Sunday, January 22, 2012

Katika vita vya kupambana na umasikini Nchini Mbunge wa Temeke Abbasi Mtemvu amekabidhi kiasi cha shilingi millioni 14 kwa vikundi saba vya wajailiamali waliojiunga katika mpango wa VICOBA unaoratibiw ana PFT . Akizungumza wakati wa kukabizi hundi hzo mbunge wa Mtemvu alisema kuwa fedha hizo zitawawezesha wana kikundi hao kujikopesha wenyewe kwa wenyewe hili waweze kujikwamua na umaskini na kuzijengea uwezo jamii iliyokata tama. “ni vema kila mtu akajiunga na vikundi vya vicoba hili aweze kupata fursa mbalimbalizinazotolewa na tasisi mbalimbali na serikali kwani ni vigumu kumsaidia mtu mmoja mmoja lakini kwenye vikundi ni raisi ” Alisema Mtemvu . Katika hafla hiyo iliyo hudhuriwa na Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Dar es salaam Mariamu kisangi alisema kuwa ni wakati wa wanawake kuamka na kuchangia fursa zilizopo na kujikwamua kiuchumi . Alisema kuwa mwanamke wa sasa na mjanja ni yule anayejishughulisha na shughuli za Maendeleo na hakuna Maendeleo bila ya kujiwekea akiba hivyo ni vema kila mwanamke akajihakikishia akiba hili aweze kuendesha familia . Pia alitoa wito kwa kina baba kuacha kwasumbua wake zao pindi wanapo jiunga na vicoba hivyo kwa kufanya hivyo watakuwa wanarudisha Maendeleo ya mwanamke nyuma kila siku .


1 comment: