Sunday, May 6, 2012

HILDA AKIKABIDHIW AZAWADI YAKE YA LAPTOP NA MGENI RASMI


HILDA NDIYE RED'S MISS USTAWI 2012

 MUIGIZAJI MKONGWE KWENYE TASNIA YA BONGO MUVI ,SINTA A.K.A J LO WA BONGO AKIWA NA WANAKAMATI KUJADILI MSTAKABALI WA SHUGHULI WAKATI REASOL
 WATU KADHAA AMBAO NI WANAFUNZI WA CHUO CHA USTAWI WAKILA BATA KUSUBILI MCHAKATO WA SHINDANO LA RED'S MISS USTAWI
 DULLY SYKES BABA TORIANO AKITOA SHOO WAKATI WA SHINDANO
 MAJAJI WA SIKU HIYO WANA HABARI ALFRED LUCAS ,VICKY KIMARO NA JAMES RANGE WAKICHAKALIKA KUJUMLISHA MATOKEO
MKURUGENZI WA JIRUSHEWEEKEND BLOG HUMPHREY SHAO AMABAYE AMEVAA SHATI LA BLUU AKIWA NA WADAU WENGINE KUTOKA USTAWI WAKIFATILIA SHOO KWA UMAKINI MKUBWA.

Thursday, May 3, 2012

AND 1 ilivyowakuna wabongo last week





GRAND MALT YAZINDUA TUZO ZA “EXCEL WITH GRAND MALT 2012”.

Kinywaji maarufu cha Grand Malt leo kimezindua tuzo kwa wanafunzi wa elimu ya juu zijulikanazo kama “Excel with Grand Malt”, huu ukiwa ni mwaka wa pili kwa tuzo hizi kutolewa.

Akizungumzia tuzo hizo, meneja wa kinywaji cha Grand Malt Bi. Consolata Adam alisema; Excel with Grand Malt ni tuzo za aina yake ambazo zimelenga kutambua na kuthamini mchango wanaoonesha wanafunzi katika fani mbalimbali nje ya masomo ya darasani. Tunatambua kuwa kazi kubwa ya mwanafunzi anapokuwa chuoni ni kuhudhuria vipindi vya darasani na kupata elimu, bali tunapenda pia kuwatambua wale wachache ambao wanakwenda mbali zaidi na kufanya mambo ya maendeleo katika mazingira yao ya chuo.

Tuzo hizi zilianzishwa mwaka jana ambapo tuliweza kufika katika mikoa sita na kufikia vyuo vipatavyo ishirini. Kwa mwaka huu mchakato utaanza mwezi Aprili hadi June, na Mikoa itakayohusika ni pamoja na Dar es salaam, Morogoro, Iringa, Dodoma, Kilimanjaro na Mwanza ambapo vyuo vipatavyo 21 vitashiriki. Kama ilivyokuwa mwaka jana, fani zitakazoshindanishwa ni Ubunifu (Innovation), Michezo (sports), Utamaduni na burudani (Culture & Entertainment) na Mazingira na Huduma za jamii (Environment & social responsibilities). Kama ilivyo ada, washindi katika fani hizi watajipatia zawadi mbalimbali toka Grand Malt ikiwa ni pamoja na pesa za kununulia vitabu na vyeti vya ushindi.

Kwa sasa natangaza rasmi kuwa tunzo hizi zimezinduliwa rasmi na mkoa wa kwanza utakuwa ni Morogoro ambapo tunatarajia kufanya tamasha kubwa kwenye viwanja vya chuo kikuu cha SUA siku ya jumamosi kisha jumapili tutafanya tamasha la ufunguzi kwenye Viwanja vya chuo cha CBE mkoani Dodoma na kutakuwa na burudani zitakazoongozwa na nguli wa Hip hop nchini Joh Makini ,zawadi nyingi na zaidi kutakuwa na GrandMalt baridi na hakutakuwa na kiingilio chochote. Alisema Bi. Consolata.

Akielezea umuhimu wa Tuzo hizo, meneja masoko wa TBL Bw. Fimbo Butallah alisema; Tunafurahi sana kuona vyuo vyote vilipokea tuzo hizi kwa furaha kubwa, hii ni kwa sababu wanatambua umuhimu wake. Kupitia tuzo hizi ambazo zitakuwa zikitolewa kila mwaka, Grand Malt inatoa changamoto kwa vijana walio vyuoni kuona umuhimu wa kujituma na kufanya mambo mengi na makubwa zaidi ya kufaulu mitihani ya darasani tu. Tunaomba viongozi wa serikali za wanafunzi na viongozi wa vyuo kuendelea kutoa ushirikiano kama walivyofanya mwaka jana ili kuleta ufanisi zaidi katika tuzo za mwaka huu. Kama ilivyo kawaida, utaratibu utakuwa ule ule ambapo wanchuo watapendekeza majina ya vijana wanaoamini kuwa wamefanya mambo makubwa ndani ya vyuo vyao katika tasnia zilizotajwa hapo awali, kisha kufuatiwa na kipindi cha kupiga kura ambapo washindi watapatikana. Alimaliza Bw. Butallah

