Wednesday, September 21, 2011

Wednesday, September 21, 2011

*MAKAMU WA RAIS DKT BILAL MGENI RASMI UTIAJI SAINI MKATABA WA MIRADI YA MAKAA YA MAWE YA MCHUCHUMA NA CHUMA CHA LIGANGA BAINA YA NDC NA KAMPUNI YA CHINA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye utiaji saini mkataba wa miradi ya Makaa ya Mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, baina ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya nchini China, uliofanyika kwenye ukumbu wa Mlimani City Dar es Salaam, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika Bendera maalum ya kumbukumbu ya watu wa China,  wakati Mwenyekiti wa Bodi ya NDC, Christant Mzindakaya (kulia) na  Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya China, Liu Canglong, (kushoto) wakisainiana mkataba wa miradi ya Makaa ya Mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga katika  ukumbi wa mlimani City jijini Dar es Salaam, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akishuhudia zoezi la utiaji saini mkataba wa miradi ya Makaa ya mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, baina ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na Kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya China, wakati Mwenyekiti wa Bodi ya NDC, Christant Mzindakaya na Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni hiyo, Liu Canglong, wakisainiana mkataba huo katika ukumbi wa mlimani City jijini Dar es Salaam, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akishuhudia zoezi la utiaji saini na kubadilishana  mkataba wa miradi ya Makaa ya mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, baina ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na Kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya China, wakati Mwenyekiti wa Bodi ya NDC, Christant Mzindakaya na Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni hiyo, Liu Canglong, wakisainiana mkataba huo katika ukumbi wa mlimani City jijini Dar es Salaam, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) Christant Mzindakaya, nje ya ukumbi wa Mlimani City.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya Sichuan Hngda Corporation Ltd, Liu Canglong, baada ya kuhudhulia zoezi la utiaji saini mkataba wa miradi ya Makaa ya Mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga.
Kutoka Kulia, Ni Deo Filikunjombe, Zitto Kabwe na mhamud Mgimwa, ambao ni miongoni mwa wajumbe, wakiwa katika hafla hiyo.

Wednesday, September 14, 2011

JK ATEGUA KITENDAWILI CHA WAKUU WA MIKOA

14 Septemba, 2011
                                                                      
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 
RAIS KIKWETE ATEUA WAKUU WA MIKOA WAPYA
 
RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Mikoa nchini.
 
Katika mabadiliko hayo, amewateua Wakuu wa Mikoa wapya 15, kuwabadilisha vituo vya kazi Wakuu wa Mikoa watano na wengine saba wamestaafu kwa mujibu wa taratibu. Mkuu wa Mkoa wa Singida amebaki kwenye kituo chake cha kazi wakati Wakuu wa Mikoa wengine wanne watapangiwa kazi nyingine.
 
Aidha, Wakuu wa Mikoa mipya minne ya Simiyu, Geita, Katavi na Njombe itakayoundwa baada ya taratibu kukamilika watatangazwa baadaye.
 
Kwa mujibu wa mabadiliko hayo, Wakuu wa Wilaya 11 wamepandishwa Vyeo na kuwa Wakuu wa Mikoa kama ifuatavyo: Bw. John Gabriel Tupa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara; Bw. Saidi Thabit Mwambungu (Ruvuma); Bi. Chiku S. Gallawa (Tanga); Bw. Leonidas T. Gama (Kilimanjaro); Dk. Rehema Nchimbi (Dodoma); Bw. Elaston Mbwillo (Manyara); Kanali Fabian Massawe (Kagera); na Bibi. Fatma Abubakar Mwassa (Tabora). Wakuu wa Wilaya wengine walioteuliwa ni Bw. Ali Nassoro Rufunga, (Lindi); Eng. Ernest Welle Ndikillo, (Mwanza); na Bw. Magesa Stanslaus Mulongo Mkuu wa Mkoa (Arusha).
 
Walioteuliwa nje ya nafasi hizo ni Eng. Stella Manyanya (Rukwa); Bibi Mwantumu Mahiza, (Pwani); Bw. Joel Nkaya Bendera (Morogoro) na Bw. Ludovick Mwananzila (Shinyanga).
 
Waliobadilishwa vituo vya kazi ni Bw. Abbas Kandoro anayekwenda Mbeya akitokea Mwanza; Bw. Said Mecki Sadiki anayekwenda Dar es Salaam akitokea Lindi; Bibi Christine Ishengoma anayekwenda Iringa akitokea Ruvuma; Lt. Kanali Issa Machibya anayekwenda Kigoma akitokea Morogoro; na Kanali Joseph Simbakalia anayekwenda Mtwara akitokea Kigoma. Dk. Parseko Ole Kone ataendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.
 
