Wednesday, February 20, 2013



Umuhimu wa kutunza Kumbukumbu Tunapoelekea urasimishaji
NA HUMPHREY SHAO

MARA zote tasnia ya sanaa na wasanii wenyewe wamekuwa watu wa kutoa lawama serikalini bila kustadi nini wanatakiwa kufanya hili kuweza kufikia weredi kama ilivyo kwa wasanii wengine wa kimataifa.

Hali hiyo imeelezwa na  mkurugenzi wa utafiti na na mafufunzo kutoka BASATA Godfrey  Lebejo wakati kutoa muadhara katika jukwaa la sanaa linalo andaliwa na BASATA kwa kushirikiana na CAJA uunaofanyika kila jumatatu katika ukumbi wa BASATA juu ya umuhimu wa wasanii kutuinza kumbukumbu tunapoelekea urasimishaji.

Lebejo anaanza kwa kutaja nini kinachotakiwa kumfanya msanii aweze kufanya utafiti wa kazi zake.

Dhana hasa ya tafiti ni kutakiwa kujiuliza maswali ama kuuliza maswali watu wengine kama wanavyofanya wachezaji mpira huku kukiwa na lengo moja la kupata jibu lilo sahii katika kufanikisha kazi yako ya sanaa.

Anataja kuwa chamsingi kinachotakiwa katika kufanya tafiti hili kuweza kupata habari ya kweli kwa ajili ya kuziba pengo lililopo katika tasnia husika, hivyo kusisitiza kuwa kama kuna tafiti inafanyika alafu aishuki chini kwa walengwa hiyo aina maana katika maendeleo ya Tanzania.

“ kama kuna la msingi wasanii wanatakiwa kufanya ni hili hapa la kujiuliza maswali haya (1) Nifanyeje kazi yangu (2) Nani mlaji wa kazi yangu (3) wapi ntauza kazi yangu (4) Soko likoje” alisema Lebejo.

Anawasilisha kuwa tafiti zinatoa hali halisi ya kazi za sanaa na sanaa kwa ujumla kujua ikoje na kutoa majibu nini kifanyike hili matatizo yaweze kuondoka.

Aliongeza kuwa kama msanii lazima ajiulize matatizo  gani yanayo ikabili sanaa na kwa kipindi chote ambacho  msanii yupo sokoni na kama anataka kuingiza kazi sokoni.

Katika urasimishaji wa kazi za sanaa Lebejo alisema kuwa serikali imeamua kurasimisha kazi kwa kuanzia kwenye muziki na filamu kufuatia kuwepo kwa tafiti juu ya hali halisi ya faida za kazi hizi katika kukuza pato la Taifa.

“kwa miaka mingi serikali imeshindwa kutambua jinsi gani sanaa zilivyocghangia katika pato la taifa licha ya kuwepo vyombo mbalimbali vya kusimamia kazi za sanaa hapa nchini” alisema Lebejo.

Alisema kuwa hali hiyo imetokana na serikali kutoingiza urasimu wa kazi za sanaa kuwa rasmi na kupuzia    mchango wake na kutotilia manani.

Alitaja sanaa kama za uchoraji na uchongaji zimekuwa zikingizia taifa fedha nyingi za kigeni kuliko sanaa nyingine huku ufumaji na upikaji wa nguo kama batiki zikifuatia kutokana na wageni wengi wanaofika hapa nchini kupenda bidhaa hizo lakini kiasi chote hicho utambiwa nimapato ya utalii na kusahau umuhimu wa sanaa.

Anatanabaisha kuwa hali hiyo ilitokana na sera ya utamaduni kutotamka sanaa kama kazi kama zilivyo kazi nyingine na kupelekea michango yao kuto onekana.

Mara baada ya kuwepo kwa mkanganyiko na malalamiko mengi kutoka kwa wasanii hapa nchini ilipelekea serikali kufanya tafiti kupitia mtafiti kutoka Chuo kikuu Yehova nisi na kutanabaisha kuwa sanaa inalipa hali iliyopelekea serikali kurasimisha kazi hizo kuanzia julai mwaka huu.

Lebejo alieleza kuwa serikali imeamua kutatua matatizo yaliyopo katika sekta ya sanaa kupita urasimishaji hivyo kutokana na matokeo ya matatizo yaliyopo katika sanaa.

