Thursday, November 14, 2013



Na Jennifer Ullembo

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, anatarajia kuachia albamu yake ya kwanza, Januari au Februari mwakani.

Akizungumza na Rai jana, msanii huyo alisema, albamu hiyo ni ya kwanza tangu, alipoanza kujihusisha na masuala ya muziki wa bongo fleva.

Alisema albamu hiyo itakuwa na nyimbo 10, huku nyimbo zake zote zilizoweza kutamba na kumtambulisha zikiwa ndani yake.

“Nilianza na Nainai, hata zile zilizofatia na hizi za sasa hivi, zitakuwemo kwenye albamu yangu hii, mpya mbayo ni mara kwanza kuachia kwa kipindi kirefu,”alisema Ommy Dimpoz.

Msanii huyo alisema, anatarajia kumuachia jukumu la kutafuta jina la albamu, meneja wake Mubenga, ambapo kama albamu hiyo itachelewa haitavuka siku ya Valentine mwakani.


Na Jennifer Ullembo

MSANII wa muziki wa kizazi kipya,  Sunday Mangu ‘Linex’, anatarajia kutambulisha, msanii mpya  ambaye ametokea, kwenye kundi lake la Sauti za Afrika ‘VOA’.

Akizungumza na Rai jana, Linex alisema, msanii huyo atajulikana kama Ssen Lubi na tayari amefanikiwa kufanya wimbo wake, alioupa jina la ‘Kiroho Safi’.

Linex alisema, Lubi ni msanii mpya , ambaye amekuzwa na kupewa mafunzo zaidi, kupitia kundi lao la VOA.

“Msanii huyu ni mpya, najivunia kuvumbua kipaji hichi, anatarajia kuachia wimbo wake mpya wa Kiroho Safi, ambao amemshirikisha Chege Chigunda,”alisema Linex.
  
 Msanii huyo alisema, anaowamba wadau wa muziki kukipokea kipaji kipya, huku akihahidi kuendelea kuibua vipaji vya wasanii wengine wachanga.

Na Jennifer Ullembo
WASANII wa muziki wa kizazi kipya, Chege Chugunda ‘Chege’ na  ‘Temba’, wanatarajia kuachia wimbo wao mpya, uliopewa jina la ‘Kama Kasuku’.

Akizungumza na Rai jana, mmoja wa wasanii hao Chege, alisema kuwa tayari wameingia studio juzi, kuandaa kazi hiyo inayotarajiwa kuachiwa, kabla ya kumalizika kwa mwaka.

Chege alisema, ushirikiano ambao wamekuwa, wakiufanya kwa pamoja na Temba, umeweza kuwaongezea umaarufu zaidi, kwenye kazi zao.

“Tumepanga kumaliza mwaka huu, kwa kuachia wimbo wetu mpya wa Kama Kasuku, mashabiki wajiande kusikia kazi nzuri kutoka kwetu,”alisema Chege.

Msanii huyo aliendelea kusema, mbali na kuachia kazi hiyo ya Kama Kasuku, wanatarajia kufanya shoo mbalimbali za mwisho wa mwaka, ambapo tayari wameanza kupokea  maombi kutoka kwa mashabiki.

MAKAMU WA RAIS GHARIB BILAL NA JAJI MANETO WATO POLE KATIKAMSIBA WA DK MVUNGI






UMASKINI BADO TATIZO NCHINI



ufunguzi kil maathon









Mbunge wa Temeke Abasi Mtemvu akabidhiwa Tuzo ya Heshima na Dk Rahabu Mgunduzi wa Dawa ya Fitarawa

 Mtemvu akiwa na Dk Rahabu pamoja na Catherine Kahabi


 Mtevu na Dk Rahabu


 mtemvu akikabidhiwa tuzo yake






Roverr Community showcase the talents of Sober House art programs both from Zanzibar and Tanzania Mainland

 Abdalahman Abdalah Chair man akionyesha bahadhi ya kazi zilizofanyw ana vijana walio acha uteja.
 Mrembo huyu ambaye alikuwa Nesi kisha kujiingiza katika Dawa za kulevya
 Kucos mtaalamu wa michoro na ufinyangaji akiw ana kinyago chakecha malezi ya mama na mtoto
 computer akiwa katika kazi za kinadada




Tuesday, October 29, 2013

MAMA SALMA AFUNGUA MAONYESHO YA MOWE


 
MAMA SALMA
Mke wa Rais wa Tanzania Mama Salma Kikwete kivishwa mapambo ya kimasai na mjasiliamali wa kimasai ,Ester Labani Moreto kutoka kikundi cha USUPATI chalinze ,pindi alipokuwa akitembelea mabanda ya wafanyabishara hao wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya mwezi wa wajasiliamali wanawake (MOWE) yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam jana. Picha na Humphrey Shao.

 
STRABAG
Wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi  wa barabara ya mabasi yaendayo kasi katika barabara ya morogoro STRABAG wakiweka vizuri  rami katika eneo la Jangwani mara baada ya gari hilo kumwaga rami hiyo kwa wingi. PIcha na Humphrey Shao.


TRAFIC
Askari wa usalama barabarani mkoa wa Dar es Salaam akimuandikia cheti cha kulipa faini Dereva wa pikipiki mara baada kukutw ana makosa. Picha na Humphrey Shao.