Waliostaafu ni Bw. Mohammed Babu, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera; Bw. Isidore Shirima aliyekuwa Arusha; Kanali (mst.) Anatory Tarimo aliyekuwa Mtwara; Bw. John Mwakipesile, aliyekuwa Mbeya. Wengine ni Kanali Enos Mfuru aliyekuwa Mara; Brig. Jen. Dk. Johanes Balele aliyekuwa Shinyanga; na Meja Jen. Mst. Said S. Kalembo aliyekuwa Tanga.
 
Wakuu wa Mikoa wanne waliostaafu ambao watapangiwa vituo vingine vya kazi ni Bibi Amina Mrisho aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani; Dk. James Msekela aliyekuwa Dodoma; Bw. Abeid Mwinyimusa aliyekuwa Tabora na Bw. Daniel Ole Njoolay aliyekuwa Rukwa.
 
Wakuu wote wa Mikoa waliopo sasa wameagizwa kuandaa Hati za Makabidhiano (Handing Over Notes) katika muda wa siku 14 kuanzia siku ya kuapishwa kwa Wakuu wapya wa Mikoa. Aidha Wakuu wa Wilaya ambao wamepandishwa vyeo kuwa Wakuu wa Mikoa nao wanapaswa kufanya hivyo hivyo kwa ajili ya Wakuu wa Wilaya watakaopangiwa vituo vitakavyokuwa vimeachwa wazi kutokana na uteuzi wao.
 
Wakuu wa Mikoa ile minne mipya na Wakuu wa Wilaya watakaoteuliwa hapo baadaye nao watatakiwa kuandaa Hati za Makabidhiano ndani ya siku 14 tangu kuapishwa.
 
Makabidhiano hayo lazima yahusishe pia kutembelea kwa pamoja baadhi ya maeneo na miradi ambayo ni muhimu kama sehemu ya makabidhiano yao.
  
Wakuu wote wa Mikoa walioteuliwa na Wakuu wa Mikoa minne mipya wakaoteuliwa  pamoja na Wakuu wote wa Wilaya watakaoteuliwa baada ya zoezi kukamilika watatakiwa kuhudhuria mafunzo ya wiki tatu kwenye Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo zaidi wa kiuongozi na kiutendaji.
 
Wakuu hao wapya wa mikoa wataapishwa siku ya Ijumaa, Septemba 16, 2011 saa 4.00 asubuhi kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
 
Wakuu hao wapya wa mikoa; vituo wanavyokwenda na vituo walivyotoka ni kama ifuatavyo:
 
Na.
JINA LA MKUU WA MKOA
KITUO AENDAKO
KITUO ATOKAKO
1.      
Bw. Saidi Mecki Sadiki
DAR ES SALAAM
RC - Lindi
2.      
Bw. John Gabriel Tupa
MARA
DC - Dodoma
3.      
Bw. Saidi Thabit Mwambungu
RUVUMA
DC - Morogoro
4.      
Kanali Joseph Simbakalia
MTWARA
RC Kigoma
5.      
Bi. Chiku S. Gallawa
TANGA
DC - Temeke
6.      
Bw. Abbas Kandoro
MBEYA
RC Mwanza
7.      
Bw. Leonidas T. Gama
KILIMANJARO
DC – Ilala
8.      
Dkt. Parseko Ole Kone
SINGIDA
RC Singida
9.      
Eng. Stella Manyanya
RUKWA
Mbunge V/Maalum
10.  
Bibi Christine Ishengoma
IRINGA
RC Ruvuma
11.  
Dk. Rehema Nchimbi
DODOMA
DC - Newala
12.  
Bw. Elaston John Mbwillo
MANYARA
DC – Mtwara
13.  
Col. Fabian I. Massawe
KAGERA
DC - Karagwe
14.  
Bibi. Mwantumu Mahiza
PWANI
Mbunge/NW Mstaafu
15.  
Bibi. Fatma A. Mwassa
TABORA
DC - Mvomero
16.  
Bw. Ali Nassoro Rufunga
LINDI
DC - Manyoni
17.  
Eng. Ernest Welle Ndikillo
MWANZA
DC - Kilombero
18.  
Lt. Col. Issa Machibya
KIGOMA
RC Morogoro
19.  
Bw. Magesa S. Mulongo
ARUSHA
DC - Bagamoyo
20.  
Bw. Joel Nkaya Bendera
MOROGORO
Mbunge/NW Mstaafu
21.  
Bw. Ludovick Mwananzila
SHINYANGA
Mbunge/NW Mstaafu
 
