Monday, November 28, 2011

ANTIVIRUS" BURUDANI KWA MASHABIKI MUZIKI UNALIPA ILIVYOSHEHENI WATU


Muonekano wa Stage
Soggy






Raia wakiwa tayari kwa show
Vinega wakiwa jukwaani
Sugu aki perform uwanjani hapo
Umati wa watu walioudhuria tamasha hilo
Muonekano wa stage
Vinega wafuasi wakiwa wamejaa
Wanaharakati wakiwa na bango lenye ujumbe
Soggy nae akiachia burudani kwa mashabiki
Maandalizi ya Stage



Hizo ni baadhi tu ya picha ila kwa picha za matukio zaidi zita
WASANII NA WAHESHIMIWA WAKIVUNJA (ANTIVIRUS) VINEGA NA KUFUNIKA SHOO YA DMX VILIVYO


Mheshimiwa Mbowe Mbunge wa Hai mkoani Kilimanjaro (CHADEMA) akitoa salamu kwa mashabiki
Hard Mad Kidume nae alikuwepo
Joseph Mbilinyi (MB) Mbeya a.k.a Sugu akivunja ki mzuka zaidi
Mashabiki wakiwa na furaha
Mr. Simple pia ni diwani
Mkoloni akivunja
Dj Sox from Mabaga Fresh
Daz Baba akivunja kwa hisia kali
Unamkumbuka Sister P? basi nae alikuwepo
Zay to the B mwana dada gaidi shavu moja na Sister P nae alivunja

Picha kutoka Global

0 comments:

Post a Comment


MIMBA YA WEMA YACHOROPOKA DIAMOND ALILIA KIUMBE CHAKE

HUJAFA hujaumbika! Ni habari mbaya inayogusa ‘kapo’ ya Wema Isaac Sepetu na Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond’ baada ya mnyange huyo kupoteza uzao wao kufuatia mimba yake ya takribani miezi miwili kuchoropoka, Ijumaa Wikienda linairusha hewani ‘laivu’ bila chenga.

TUJIKUMBUSHE SIKU YA FURAHA
Wiki kadhaa zilizopita, huku akiwa na furaha, Wema ambaye ni staa mkubwa wa filamu za Kibongo, alisimama mbele ya kamera za video za gazeti ndugu la hili, Risasi Mchanganyiko na kuthibitisha kuwa ana ujauzito wa mwezi mmoja na nusu baada ya kutoka kwenye vipimo (pregnancy test).

“Ni jambo la furaha sana, ni muda muafaka kwangu kupata mtoto,” alinukuliwa Wema akiwa hachezi mbali na ubuyu, ndimu na maembe mabichi.
CHANZO
Wiki mbili baadaye, The Biggest IQ Paper, Ijumaa Wikienda lilipokea simu kutoka kwa chanzo chake na mazungumzo yalikuwa hivi;
Chanzo: Ijumaa Wikienda mna habari?Wikienda: Habari tunazo nyingi tu, soma magazeti ya Global Publishers, lakini kama una ya kwako, nayo ni muhimu ukitupatia tutairusha hewani.
Chanzo: Kwa taarifa yenu, mimba ya Wema imechoropoka na hapa tunapozungumza yupo hoi kitandani, anaumwa.
Wikienda: Una uhakika? Amelazwa hospitali gani?
Chanzo: Kwani nilishawahi kuwadanganya? Yupo nyumbani anakoishi na Diamond, Sinza-Madukani, Dar. Sitaki mahojiano zaidi, fuatilieni mtajua ukweli na tafadhali naomba msinitaje.
IJUMAA WIKIENDA MZIGONI
Baada ya maelezo hayo, Ijumaa Wikienda lilizama mzigoni na kujikusanyia data zilizokaribia kwenye ukweli kutoka kwa watu wa karibu na wapenzi hao.
Hata hivyo, timu ya Ijumaa Wikienda ilipotaka kumuweka Wema kwenye ‘tageti’, alisafiri na Diamond kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya shoo na mapumziko mafupi.
AREJEA BONGO, AWEKWA ‘MTUKATI’ Aliporejea Bongo mwishoni mwa wiki iliyopita, Ijumaa Wikienda lilimuweka ‘mtukati’ na kumtaka kuonesha kibendi kilipoyeyukia. Alifunguka huku akijua kuwa akibisha, aibu itamfika kwani hana tena kile kitumbo kilichogeuka kero kwa mastaa wenzake kufuatia kutema mate ovyo.
Alisema: “Ilikuwa Jumatatu ileee (wiki mbili zilizopita), nilikuwa katika hali mbaya na baadaye niligundua kuwa mimba yangu inachoropoka. Nilikimbilia ‘famasi’ ya Primar na kumweleza mtaalamu hali yangu.“Aliniambia mimba yangu imechoropoka hivyo nilipatiwa dawa kwa ajili ya kusafisha kizazi.
MUNGU HAKUPANGA AZAE?
“Ukweli niliumia sana, lakini nilijua Mungu hakupanga nizae wakati huu, najua amenipangia muda muafaka.“Nahisi chanzo ni vipigo vya ‘toto yangu’ (Diamond Platinum Baby), lakini pia nahisi ni kwa sababu ya matumizi ya pombe kali.
DIAMOND ALIA KAMA MTOTO MDOGO
“Nilipomjulisha Diamond juu ya kupoteza kiumbe chake tumboni, alijisikia vibaya sana, alilia kwa uchungu kama mtoto mdogo.
“Kwa sasa niko fiti kabisa na namuomba Mungu nishike ujauzito mwingine kwani natamani kupata mtoto kuliko kitu kingine chochote.”
DIAMOND VIPI?
Diamond alikiri kumtandika Wema kutokana na kushindwa kuzuia hasira hasa mwanadada huyo anapomkosea, lakini hakuweza kuzungumzia kuchoropoka kwa ujauzito huo.
“Hata makofi muda mwingine yanafunza,” alisema Diamond.http://www.globalpublishers

