya Temeke imeongeza kata 6 na hivyo kufanya idadi ya kata 30.TEYODEN inapanga kutanua wigo wake wa kazi na kuzifikia kata zote 30 hali inayofanya TEYODEN kuwa ndio chombo pekee kinachoweza kuwafikia vijana moja kwa moja. Kufuataia swala hilo TEYODEN hivi iliweza kupata ufadhili kutoka kwa Foundation For Civil Society juu ya elimu kuhusu ushiriki na ushirikiswaji wa vijana katika ngazi za maamuzi na mambo muhimu katika jamiii . Kutokana na juhudi hizo, TEYODEN ilianzishwa ili kuunganisha nguvu za vijana katika kutatua matatizo yao , na pia kuboresha mifumo ya uongozi, utendaji pamoja na uhakika wa upatikanaji wa rasilimali ili kuufanya Mtandao uwe endelevu na uweze kuendeleza vijana wa Temeke. Katika ukuaji wa mtandao huu, changamoto mbalimbali zilmekuwa zikijitokeza katika usimamizi na uendeshaji wa mipango ya kila siku ndani ya TEYODEN hasa kwa sasa limejitokeza sana suala la uwajibikaji kwa vijana,ushiriki na ushirikishwaji wao katika shughuli za maendeleo na kijamii. Sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007 inatamka wazi katika kipengele 3.3 kuwa vijana wana wajibu maalum katika jamii kama raia wema katika taifa lenye demokrasia.Wanatakiwa kulinda maisha yao,kulinda katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania,kuheshimu maadili katika vipengele vyote vya maisha na kushiriki kwa uhuru na kikamilifu katika maisha ya kijamii,kiuchumi na kisiasa nchini.Hata hivyo hakuna utaratibu ulio wazi wa kuwaanda vijana kutimiza wajibu huu wa kijamii. Hivyo TEYODEN imefanya tafiti na kubaini kuwa kuna mahitaji ya kutekeleza mradi wa kuamsha ari ya uwajibikaji, ushiriki na ushiriki wa vijana katika shughuli za kijamii na kimaendeleo ili kutafsili sera ya vijana kwa vitendo . Hivi karibuni TEYODEN ilweza kupata kufanya tamasha la nje juu ya mada kuu kuhusu ushirikishwaji wa vijana ambapo waliweza kumualika Diwani wa kata ya azamio Khamisi mzuzuri kama mgeni rasmi. Mzuzuri anaeleza kuwa njia pekee ya kuwasaidia vijana katiaka wilaya hiyo ni kuwapa nafasi ya kushiriki katika vikao mbalimbali vya kata na hata baraza la madiwani . “vijana suala la uwajibikaji ushiriki na na ushirikiswaji wa vijana ni suala muhimu sana kwa kuwa vijana wanafanya kundi kubwa la watu katika manispaa ya Temeke na wastani wa asilimia 50 lakini kijana ndio nguvu kazi ya taifa ” alismea mzuzuri. Analeza kuwa kwa asilimaia 68 taifa linategemea nguvu kazi ya vijana na hata halamshauri ya Manispaa ya Temeke imekuwa ikitegemea kundi la vijana kama ndio nyenzo kuu ya uzalishaji lakini bado kunachangamoto ya vijana ya utopewa taharifa sahii kwa vijana . Aliweka wazi kuwa suala la ushirikishwaji wa vijana katika vikao na hata shughuli mbalimbali siyo la wilaya bali bali linajikita katika ngazi ya taifa hivyo kusema swla la ushirikishwaji sio la kiwilaya peke yake bali ni la kitaifa kwa ujumla . Hivyo kueleza kuwa kwa sasa serikali imeweza kufikia nusu ya malengo kwa kuwashirikisha vijana kwa kupitisha mkakati wa ushirikishwaji wa vijana kitaifa makkati huo ukipitishwa utatatumika kama muongozo wa ushiriki na ushirikishwaji wa vijana wa taifa nzima . Kwa upande wake Mweneyekiti wa matanadao wa vijana Hassan Pwemu alieleza kuwa vijana wa manispaa ya Temeke wanacahanagamoto kubwa ya kutoshirikishwa katika mabambo mbalimbali kuanzi anagazi ya mitaa mpka wilaya . Kuafuatia swla hilo vijana wengi wemukuwa na uhaba wa taharifa muhimu ambazo zinaweza kuwavusha kutoka ngazi moja hadi nyingine hili kuweza kupanua uelewa binafsi . Anaeeleza kuwa Upo ushahidi mwingi unaonyeshwa kwamba wasichana walizaa kabla ya umri na waliosahaulika na wapenzi na familia zao wanakumbwa na changamoto nyingi ambazo zinawaweka katika hatari za kuambukizwa V.V.U na kuishi katika mazingira magumu zaidi.Lakini hakuna programu zinazowaangalia kama kundi maalumu. Inakadiliwa kuwa katika Manispaa ya Temeke vijana ndio kundi kubwa wastani wa asilimia 60% hivi.Temeke ina kiwango kikubwa cha wasichana walio katika mazingira hatarishi na ambao hawaendi shule au wameishia darasa la saba.Kwa bahati mbaya V.V.U/UKIMWI.Programu nyingi za manispaa ya Temeke zinawalenga vijana walio ndani ya shule na walio nje ya shule kwa jumla. Kwa mujibu wa tafiti inayohusu kiwango cha hatari za maambukizi ya V.V.U kwa vijana walio chini ya miaka 20 ulifanya na Taasisi ya TAMASHA kwa kushirikiana na TEYODEN umeonyesha kuwa Wasichana walio katika umri wa balehe hawapo salama popote pala katika mji huu wa Dar es salaam na kwingineko .msichana anapofikisha umri wa kuvunja ungo tu anahesabika kama mtu mzima anayeweza kuchukua majukumu ya usichana . Hivyo katika umri mdogo wa miaka 12 tu wanaanza kupata misukosuko ya kutakwa kimapenzi kutoka kwa wauza duka wauza magenge watu wasokoni walimu madakatari makondakta wa magari na watembea kwa miguu . Changamoto hizi wanakumabana nazo pasipo na mbinu au kinga yoyote mwisho wa yote hukubali na kupata mimba mimba hizi wanzo zipata katika umri mdogo na maisha yao huanza kuapata mwelekeo mbaya na kuharibika kwa kuamua kuzaa aua kutoa mimba .


No comments:

Post a Comment