 
 

Tuesday, September 13, 2011

WAANDISHI WAFANYA ZIARA KWENEYE NDEGE

Bw.Abdul Aziz Alhai Kulia akizungumza na wandishi wa habari
yake  Dubai, leo imekuwa mwenyeji  wa wawakilishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari na mawakala wa usafiri katika kuwafahamisha huduma zake na shughuli wazifanyazo  Tanzania.
Akizungumza baada ya ziara ya ndege ya
Emirates wenyeji wa wadau wa usafiri Tanzania
DAR ES SALAAM, TANZANIA: Sept 13, 2011: kampuni ya Emirates ya kimataifa yenye makao Emirates katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere ' Meneja wa Emirates bwana  Abdul Aziz Al Hai alisema ziara ilikuwa na nia ya kuleta uzoefu wa Emirates na ukarimu wake  kwa wakala wa usafiri na wanahabari, kama wadau wakuu wa biashara ya usafiri wa anga. 
Ziara hii ni muhimu kwetu kwani tunataka kujenga mahusiano  na washirika wetu wa kibiashara na vyombo vya habari hapa nchini Tanzania. Kwa uzoefu wa ndege za  Emirates na bidhaa zake zenye ubora na kupata kujua ubora wa huduma zetu ambazo tungependa wakala wa usafiri  na vyombo vya habari  hapa Tanzania kuufahamu ubora wa bidhaa  zetu” alisema Al Hai. 
Aliendelea kusema: “Emirates, tunaendelea kutafuta njia mpya za kufanya kazi na washirika wetu ili kuboresha huduma zetu kwa wateja wetu. kwakuwa tunafanya kazi na  mawakala wa usafiri tunataka wateja wetu kuwa na uzoefu mzuri na  Emirates kuanzia wanaponunua tiketi kwao. Pia tunatambua mchango wa vyombo vya habari ulioutoa na unaoendelea kuutoa  kwa kuujulisha umma kuhusu biashara zetu hapa Tanzania”.  
Bwana Al Hai alibainisha kwamba tangu Emirates imeanza shughuli zake hapa Tanzania, biashara ya usafiri wa anga  imekuwa ikiongezeka, na kuongeza kuwa Tanzania ni soko muhimu kwa Emirates katika kanda ya Afrika Mashariki.
“Tumeona ukuaji mkubwa hapa  Tanzania ambapo umeongeza mapato ya Emirates katika kanda ya Afrika Mashariki. Kufanya kazi na mawakala wa usafiri katika vituo vyote ambapo nguvu ya kusafiri kwetu kunaendana  na ubora wa Emirates unaotoa kwa raia wa nchi hii,” alisema.
Aliongezeakwa kusema  ahadi ya Emirates kwa utoaji wa huduma zenye viwango vya juu umeonekana kwenye tuzo 400 za ubora wa kimataifa iliyozipata  tokea ilipoanza huduma zake miaka 25 iliyopita.
Bwana Al Hai pia alibainisha kwamba Emirates imeorodhesha idadi ya ofa maalumu kwa wasafiri wa Tanzania,kuanzia kifurushi cha kituo cha Dubai  mpaka Summer Smiles, na vimebuniwa kusaidia familia kukutana pamoja na kufurahia ubora unaotolewa na Dubai.


“Kwa sasa Dubai ni sehemu yenye punguzo la pekee kuliko sehemu nyingine yoyote.Taarifa ya fedha tuliyorekodi mwaka jana imetusaidia kuanzisha mipango yakinifu.Thamani Ya wateja wetu wa Tanzania inatazamia kuleta ofa maalumu kwa miezi michache ijayo,” alisema

Emirates ni moja ya mashirika ya ndege yanayokua kwa kasi duniani  ambapo kwa sasa inatoa huduma kwa vituo 114 katika nchi 67, ripoti ya mwaka wa fedha iliyopita inaonyesha faida kamili ni dola milioni 964 kwa ongezeko la idadi ya abiria.Ndege  imebeba abiria milioni 31.4 kwa mwaka 2010 -2011 mpaka asilimia 14.5 kuanzia mwaka 2009-2010 na tani milioni  1.8 za mizigo, mpaka asilimia 11.8 katika kipindi hicho.
“Mafanikio yetu yametokana na dhamira yetu ya kuongoza sekta hii kwa ubunifu. Tunafanya mambo kwa utofauti. Tunaelewa umuhimu wa kuendelea kuwa wabunifu katika kutimiza mahitaji wa wateja wetu.Hii imetuwezesha sisi kuwa mstari wa mbele katika soko na tunatazamia maendeleo mapya kwa mwaka huu kutoka kwenu kama washirika wetu,” alisema.
Shirika hili la ndege  lilianza kutoa huduma zake hapa Tanzania mwaka 1997 na sasa linatoa huduma za kila siku katika kiwanja cha kimataifa cha  Mwalimu Julius Nyerere na Dubai

……….End……….