“licha ya kuwepo kwa urasimishaji wa kazi za sanaa lakini bado kuna jambo gumu sana linalo onekana kwa wasanii wengi wa Tanzania kuwa ni wagumu kutunza kumbukumbu za kazi zao na matokeo ya kazi hizo hali iliyosababisha kuwepo na mgogoro mkubwa juu ya swala zima la haki miliki” alisema Lebejo.

Alitaja kuwa waimbaji wengi watanzania wamekuwa wakitumia haki miliki za watu na za mataifa mengine katika nyimbo zao hivyo taifa litakapoingia katika mchakato wa urasimishaji wa kazi hakuna nyimbo ya mtu yenye midundo itakayopigwa hapa nchini.

Alitaja mfano kuwa nyimbo nyingi za muziki wa injili zimeelemea katika midundo ya Afrika kusini na mingine Makhirikhiri na kusahau kuwa hiyo ni haki ya watu na utamaduni wao hivyo sheria itawataka kutumia midundo za makabila ya watanzania.

  Alisema kuwa midundo na maanzari za nje ya nchi kubanwa hali hiyo itawafanya wasanii wa kitanzania na waandaaji wanaochipua kama uyoga kuwa wabunifu.

Hilo litakwenda sambamba na wasanii wenyewe kujitambua kwa kuweza kuandaa taharifa zao binafsi ‘cv’ hili kufanya kutambulika kirahisi na watu wakimataifa.

Hali hiyo ilikwenda sambamba na wachangiaji mbalimbali kutoa maoni yao juu ya mada hiyo katika kufikia malengo ya kimataifa kwa wasanii wa ndani.

Sacha Emanuel ni mwandishi wa script na katibu wa shirikisho la wandishi wa Muswada ‘script’ wilaya ya ilala alishangazwa na mashirikisho kuwa mstari wa nyuma katika kutoa elimu nakupokea mafunzo yanayotolewa na basata kuwafikishia wasanii.

“shida ipo sana hapa nchini kwani wandishi wa miswada na waongozaji ambao mara zote wamekuwa watu wa kukopi vitu kutoka nje ya nchi kutokana na kuwa wavivu wa kufanya tafiti” alisema Sacha.

Nae Amisa Sambwe alitaka wasanii kujiuliza na kujisomea hili kujua ni tafiti gani wanatakiwa kufanya na kwa wakati gani zifanyike.

NA HUMPHREY SHAO

JINA la Isike Samweli  sio jina geni kwa wale wapenzi tunaofatilia kwa karibu sana filamu za hapa nchini na hata kung’amua ni msani gani anafanya vizuri licha ya kutokuwa na jina kubwa katika tasnia hii ya filamu.

Hivi karibuni nilipata nafasi ya kutembelea maeneo ya kariakoo kumuona rafiki yangu mwenye asili ya kihindi nayefahamika kwa jina la Purteshi kwa wale wadau wa filamu wanamjua mtu huyu ndipo nilipopata fursa ya kumuona kijana huyu katika ofisi hizo bila kung’amua ni nani.

Sekunde chache baadae anawasili msanii wa filamu mwingine Lucknes Mokiwa ambaye ni rafiki yangu wa karibu na kunitambulisha kuwa huyu ndio Isike, mtayarishjai mdogo kulikoi wote hapa Tanzania  nilishtuka kwani yupo tofauti na jinsi jina lake nilivyokuwa nikilisoma katika filamu mbalimbali.

Kama ilivyozoeleka hapa nchini ni vigumukuamini kijana mdogo wa miaka 19 kuwa mtayarishaji wa filamu nyingi ambazo hata hao wasanii maharufu awajafikia.
 
Isike ambaye alizaliwa Septemba mwaka 1993 na kupata elimu ya msingi katika shule ya msingi Magomeni na badae aliweza kucahaguliwa kujiunga na sekondari ya goba ambayo wilaya kinondoni.

Anaeleza kuwa hapo awali aliweza kujiusiha na utangazaji wa vipindi vya watoto lakini alipokuwa darasa la saba aliweza kushawishika moja kwa moja kujiunga na sanaa ya uigizaji.




“kama kuna mtu mwenye bahati ni mimi kwani niliweza kuingia kwenye sanaa kwa mguu wa kulia katika kikundi cha shirikisho na mara baada ya miezi sita niliweza kuchaguliwa kucheza igizo la ukumu ya tunu ambalo liliweza kunitambulisha huku kampuni ya kwanza kufanya nao kazi ilikuwa ni Benchmark” Alisema Isike.