Kwa upande wake meneja mahusiano na mawasiliano wa Tbl Bi Edith Mushi Alisema GrandMalt kwa kuzingatia umuhimu wa juhudi za serikali katika kuhamasisha jamii kutunza mazingira kwa kupanda miti mwaka huu Grand Malt itafanya zoezi maalum kwenye kila chuo kwa kupanda miti imara itakayosaidia kutunza na kuboresha mazingira ya vyuo hivyo ili kuandaa mazingira bora ya kusomea ya wanafunzi wa sasa na wa vizazi vijavyo ambapo mkoani Dodoma zoezi hilo litafanyika jumatatu May 07,2012 katika vyuo vya UDOM na CBE tawi la Dodoma na Mkoani Morogoro zoezi hilo litafanyika kwenye vyuo vya SUA na Mzumbe siku ya jumanne May 08,2012 asubuhi, kisho zoezi hilo litaendelea katika mikoa ya Iringa,kilimanjaro,Mwanza na Dar Es Salaam.

Wednesday, May 2, 2012

Eleven killed in Egypt clashes over army rule



 Photo



CAIRO (Reuters) - Eleven people were killed and more than 160 wounded near Egypt's Defence Ministry on Wednesday after armed men assaulted protesters demanding an end to army rule, prompting two Islamist candidates to suspend their presidential election campaigns.
Unidentified "thugs" armed with guns or batons attacked demonstrators who included hundreds of ultraconservative Salafi Islamists protesting at the exclusion of their candidate from this month's vote, state news agency MENA reported.
The violence casts a deep shadow over the presidential election due on May 23 and 24, with a run-off in June, and highlights the fragility of Egypt's transition to democracy, which has been punctuated by violence and political bickering.
Security and medical sources gave a toll of 11 dead and over 160 wounded in the clashes outside the Defence Ministry in central Cairo's Abbasiya district. The fighting raged on unabated through the morning, but subsided in the afternoon.
"Where is the army? Why are they not stopping these people?" cried a bystander as the violence persisted. Shots rang out as young men dashed back and forth across debris-scattered streets, hurling rocks, glass and petrol bombs.
"Down, down with military rule," yelled protesters.
Wounded men were hauled away as others filled bottles with petrol while shots rang out. A Reuters witness saw some combatants carrying guns and one with a sword.
The army sent in extra vehicles and troops, but pledged in a statement not to disperse peaceful demonstrators.   Continued...

SERIKALI YATAKIWA KUACHA KUINGILIAKAZI ZA TUME YA KATIBA


SERIKALI imetakiwa kuacha kuiingilia kazi za Tume ya Mabadiliko ya Katiba na badala yake iwape uhuru wa kufanyakazi hiyo kwa ufasaha na kuandaa katiba wanayoitaka wananchi.

Hayo yamesemwa jana na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Sinde Warioba wakati wa uzinduzi wa tume hiyo na kukabidhiwa jengo la kufanyia kazi hiyo.

Mwenyekiti huyo amesema isije ikafika wakati tume ikashindwa kufanyakazi ipasavyo kwa sababu ya maslahi ya watu wachache kwani kufanya hivyo itakuwa ni kuingilia uhuru wa tume na kuwanyima haki wananchi ya kupendekeza katiba waipendayo.

“ Nyie mliotuchagua tunaomba tafadhari mtupe nafasi isije ikaja leo au kesho mnaanza kutusumbua tupindishe kilichopo kwa madai mna watu wenu ndani ya tume naomba ieleweke kuwa tume si ya kikundi fulani ni ya wananchi  hivyo hatutaki kufanyakazi kwa presha ya watu fulani,”amesema Warioba.

Amesema kazi waliyopewa ni ngumu hivyo wana imani serikali itawapa ushirikiano wa kuwafikia wananchi wote ili waweze kutoa maamuzi yao na kuandaa katiba yenye maslahi ya umma.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amesema Serikali imeandaa mazingira safi ya kuhakikisha tume hiyo inafanyakazi kwa ufanisi zaidi.

Amesema  kuwa serikali imetekeleza ahadi aliyoitoa rais alipoiapisha tume hiyo Aprili 13 mwaka huu ya kuhakikisha tume hiyo inafanyakazi kwenye mazingira stahiki yenye ulinzi wa kutosha, usalama , na vifaa vya mawasiliano na vya kutunzia kumbukumbu vya kisasa.

Pia serikali imenunua magari 30, kwa ajili ya tume hiyo ili kuweza kuwafikia wananchi kwa urahisi na kuepuka vikwazo katika utendaji wa kazi hiyo na fungu maalum la fedha limetengwa..