TAKWIMU ZA UCHUMI ADHARANI

Mkurugenzi wa masuala ya takwimu Bw.Morrice Nyattega akizungumza na waandishi juu ya masuala ya Takwimu ya uchumi ya robo mwaka

Friday, September 2, 2011

Libeneke jipya la wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania


Kwanza tunapenda kuwasalimu sana Ndugu walimu na wanafunzi na wadau wote mliopo popote nchini Tanzania na Duniani kwa ujumla, Kwa heshima na Taadhima tunapenda kuwatambukisha kwenu Blog mpya kabisa inayo kwenda kwa jina la MATUKIO NA WANAVYUO ambapo lengo kubwa ni kuwakutanisha wanavyuo wote Nchi nzima na kubadilishana mawazo pia kujua nini kinaendelea kila wakati kupitia mtandao huu, Hatuna mengi sana ya kuandika hapa kwa maana mtandao wenu unajieleza vizuri kabisa, pia mtandao huu ni wanavyuo wote waliopo vyuoni sasa na wale walio maliza pia ni wa watanzania wote kwa ujumla kwa maana kuna mambo yanayo wahusu na muhimu. Tunawaomba mpitie kila kona ya mtandao huu na kutoa maoni kama yapo nini kiongezwe ama kuboreshwa zaidi, Tunawakumbusha tena mtandao huu ni wako. 
Sisi tunaongoza tuu kwa mawasiliano zaidi tutumie Barua pepe kupitia
( twanavyuo@live.com)
tunatanguliza  shukrani zetu pia atakae pata taarifa hii ampe na mwenzake
Asanteni sana.
Matukio na wanavyuo Crew
'BREAKING NEWS.....MUAMMAR GADDAFI AANGUA KILIO' NI BAADA YA NAKALA YA KITABU CHAKE KUCHOMWA MOTO NA WAASI

TRIPOLI,LIBYA
Mummar Gaddafi ambaye alikuwa rais wa Libya kwa miongo zaidi ya minne na siku 363, mwaka  1975 aliamua kuandaa falsafa za utawala wake kwa kuandaa kitabu maalum cha kijani (Green Book) ambacho kilijikita katika falsafa za kisiasa, uchumi na utawala wa ujamaa.

Kwa mujibu wa wanaharakai wanasema kwamba kupitia ‘falsafa ya ulimwengu wa tatu’ katika kitabu chake cha Kijani(Green Book), Kanali Qaddafi aliweza kuijenga Libya kuanzia nyanja za kisiasa, uchumi, mfumo wa ulinzi imara wa kijeshi.

Kufanikiwa kuanzisha na kuiendesha Jamahiriya ya watu walibya, miundombinu bora, ujamaa na utawala wa watu wa kushiriki katika maendeleo moja kwa moja toka 1975  na kuebdelea.

Dhumuni kubwa la kitabu cha kijani, kanali Gaddafi anasema ni kuelimisha wapinzani  ili waweze kutambua nafasi na namna ambavyo mahitaji ya walibya kupitia mfumo wa ujamaa yanavyotekelezwa.

Green Book ni kitabu kidogo ambacho kinaelezea kwa undani juu ya masuala ya siasa  za Libya  kikilenga kuwafikia walibya wote ili waweze kukisoma na kifahamu kile ambacho  wanapaswa kufanya na yale  ambayo walipaswa kuyapuuza kutoka kwa maadu ili waweze kupiga hatua za kimaendeleo.

Kitabu hicho ambacho kimeandikwa kwa lugha nyepesi yenye kueleweka na wananchi mbalimbali  hususan lugha ya kiharabu na kiingereza kimeambatanishwa na nukuu mbalimbali ambazo zinatia hamasa  ya usomaji.

Ambapo kilifanikiwa kusambazwa ndani na nje ya nchi, inasadikika kwamba toka vita vya kumuondoa madarakani kanali Gaddafi maelfu kwa maelfu ya nakala za kitabu chake hicho zimechomwa na  waasi ili kupoteza kumbukumbu za kitabu hicho kuenziwa.