BAADA YA MKUTANO WA JK NA VIONGOZI WA CHADEMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wa Serikali yake leo, Jumapili, Novemba 27, 2011, amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, yamefanyika katika mazingira ya urafiki na ujumbe wa CHADEMA umewasilisha mapendekezo yake kuhusu mchakato wa kuandika Katiba Mpya ya Tanzania. Serikali imepokea mapendekezo hayo.

Hata hivyo, pande zote mbili zimekubaliana kukutana tena asubuhi ya kesho, Jumatatu, Novemba 28, 2011, ili kuipa nafasi Serikali iweze kutafakari mapendekezo hayo.

Lakini pande hizo mbili zimekubaliana kuwa Katiba ya sasa ni Katiba nzuri iliyolilea Taifa kwa miaka 50 iliyopita kwa sababu ni Katiba ya sasa iliyoliwezesha Taifa la Tanzania kuwa na amani,  utulivu na kupata maendeleo makubwa ambayo nchi yetu imepata mpaka sasa.

Pia pande zote mbili zimekubaliana kuhusu umuhimu wa kutunga Katibu Mpya kama Mheshimiwa Rais Kikwete alivyoliahidi taifa wakati wa salamu zake za mwaka mpya Desemba 31, mwaka jana, 2010, Katiba ambayo italiongoza Taifa la Tanzania kwa miaka mingine 50 ijayo.

Katika mazungumzo hayo, Mheshimiwa Rais aliwahakikishia wajumbe hao wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Mheshimiwa Freeman Mbowe kuwa ni dhamira yake na ya Serikali yake kuhakikisha kuwa Tanzania inapata Katiba mpya.

Katika mkutano huo, pande zote mbili zimekubaliana kuwa ni jambo muhimu sana kwa mchakato mzima wa kutungwa kwa Katiba Mpya kuendeshwa kwa namna ya kulinda na kudumisha tunu za taifa za amani, utulivu na umoja wa kitaifa.

Aidha, pande zote mbili zimekubaliana kuwa mchakato huo uendeshwe kwa kuzingatia misingi ya mambo mengine muhimu kwa taifa la Tanzania kama vile kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani, kuligawa Taifa kwa misingi ya udini na ukabila ama kutugawa kwa misingi ya maeneo.  
IMETOLEWA NA:
 KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
NOVEMBA 27, 2011
DAR ES SALAAM

Monday, November 21, 2011

Makamu Waziri wa Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Mheshimiwa Jiang Yaoping(kulia) akitoa zawadi kwa  Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo (kushoto ) jana jijini Dar es salaam mara baada ya kutia saini   hati ya mikataba mitatu(3 )ya mikopo isiyo na riba yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 89.8 na barua ya msaada wa ujenzi wa Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere kwa thamani ya Dola milioni 5.6  jana jijini Dar es salaam .
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Mandeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimio ya Kamati kuu ya chama hicho moja wapo kwenda kumuona Rais Jakaya Kikwete kuhusu muswada wa katiba. Mazungumzo hayo yalifanyika makao Makuu ya Chama hicho Dar es Salaam jana. (Wengine katika picha toka kushoto) ni Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho zanzibarSaid Issa Mohamed na Katibu Mkuu wa Chamam hicho Dk. Willbroad Slaa
Wajumbe wa Kikao cha cha Kamati Kuu cha Chama  cha Mapinduzi   wamesimama  kwa ajili ya kuwakalibisha viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho walipokuwa wakiingia ukumbini kwa ajili ya  kufunguliwa na Mwenyekiti wake , Jakaya Kikwete.