 Alinieleza akiwa na umri wa miaka 16  aliweza kuandaa filamu yake hapo akiwa na  kuwa kama mtayarishaji wa kwanza mtoto hapa nchini.

Akiwa kidato cha kwanza Filamu hiyo ilikwenda kwa jina la ‘2 sister’ iliweza kuwashirikisha wasanii kama Masinde, penina na Hidaya Njaidi kisha kufuatiwa na filamu iliyokwenda kwa jina la ‘Missed Call’ ambayo iliwashirikisha Hashimu Kambi ,Tekla Mjata, Komando Yoso.

Mara baada ya kufanikiwa kuuza filamu hizo huku akitumia njia ya kusambaza mwenyewe  aliweza kupata mafanikio makubwa ambayo kamwe hato ya sahau maisha ni mwake.

“kama nilivyo kueleza mimi nilifiwa na wazazi wangu wote wawili nikiwa darasa la nne hivyo fedha hizo ziliwezesha kuanza kujitegemea kwa kupanga chumba changu mwenyewe na kuanza kujilipia ada yangu ya shule na kuacha kukaa kwa mjomba yangu ambaye alikuwa akinilea kwani mtazamo wake na wangu ulikuwa tofauti katika sanaa” alisema Isike.


Anaeleza kipato hicho kilimfanya aweze kuisadia familia yake pia na muda mchache baadae mwaka 2010 aliweza kupata mkataba na kampuni ya KAPIKO na kutenegenza filamu iliyokwenda kwa jina la ‘Love in School’.

Filamu hii ambayo aliweza kumshirikisha Flora Mvungi, Hidaya Njaidi Iliweza kufanya vizuri sokoni kuliko alivyotegemea na kupewa nafasi ya kufanya filamu nyingine katika kampuni hiyo ya KAPIKO.

‘The impact’ ndo jina la filamu hiyo ambayo iliweza kumshirikisha mwanadada mahiri Jackline Wolper, Hashim Kambi, Flora Mvungi nayo iliweza kufanya vema na kumpeleka katika ukurasa mpya wa maisha ya sanaa.


Mara baada ya hapo aliweza kupumzika kwa kipindi cha miezi minne kwa ajili ya kujiandaa na mitihani ya kidato cha nne.

Anaeleza kuwa kila kazi inachangamoto yake hasa kwa wakati uliopo Isike anakiri kuwa aliweza kupata changamoto kubwa sana kwa kucheleweshewa malipo yake na


bahadhi ya kampuni alizoingia nazo mkataba kulingana na umri wake kiasi cha kumkera sana.

Lakini anakiri kuwa amekuwa akiheshimiwa na wasani wakubwa kuliko alivyotegemea hali inayomfanya ajisikiea bora zaidi kuliko hapo awali.


Anatanabaisha kuwa mara baada kumaliza mitihani yake ya kidato cha nne aliweza kujiunga na kampuni ya PAPAZI ambayo iliweza kusaini nae mkataba kisha kufanya nao kazi ambapo mwaka 2012 aliweza kutoka na filamu iliyokwenda kwa jina la ‘Ivan Tears’  na kufanya poa katika soko la filamu.

Alitaja filamu hiyo iliyiomshirikisha mwanadada shilole na baadae kutoa filamu ya ‘loose control’ ambayo ilimshirikisha Catty ,Tecla Mjata, Kojack na Steve wamaisha Plus hapo ndio ulikuwa mwisho wa kufanyakazi na PAPAZI.


Baadae alifanya filamu ya ‘Jealous’ iliyowashirikisha Mainda , Hashimu Kambi na Hidaya Njaidi ambayo iliweza kusambazwa na kampuni ya Pastor Muyamba.

Hata hivyo nyota ilizidi kung’ara kwa kijana huyu kufanikiwa kupata mkataba na Kampuni ya SPLASH kwa kuanza na filamu ya Oxygen ambayo mwanadada Elizabeth Michael ‘LULU’alicheza kama star.

Filamu hiyo iliyofanya vema sokoni ilimfanya kuongezewa muda wa kufanya filamu nyingine na kampuni hiyo ndipo mwezi janauri mwaka huu alitoka na filamu inayokwenda kwa jina la lonely.