Kwa mujibu wa wanaharakati wanasema kwamba kitabu hicho kutokana na uzito wake ndani ya taifa la Libya toka kitungwe  watoto  nchini humo huwa wanatumia masaa mawili kila  wiki, kujifunza kitabu hicho kama sehemu yao ya mitaala ya masomo

Huku  kikitangazwa kila siku  katika vituo vya television na redio, licha ya kwamba taratibu za kuelezea kitabu hicho zinapatikana katika mbao mbalimbali kubwa za matangazo   nchini humo.

Kitabu hicho ambacho kimegawanyika katika sehemu kuu tatu  kina kurasa 110 huku kila ukurasa ulioandikwa kwa lugha nyepesi ukiwa na maneno mia mbili.

Moja wapo ya mambo ya msi ngi katika kitabu hicho yaliyoainishwa ni pamoja na suluhisho la matatizo ya demokrasia na utawala wa watu (kilichapwa mwanzoni mwa 1975).

Shemu ya pili ya kitabu hicho kinaelezea kwa undani juu ya Suluhisho la  changamoto zinazokumba sekta ya uchumi kupitia mfumo wa ujamaa  ambacho kilipigwa chapa mwaka  1977.

Sehemu ya tatu ya kitabu chake ambacho kilipigwa chapa Septemba , 1981 ambacho kinaeleza kwa kina juu ya misingi ya ya jamii hususan uwajibikaji na utekelelezaji wa wajibu kwa kufuata nadharia ya kimataifa .

Suala la kwanza ni pamoja na msimamo wake ambao anasisitiza kwamba  kwa kuwa wanawake huwa wanateseka zaidi katika jamii kutokana na ubebaji wa uchungu ni lazima wapewe fursa ya kiutendaji ndani ya taifa ilikuwarejeshea matumaini.

 "Wanawake, kama watu, ni binadamu, huu ni ukweli usiopingika... Wanawake ni tofauti na watu katika mfumo wamaisha kwa sababu ni wanawake,ukiangalia hata katika  ufalme wa mimea na wanyama wanawake wote wana umuhimu tena wa pekee tofauti na wanaume wana upee wao na nafasi yao pia,” anasema Kanali Gaddafi.

Anasema katika kitabu hicho cha kijani kwamba kwa mujibu wa Uzazi wanawake, ni tofauti na wanaume, kwani wao uvunja ungo kila mwezi  na hata uzoefu wa kubeba mimba  huku akinyoyesha kwazaidi ya miaka miwili kinyume kabisha na wanaume hivyo ni wajibu wa kila jamii kumrejeshea heshima mwanamke na  hata kupewa kipaumbele.

Kanali Gaddafi katika kitabu chake hicho anaendelea kusema kuwa  kila  jambo lina mwanzo na mwisho wake kwani miaka nenda rudi Afrika ilitawaliwa na rangi nyeupehadi kufikia hatua ya kupoteza taswira hivyo basi ni zamu ya waafrika nao kujitawala.

. "Kuna mzunguko katika  historia ya kijamii kwani  utawala wa mbio za njano wao waliona ni manufaa kwao kupitia  dunia, wakati walikuja kutoka Asia rangi nyeupe ya majaribio katika maeneo  ya utawala wengine wakatokea Magharibi hadi kufikia mabara yote kuingia Afrika, waliweza lakini sasa basi,sasa ni zamu ya watu weusi kupiga mbio za kiutawala katika dunia, " anasema Kanali Gaddafi.

Anasema maisha ya kila siku haiwezekani mtu mmoja kujimilikisha rasilimali ambazo  zinaziba nafasi kwa wengi kupata mafanikio huo utakuwa siyo mfumo stahiki wa kudumisha demokrasia na ujamaa kwa kuwa watu wote wana haki  za asili za kujieleza kwa njia yoyote ile haijalisha hata kama muhusika ni mwendawazimu ni lazima apewe nafasi.

“Watasema sana lakini, yote yanayosemwa yanatokana na maneo ya kizushi, ukweli ni kwamba kila mmoja ana haki ya kumiliki mali sawa, ujamaa kupitia demokrasia na haki ya kusema, lazima elimu ipatikane kwa taratibu za kufuata mfumo wan chini yetu kila siku haijalishi, hatuwezi kuendeshwa kwa kusahau uhalisia wetu ndiyo maana tukiwapa nafasi sana watakuwa wanatuendesha,” anasema Kanali Gaddafi.









Inasadikika kwamba maelfu kwa maelfu ya nakala ya kitabu hicho zimechomwa moto na waasi toka wapindue mamlaka ya Gaddafi mwaka huu, mjini Tripoli.