Monday, November 21, 2011

Makamu Waziri wa Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Mheshimiwa Jiang Yaoping(kulia) akitoa zawadi kwa  Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo (kushoto ) jana jijini Dar es salaam mara baada ya kutia saini   hati ya mikataba mitatu(3 )ya mikopo isiyo na riba yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 89.8 na barua ya msaada wa ujenzi wa Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere kwa thamani ya Dola milioni 5.6  jana jijini Dar es salaam .
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Mandeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimio ya Kamati kuu ya chama hicho moja wapo kwenda kumuona Rais Jakaya Kikwete kuhusu muswada wa katiba. Mazungumzo hayo yalifanyika makao Makuu ya Chama hicho Dar es Salaam jana. (Wengine katika picha toka kushoto) ni Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho zanzibarSaid Issa Mohamed na Katibu Mkuu wa Chamam hicho Dk. Willbroad Slaa
Wajumbe wa Kikao cha cha Kamati Kuu cha Chama  cha Mapinduzi   wamesimama  kwa ajili ya kuwakalibisha viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho walipokuwa wakiingia ukumbini kwa ajili ya  kufunguliwa na Mwenyekiti wake , Jakaya Kikwete.

No comments:

Post a Comment