Filamu ambayo amefanya na hemedi suleimani na wengine wengi kuwa gumzo katika mitaa yote ya jiji la Dar es Salaam.

Filamu nyingine ambazo ameweza kufanya ni kama ‘Sad Moment’ na kukiri kuwa nidhamu na uti ndio silaha ya mafanikio katika kazi zake za sanaa licha ya watu kuongea mengi na kusahau nini wanatakiwa kufanya.

“kiukweli nitakuwa mnafiki nisipo washukuru wasanii wenzangu kama Dotnata, Jackline Wolper, Lucknes Mokiwa na wengine wengi kwa kuwa msaada mkubwa kwangu kwani wao ndio wamekuwa watu wa kunitia moyo kila siku.

Anaeleza kuwa ndoto zake ni kufika mbali na kimataifa zaidi kwani tayari njia imepatikana na kikubwa anachojivunia ni umri wake ambao unamruhusu kufanya mambo makubwa.


MWAJAUMA JIMAMA AIPAMBA MASHAUZI TCC

Mnenguaji Maarufu nchini Mwajuma Thabiti ' Mwajuma jimama' akifanya vitu vyake mbele ya mwimbaji wa bendi ya Mashauzi Classic, Isha Ramadhani wakati bendi hiyo ilipofanya onesho lake katika ukumbi wa TCC Chang'ombe Dar es salaam 
Mmoja wa mashabiki wa fani ya unenguaji  kulia akimpingia makofi baada ya kumtunza Mnenguaji Maarufu nchini Mwajuma Thabiti ' Mwajuma jimama' ambaye anaonekana akifanya vibwanga vyake  wakati wa maonesho ya bendi ya Mashauzi Classic katika ukumbi wa TCC Chang'ombe Dar es salaam
Mnenguaji Maarufu nchini Mwajuma Thabiti ' Mwajuma jimama' akifanya vitu vyake mbele ya mwimbaji wa bendi ya Mashauzi Classic, Isha Ramadhani wakati bendi hiyo ilipofanya onesho lake katika ukumbi wa TCC Chang'ombe Dar es salaam 
Isha Ramadhani kushoto akiwa na mnenguaji maarufu Mwajuma Thabiti ' Mwajuma Jimama'
Mnenguaji Maarufu nchini Mwajuma Thabiti ' Mwajuma jimama' akifanya vitu vyake mbele ya mwimbaji wa bendi ya Mashauzi Classic, Isha Ramadhani wakati bendi hiyo ilipofanya onesho lake katika ukumbi wa TCC Chang'ombe Dar es salaam pich