“ Serikali imedhamiria kuipa uhuru tume, kuwapa sehemu nzuri ya kufanyiakazi pamoja na nyumba za kuishi wana tume ambao wanatoka nje ya Dar es Salaam,”amesema Sefue.

Naye Waziri wa Katiba na Sheria, Cellina Kombani  amesema umuhimu wa mabadiliko ya katiba ya nchi ni mkubwa na wananchi wana matumaini na tume na ndiyo maana ilipotangazwa hakuna malalamiko yaliyojitokeza.

Ameitaka tume hiyo ijipange vyema ili kuhakikisha inatoa elimu ya katiba iliyopo ili wananchi waweze kutoa maoni ya katiba waipendayo kwani muundo wa katiba hiyo ni jambo nyeti na lenye kuleta msisimuko.

“ Nina imani amani  itatawala na uwazi, kwani mchakato huu ni wa kuboreha mazuri, kuondoa mapungufu pia ni kujipima tulikotoka na tuendako kwani nia si kuvunja umoja wetu bali mawazo ya wananchi yataheshimiwa, “amesema Kombani.

Kombani ameongeza kuwa tume hiyo ndiyo nguzo ya mchakato wa katiba mpya huku akisisitiza kufanikiwa au kutofanikiwa kutatokana na tume hiyo kutekeleza majukumu yao kwa kuwashirikisha wananchi bila ubaguzi.

“ Kazi hii inahitaji ushirikiano zaidi nafahamu kuna kipindi mtakwazika na kutamani kuimbia kazi hii lakini mkiwashirikisha wananchi mtafikia muafaka na hatimaye tutapata katiba inayostahili,”amesema Kombani.


Wakati huohuo, Waziri wa Katiba na Sheria Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Abubakari Khamis Bakari amesema tume imepewa kazi ngumu ya kuwaelimisha wananchi kwani wengi wao hawajui maana ya muungano.

Amesema ili katiba iwe yenye kukidhi haja ni muhimu wananchi wakapewa fursa ya kutoa maoni ambayo yataisaidia tume hiyo  kurahisisha kazi yao.


Amewatahadharisha wananchi kuacha kutumia mchakato huo kama njia ya kuibomoa nchi  na badala yake fursa hiyo itumike kuunda katiba yenye mantiki na inayokubaliwa na watu wote.

Hata hivyo hafla hiyo iliingiliwa na dosari baada ya jenereta lililopo jirani na jengo hilo kulipuka jana asubuhi na kusababisha umeme katika jengo hilo kukatika  hivyo kufanya hafla hiyo kuendeshwa bila vipaza sauti.

mwisho

BOXING   MAWE   NGUMI
V/S   
JAMES MOKIWA V/S RAMA KUMBELE
UBINGWA WA T.P.B.O
MAPAMBANO YOTE NI KAMA IFUATAVYO;-

RAMADHAN KUMBELE(DAVIS CORNER-TANDIKA) v/s JAMES MOKIWA(CHICHI MAWE GYM

KARIM SALUM”paquiao” v/s ANORD YOHANA”biggie’(CHICHI MAWE GYM)

DOI MIYEYUSHO(CHICHI MAWE GYM) v/s JUMANNE MTENGELA (MABIBO GYM)

JAFAR MAJIA”mr nice” v/s DAUD MUHUNZI (MSISIRI GYM)
DOTO KIPACHA  V/S  JOSEPH RICHARD
FRANCIS SUBA v/s JOSEPH PITER”mbowe’-(MKONO WA CHUMA)

SADAT MIYEYUSHO(CHICHI MAWE GYM) v/s SWEDI HASSAN(dame gym-nomo camp)

                                             MARTIN RICHARD(BigRight Boxing) v/s YOHANA THOBIAS(CHICHI MAWE GYM

HEAVY WEIGHT
ANORD "BIGGIE V/S KARIM "PAQUIAO"KIINGILIO;
KAWAIDA TSH 4,000/=
VITI MAALUM TSH 6,000/=JUMAPILI kuanzia saa 10jioni.20/5/2012 VIJANA HALL-KINONDONINJOO USHUHUDIE MAWE YA NGUVU MABONDIA WAMEJIANDAA VYA KUTOSHA NA WAMEAHIDI LAZIMA MTU ALALE.
PIA KUTAKUWA NA MAONESHO YA WAJASILIAMALI,ASASI ZA KIJAMII NA KIUCHUMI ZITAKUWEPO KUELEZEA KAZI ZAO
V/S   
V/S   
KUTAKUWEPO NA PROJECTOR ITAKAYOONESHA MAPAMBANO YA FRANCIS MIYEYUSHO
YAKIWEMO NA MBWANA MATUMLA i,ii & iii NA MENGINE YA HAPA NA ULAYA
V/S