Mchezaji mpya wa Yanga Hassan Dilunga Kushoto akijaribu
kuchukua mpira wa kutoka kwa kiungo wa Timu hiyo Athuman Iddi(Chuji) Wakati wa
mazoezi ya timu hiyo, wachezaji hao ambao wamejiunga na kikosi hich jana mara
baada ya kumalizika kwa mashindano ya Chalenji. Picha na Humphrey Shao.
Beki
wa kulia wa klabu ya Yanga Rajabu zahiri akiwa chini anagangwa na Daktari wa
timu hiyo Nassoro Matyuza kushoto ni kiungo wa timu hiyo Nizar Khalfan . Picha
Na Humphrey Shao.
Na Humphrey
Shao, Dar es Salaam
KOCHA wa
klabu ya Yanga Ernie Brandts amesema ameridhishwa na kiwango kilichionyeshwa na
mchezaji wa timu hiyo wakati wa mazoezi na kumtaja ni mmoja kati ya wachezaji
wenye uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza.
Brandts
alisema hayo alipiokuwa akizungumza na Rai mara baada ya kumalizika kwa mazoezi
ya timu hiyo katika viwanja vya bora kijitonyama.
“Kila
mchezaji ananafasi ya kucheza kikosi cha kwanza lakini Yule anayeonyesha uwezo
na juhudi mara zote ndio ushikilia hiyo namba, hivyo kwa dilunga kwake ni
mwanzo mzuri kama nilivyomuaona tangu awali naamini ataleta mabadiliko makubwa”
alisema Brandts.
Alisema kuwa
kwa sasa timu yake iko vizuri na inajiandaa na mchezo wake wa kirafiki dhidi ya
timu ya Simba unaotambulika kw ajina la nani mtani jembe.
Aliongeza
kuwa kwa sasa ni mapema sana kuzungumzia mchezo huo kwani nasubiri wachezaji
wangu wote watimie ndio nitakuw ana kauli kwa ajili ya mchezo huo.
Mwisho
Na Humphrey
Shao, Dar es Salaam
Beki wa
kulia wa klabu ya Yanga Rajabu Zahir ameumia goti la kushoto wakati akiwa
mazoezini na timu hiyo nakupelekea kutolewa nje.
Kwa mujibu
wa taharifa ya daktari wa timu hiyo Nassoro Matyuza alisema kuwa maumivu hayo
sio makubwa sana hivyo anahitaji mapumziko ya siku moja kwa ajili ya kujiweka
sawa.
“Maimivu
yake sio makubwa hivyo nawatoa hofu wapenzi wa yanga kuwa muda mfupi tu atakuw
afiti hivyo tgemeeni kumona katika michezo inayokuja “ alisema matuzya .
Mbali na
huyo wachezaji wengine ambao walikaa nje kwa ajili ya mejeruhi ni Salum Telela
na Nadir Haroub ‘Canavaro’ ambao wao walikuwa nje ya uwanja.
Wachezaji
Kelvin Yondani,Emmanuel Okwi pamoja na Amisi Kiiza ambao bado awajaripoti
kikosini mpaka sasa.
Mshambuliaji wa klabu ya Yanga Said Bahanuzi akimpa mwili
kiungo wa timu hiyo Haruna Niyonzima wakati wa Mazoezi ya timu hiyo katika
viwanja vya bora kijitonyama. Picha Na Humphrey Shao.