Friday, February 15, 2013

mwanaeme mwenye mataiti aishangaza Dunia

Wednesday, May 16, 2012


Rio Ferdinand Beki aliyetoswa Euro 2012 kwa fitina
  Godlisten Shao na Mashirika ya Habari.
SIKU ya tarehe 22 Julai mwaka  2002,Rio Ferdinand alijiunga na klabu ya , Manchester United, kw amkataba wa miaka mitano na kuwa mchezaji ghali aneyecheza safu ya nyuma katika historia ya  uingereza , akichukua nafasi ya beki aliyekuwa ghali kipindi cha mwaka 2001 Lilian Thuram.
Ferdinand ambaye ni raia wa uingereza alizaliwa Novemba  7, 1978 katika kitongoji cha  Peckham, mjini London, nchini England,na ni mchezaji anayecheza nafasi ya nyuma katika klabu ya Manchester United mpaka sasa na amekuwa mchezaji wa kulipwa kuanzia mwaka 1997.
Beki huyo ambaye alihamishwa kwa ada ya pauni milioni ishirini za uingereza na kuifanya klabu yake ya awali ya leeds kumtangaza kuwa inamuuza mchezaji huyo kwa ka zaidi ya pauni milioni thelasini.  
 Leeds United baadae ilichukua kiasi hicho chapesa zake za awali kama na kusaidia timu hiyo ambayo ilikuwa na tatizo la kiuchumi kipindio hicho, na kufanya Ada kamili ya kumuhamisha mchezaji huyo kwenda Manchester United kuwa Pauni milioni 33.
 Ferdinand ambaye alionekana ayuko vizuri kimchezo mara baaday kucheza chini ya kiwango katika mchezo wa klabu bingwa barani ulaya mchezo uliozikutanisha timu ya    Manchester United na Real Madrid 
Mwaka  2003, alishindwa kufika mahabara kwa ajili ya vipimo vya kugundua kama anatumia dawa za kuongeza nguvu au lah ,hali hii ilimtokea pale aliposahau kutokana nakuwa na harakati nyingi za kuhama makazi yake ya zamani nakuhamia makazi mapya na baadae kuendelea na shughuli zake zingine.
 Hali iliyosabaisha kamati ya nidhamu ya chama cha soka nchini Uingereza  FA kumtoza faini ya kutocheza msimu mzima wa ligi na klabu yake kulipa faini ya Pauni 50,000.
Hari ilifanya klabu yake Manchester United kukata rufaa kw amadai ya kuwa ameonewa kwani mchezaji mwengine kutoka Manchester City ,Christian Negouai, alitozwa faini ya Pauni 2,000 kwa kutokwenda kupima.
Ingawa ,Rais wa  FIFA Sepp Blatter alitupilia mbali rufaa hiyo kwa kusema kosa la Ferdinand alifanani na la Negouai ambaye yeye alichelewa kupima kwa sabau ya tatizo la foleni ya magari hivyo alionesha nia ya kutaka kwenda kupima wakti yeye aligoma kwenda kupima kwa sabau zake binafsi nakumuongeze aadhabu ya miezi 12 mingine.  
Ferdinand ambaye aliweza kutwa taji la ubingwa wa ligi ku kwa mara ya kwanza akiwa na klabu ya Manchester United na kupata medali ya   Carling Cup 2006, na kufuatiwa ushidi wa pili katika kipindi cha 2003 na  2005 FA Cup.
Mnamo 14 Desemba  2005, katika mchezo dhidi ya Wigan Athletic, Ferdinand aliweza kushinda bao lake la kwanza akiwa na United , katika mchezo ambao walishinda bao  4–0 . hili lilikuwa goli la kwanza mara baadaya mika mitatu akiwa  Old Trafford.
Baadae akafuatiwa na goli la nguvu la kichwa amabalo alifunga wakati wa mechi dhidi ya   West Bromwich Albion.na baade akafunga bao dakika za mwisho katika mchezo dhidi ya mahasimu wao  Liverpool mchezo uliopigwa katika dimba la  Old Trafford,na ndio lilikuwa goli muhimu kwa United mpaka leo .
Baada ya kuonyesha kiwango kikubwa katika ligi aliweza kuchaguliwa kwenye kikosi bora cha msimu wa ligi kuu ya uingereza cha mwaka  2006–07.
Ferdinand alianza vizuri msimu wa ligi wa  2007–08, kuwa kati ya mabeki wakutegemewa wa Man United ukilinganisha na hap awali alipojiunga na klabu hiyo na kuweza kupachika bao lake la kwanza la msimu katika mechi dhidi ya Aston Vila mchezo uliopigwa,20 Octoba 2007 katika dimba la Vila park.
   
Katika michuano ya  FA Cup mchezo wa robo fainali uliochezwa ,8marchi dhiodi ya Portsmouth, Ferdinand aliweza kukaa golini kma Golikipa baada ya kipa tegemezi wa klabu hiyo Edwin van der Sar kutoka uwanajani mara baada ya kuptwa namajeraha kwani kipindi hicho kipa wa akiba,Tomasz Kuszczak, kufungwa kwa penati na kupelekea kutolewa katika michuano ya FA CUP.
Mnamo  6 April 2008, kweney mchezo dhidi ya Middlesbrough, Ferdinand alitolewa nje kwa matatizo aliyoyapata kwenye mguu . hali hiyo ilimfanya kukosa mchezo war obo fainali ya UEFA ambao ulipigwa 9 april 2008  dhidi ya  A.S. Roma.
Baada ya United' kufungwa bao 2–1 na  Chelsea katika mchezo wa ligi kuu  April 2008 Ferdinand, aliweza kuwa na hasira kutokana na kichapo hicho na kutoamaini kuwa timu hiyo ingeweza kupenya kwenye ukuta wa United  .
Licha ya kuhusishw ana uvumi wa kuhamia klabu ya Barcelona ya nchini ,Hispania  tarehe 16 April 2008 kati ya  Michael Carrick na  Wes Brown, Ferdinand kw apamoja walikubaliana kusaini mkataba mwingine wa miaka mitano kuendelea kucheza United  mkataba amabo uligharimu Pauni milioni 130,000 kwa wiki na mkataba huo utamuweka mchezaji huyo katika timu hiyo ya mashetani wekundu mpaka 2013,mkataba amabao ulisainiwa15 Mei 2008.
Baada ya hapo tarehe  21 Mei 2008, Ferdinand alitajwa kuwa kama nahodha mpya Manchester United  katika mchezo wa klabu bingwa barani ulaya mchezo uliwazikutanisha Manchester United na  Chelsea. Na kufanikiwa kuchukua kombe akiwa na wachzaji wakongwe kama  Ryan Giggs, na  Gary Neville.
Ferdinand ambaye kwa sasa ataweza kuwemo kwenye kikosi cha uingereza kinacho shiriki michuano ya Euro 2012 kutokana kocha mpya wa timu hiyo Roy Hodgson kuhofia timu kushindwa kufanya vizuri katika safu ya nyuma kutokana wailihao kuwa katika ugomvi wa muda mrefu.
Hata hivyo mchezaji huyo ajazungumzia chochote ju ya mahamuzi ya meneja huyo mpya ambaye ameonekana kutegua kiwango hicho.
mwishooo
 
