Jirusheweekend
Mafanikio yanahitaji uvumilivu Mdau wa jirushe ni mwandishi wa habari kutoka New Habari Anapatikana kwa namba 0716 772231 ,Email -humphreyshao@ymail.com/shaohumphrey58@gmail.com kwa mahitaji yoyote ya kuhabarisha ,makala,matukio, picha za harusi na kuandaa event mbalimbali nitwangie
Saturday, January 25, 2014
Dk. Ali Shein kumnadi mgombea Kiembesamaki
Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki-Januari 26.
Dk. Ali Mohamed Shein, atakuwa mgeni rasmi na kumandi Mahomoud Thabit Kombo
Dk. Ali Shein kumnadi mgombea Kiembesamaki
Na Andrew Chale, Zanzibar
MAKAMO Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar
ambaye pia ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi,
Dk. Ali Mohammed Shein kesho Januari 26, anatrajiwa kumnadi mgombea wa Uwakilishi wa
jimbo la Kiembesamaki, Mahmoud Thabit Kombo, katika uchaguzi mdogo unaoendelea
kwenye jimbo hilo.
Katika tarifa yake, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai
Ali Vuai alisema kuwa, Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk Shein atakuwa mgeni rasmi kwenye mkutano
huo wa nne wa hadhara kwenye kampeni hizo zinazoendelea.
Na kuongeza kuwa, Dk. Shein atawahutubia wananchi sambamba
na kumnadi, Mgombea huyo wa nafasi ya uwakilishi, Mahmoud Thabit Kombo,
anayewania nafasi hiyo kwenye jimbo hilo la Kiembesamaki.
Vuai aliwataka wananchi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi
ilikusikiliza sera na ilani za chama hicho katika utekelezaji wake
iliwakichague chama cha Mapinduzi kwa misingi imara ya kuwaletea maendeleo.
Aidha, kwa upande wake,
Mahmoud Thabit Kombo aliwaomba wananchi wa jimbo hilo, kumpigia kura
hiyo Februari mbili, ili akawawakilishe kwenye Baraza la Wawakilishi.
“Nawaomba Wanakiembesamaki, kutumia fursa ya kipekee ya
kunichagua ilikuweza kuwawakilisha kwenye BAraza, hakika chama chetu ni sikivu na daima kipo na
wananchi katika kuwatetea na kuwaletea maendeleo” alisema, Mahmoud.
Kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Kiembesamaki, zilianza
Januari 21, ambapo zinatarajia kumalizika Februari Mosi, mwaka huu huku
wananchi wakitarajia kupiga kura ya chaguzi huo, Februari mbili.
Mwisho
Thursday, January 23, 2014
EU YAPIGA JEKI WATOTO TANZANIA
EU1: Mkuu wa Ushirikiano
kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya Tanzania Eric Beaume (kushoto)
akibadilishana hati ya makubaliano ya Mradi wa Kupambana na Ukatili kwa
Watoto na Mwakilishi wa UNICEF hapa nchini Jama Gulaid, kutoka kushoto
ni Mkurugenzi Mkazi wa Plan International Tanzania Jorgen Haldorsen,
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid na Mkurugenzi Mkazi
wa Save the Children International Tanzania Steve Thome wakishuhudia
makabidhiano ya hati hiyo jana jijini Dar es Salaam
U4: Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Seif Rashid (aliyeko mstari wa mbele katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa Mradi wa kutokomeza Ukatili kwa Watoto mara baada ya kutia saini msaada kutoka Umoja wa nchi za Ulaya jana jijini Dar es Salaam.
U4: Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Seif Rashid (aliyeko mstari wa mbele katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa Mradi wa kutokomeza Ukatili kwa Watoto mara baada ya kutia saini msaada kutoka Umoja wa nchi za Ulaya jana jijini Dar es Salaam.
MKUTANO MKUU WA NGUMI ZA KULIPWA
MKUTANO MKUU WA NGUMI ZA KULIPWA
Siku ya
terehe 1 ya mwezi wa pili katika ukumbi wa vijana hall kinondoni KUANZIA SAA
TATU NA NUSU ,kutakuwepo na mkutano mkubwa wa wanamasumbwi wote ulioitishwa na
orgnaizesheni ya ngumiza kulipwa Tanzania (TPBO) kwa lengo la kuwakutanisha mapromota
wote,mabondia na makocha wa ngumi wote
kwa lengo la kujadili ngumi za kulipwa zinapoelekewa,kujuana na kuelimishana
sheria za ngumi za kulipwa zinavyotumika
kinyume na sasa ,sheria nyingi zinafungiwa macho na kutumia uzoefu zaidi
kuendesha mgumi nchini. Mkutano huo
ulioitishwa na Rais wa TPBO bw Yasin
Abdallah akishirikiana na Ibrahim kamwe
na Mapromota wa ngumi chini ya ufadhili wa kitwe Traders unatarajiwa kuwa mkutano wa kwanza kuwakutanisha mapromota wote pamoja na mabondia wa ngumi za kulipwa wa hapa nchini ili kuboresha ngumi
na kuhamasisha wadhamini na makampuni wajitokeze kuudhamini mchezo huo ,ambao
ndio mchezo unaoliletea mataji na sifa Tanzania
katika medani za kimataifa lakini hauna udhamini wowote ,mpaka sasa ni mchezo ambao unaojiendesha wenyewe kwa nguvu za wadau wachache wachovu na mabondia wenyewe ambao uwezo wao ni mdogo
sana kukikidhi matakwa kamili ya mchezo wenyewekam ilivyo kwa wenzetu,ni mchezo
ambao una huduma nyingi zinazohitaji
nguvu ya wadhamini ili uendelee kuboreka
zaidi.
Akizungumza
na vyombo vya habari katibu wa ngumi za kulipwa nchini bw Ibrahim kamwe ,
amesema imewaalika viongozi wa baraza la michezo (BMT), na viongozi wengine
wote wa ngumi za kulipwa watakuwepo kama vile Emmanuel mlundwa,names kavishe, makaranga,Onesmo ngowi,kinyogoli, matumla, Zuwena kibena(mama zugo) na viongozi wadau
wa karibu na ngumi wamealikwa kuhudhulia mkutano huo ambao utafanyika Siku ya
terehe moja ya mwezi wa pili katika ukumbi wa vijana hall kinondoni. hivyo kamwe
alimaliza kwa kuwaomba kila anaejijua kuwa yeye ni bondia wa ngumi za kulipwa
na promota wangumi ahudhurie bila kukosa
mkutano huu muhimu sana kwa wamasumbwi ya nchi yetu.
mapambano ya ngumi mbagal azak hem
Bondia Abuu Abas kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Abdul Zugo wakati wa uhamasishaji wa tuzo za PSPF Boxing Award zilizofanyika katika viwanja vya Zakhem Mbagala Dar es salaam tuzo hizo zinafika tamati january 25 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Zugo alishinda kwa K,o ya raundi ya pili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Wednesday, January 22, 2014
ASUTWA USIKU KUCHWA KWA KUMNYANYASA MDOGO WAKE WA MIAKA SABA
Subscribe to:
Posts (Atom)