Robin van Persie mkali anayesubiriwa  kwa hamu Man City  

Godlistern Shao na Mashirika ya habari
Mashabiki wengi wa klabu ya  Arsenal wamekuwa wakimuona mshambuliaji wa Klabu hiyo Robin van Persie  kuwa ni mchezaji wa kudumu katika klabu hiyo tangu aliposaini kuchezea klabu hiyo mwaka 2004 na ni mbadala wa mshambuliaji wa kidachi  Dennis Bergkamp ambaye alitandika daluga katika masuala ya soka   
Ingawa mshambuliaji huyo amekuwa akisumbuliwa na majeruhi kadhaa marakwa mara kiasi cha kufanya mshambuliaji huyo kucheza kwa kiwango kilichodhaniwa pindi alipokuwa kijiunga na washika bunduki hao wa London.
Pamoja namatatizo yote  yaliyomkuta mchezaji  van Persie bado ameonekana kuweka mguu wake kuwa ndio biashara pekee katika maisha yake mara baada ya kuwa mshambuliaji wa kutumainiwa peke     yake akichukua nafasi ya Emmanuel Adebayor ambaye aliondoka The Gunners na kwenda kujiunga na Man City.

Robin van Persie amabye ni raia wakidachi alizaliwa Agosti 6,1983 katika Mji wa Rotterdam nchini Uholanzi  ambako ndiko alikulia na maisha yake mpira yalipoanzia.
Van Parse amabye kwa sasa anaicheze kalabu ya Arsenala huku akiwa amebakiza mwaka mmoja kumalizika kwa mkataba wake amekuwa yuko njia panda mraa baada ya Mabingwa wapya wa ligi kuu ya Uingereza Man City kumtangazia dau la kung’oa katika klabu hiyo.
Kabala ya kuchezea Arsenal Van Parsie alipata kuchezea klabu ya Feyenoord ya nchini Uolanzi kwa kipindi cha miaka mine kuanzia 2001 hadi 2004 na baade kujiunga na washika bunduki wa London.

 

Van Persie ambaye alikimbia kutoka kwenye familiya yao amabpo kipindi hicho mama yake alikuwa anafanya kazi ya kupaka rangi na baba yake alikuwa mchongaji wa vinyago huko Uholanzi 
Akiwa na umri wa miaka  14 alijiunga na timu ya vijana ya Uholanzi lakini baade alichwa na timu hiyo kutokana na kushindwa kuelewana na makocha wake na kuendelea kubaki kuichezea klabu yake ya Feyenoord. 
Baadae alionekana kuwa na kiwango cha hari ya juu na kuwa mchezaji wa kuanza katika kikosi cha kwanza cha Feyenoord kutokana na matatizo ya kumia marakwamara yalimfanya awe mtu wa kuanzia kikosi  B.
Ingawa watu wengi waliamini kuwa Van Persie  amegombana na kocha wake  Bert van Marwijk ndio sababu ya kumfanya mchezaji wa akiba katika ,pia kocha aliweza kumrejesha mchezaji huyo nyumbani mara baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu katika mchezo wa fainali za UEFA mwaka 2003 dhidi ya Real Madrid. .
 Baada ya kufanikiwa kupachika magoli nane katika msimu wa kwanza huku akitokea benchi aliweza kumshawishi kocha wake katika msimu uliofuata wa mwaka 2003-2004 kuwa ndie mchezaji anayeweza kuanza.
Baada ya kucheza kweney klabu hiyo bil;a kuwa na mafanikio yoyote nyota huyo aliweza kuuzwa katika klabu ya Arsenal ambayo alionyesha kuwa na mapenzi nayo siku za nyuma kabla ya kuuzwa katika klabu hiyo.

 

Mwaka 2004 Van Persie aliweza kusaini mkataba wa miaka mine na klabu ya Arsenal  na kufanikiwa kuwa mmoja wa wachezaji waliocheza katika kikosi kilichochukua kombe la FA mwaka 2005 kombe ambalo alijaweza kuchukuliwa tena na klabau hiyo.

Mara baada ya mkataba wake kumalizika mwaka 2009 mshambuliaji huyo aliweza kumshawishi bosi wake Arsene Wanger kumpa mkataba mpya wa miaka minne  ambao utamalizika mwakani
 Mshambuliaji huyo ambaye aliweza kumfurahisha bosi wake pindi alipokuwa uwanjani kutokana na stairi yake ya mchezo lakini alikuja kujitia doa pale alipopatiw akadi nyekundu kwenye mechi kati ya Arsenal na Southampton.
 Maisha yalibadilika na kuw amtu mwneye furaha akiwa na Gunners pale alipoweza kufunga goli pekee la kichwa na kupewa tuzo kuwa goli pekee la msimu katika ligi kuu ya England.
 Mshambuliaji huyu ambaye alikuwa kaichez anafasi ya winga lakini alicaha jkucheza nafasi hiyo mara baada ya kubadilishwa na kocha wake Arsene Wanger mara baada ya kuona kuwa awezi kufua dafu mbele ya Thierry Henry ambaye alikuwa katika kiwango cha juu sana.
 Licha ya kuwa na mafanikio yote hayo mshambuliaji huyu wa kidachi alionekana kuw ana matatizo ya majeruhi mara kwa mara huku akiwa na tatizo la Goti na henka vitu vilivyo msumbua kila mwezi.

 

Van Persie aliweza kuonyesha uwezo wa hali ya juu katika timu yake ya Tiafa kuanzia mkwa 2006 katika mashindano ya kuwania kufuzu fainali za kombe la Dunia mara baada ya kushinda mechi dhidi ya Roamania na Finland.
Pia aliweza kucheza mechi zote nne katika fainali za kombe la Dunia 2006 kama kiungo wa kutumainiwa wa Uholanzi ,pindi timu hiyo ilipopangwa na timu ngumu kama Argentina na Ivory Coast.    
Miaka miwili badae katika michuano ya Euro 2008, Van Persie alifanikiwa kushinda magoli mawili na kuifanya timu hiyo kutinga atua ya robo fainali kabla ya kutolewa na Urusi.  .
Akiwa anacheza kama winga na mshambuliaji katika timu yake ya Taifa  , Van Persie alioweza kupewa heshima ya hali ya juu na mashabiki wa mpira wan chi hiyo hasa kwa ufundi wake wa kutengeneza magoli akiwa na klabua yake na timu ya Taifa .
Haliweza kuisadia timuyake kutinga hatua ya fainali katika michuano ya kombe la Dunia ya mwaka  2010 kabala ya kufungwa na mabingwa wa kombe hilo kwa sasa Hispania na laiweza kufunga bao moja katika michuano hiyo bao alilofunga kwenye mechi dhini ya Cameroon.
Mchezaji huyu ambaye ameonekana kufanya makubwa katika msimu huu uliomalizika katika ligi kuu ya uingereza kwa kuweza kutwa tuzo ya kiatu cha dhahabu tuzo ambayo ajawahi kuipata maishani mwake.

Van persie ambaye ameweza kufunga mabao 30katika msimu huu na kufikia rekodi iliyowekjwa katika klabu ya Arsenal na mkongwe Thierry Henry msimu wa 2003/04 na pia aliweza kutwa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka tuzo inayotolewa na chama cha waandishi wa habari nchini Uingereza.

Hata hivyo yeye ajaonyesha nia ya kuhama klabu yake ya Arsenal licha ya dau nono alilotangaziwa na Man City huku wakala wake akimshawishi kukubalina na hofa hiyo ambayo ni mara tatu ya mkataba wake wa awali.